ASFC: Yanga Vs Simba lazima mmoja atoke analia leo CCM Kirumba, hakuna sare

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Yanga na Simba zinatarajiwa kukutana katika Nusu Fainali ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) 2021/22, leo Jumamosi Mei 28, 2022 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, huo ni mchezo wa mwisho kwa timu hizo kukutana msimu huu.

Katika mechi zote mbili za Ligi Kuu Bara msimu huu hakuna mbabe, zilimalizika kwa sare, mchezo wa leo unaoanza saa 9:30 Alasiri ni lazima ushindi upatikane, hivyo lazima upande mmoja wacheke wengine wahuzunike.

Unadhani ni mashabiki wa timu gani watatoka vichwa chini baada ya matokeo pale Uwanja wa CCM Kirumba?

=====================

Kinachoendelea muda huu mitaa ya Kirumba jijini Mwanza.


 
kwa nyomi la mashabiki la simba leo hapo kirumba uto sijui mnatokaje leo
 
Wale tuliowahi chance ktk vilima vya kirumba na kitangiri ili tushuhudie hii mechi bure naomba tujuane hapa πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…