1.Libya NATO walienda kuweka no fly zone kwa idhini ya UN kulinda raia waliokuwa wanauwawa na Gaddafi, Yemen wako kwenye civil war, Afghanistan chini ya Taliban walikuwa wanahifadhi magaidi wa Al Qaeda walioua watu 3000 wa US September 11.
2.Asilimia kubwa ya Ngano kutoka Urusi na Ukraine ndio inayoliwa Africa hasa Misri, Nigeria,Algeria na Morocco. Fahamu tu kwamba Ufaransa, Ujerumani na Poland ni wazalishaji wakubwa wa Ngano na wanauza kiwango kikubwa nje ya nchi zao, UK inazalisha ngano ya kutosha kwa nchi yake. Urusi inaagiza sehemu kubwa ya matunda kutoka EU.
3.Mambo ya US ku support madikteta ilitokana zaidi na USSR kulazimisha Ukomunisti kwenye maeneo mbalimbali duniani, ile ilikuwa vita baridi ambayo US naye alitumia hadi msaada wa "shetani"(nikirejea maneno ya Membe) kupambana na giza la Ukomunisti.
Leta Hoja.