kaputula
Senior Member
- Mar 29, 2012
- 173
- 226
Kuna wasomi wanawake Kikwete amewabeba awamu yake ya urais kutokana na harakati zake alipokua kiongozi wa wanafunzi chuo kikuu cha Dar es Salaam. Mtu kama Asharose anajua sana kingereza, ni msomi mzuri wa sheria lakini misimamo gani ya kisiasa anayo inatia mashaka.
Kwa mimi ninayeamini katika msimamo wa kimapinduzi na wa kijamaa sijaona ubora wowote wa Asharose hadi kila mara tunaona jina lake tukiletewa kwa uongozi nchini. Mimi naona ni mambo ya kishikaji tu.
Alipokuwa waziri wa nje zaidi ya umahiri wake kwenye kingereza sijaona kimsimamo cha maana kwake. Awamu ya kikwete ilipomalizika akawa umoja wa mataifa akiwa naibu katibu mkuu kazi ambayo mwisho alitimuliwa kwa kukosa weledi. Ndio ukweli japo tunafichwa nchini.
Enzi ya JK ikimalizika tukaona akiwekwa kugombea urais huku msimamo wake kisiasa haueleweki kuhusu siasa za kutetea umma wa wananchi. Kuingia tu mama jina lake likaibuka tena balozi uingereza.
Sasa tena huku umri umeenda tunaona eti kapewa katibu mkuu wa ccm. Utafikiri nchi hii hakuna wenye uwezo wengine na umri mdogo.
Katika huu utawala wa mama tumeona watu wa mlengo wa kimagufuli wakitengwa na kupigwa teke.
Mlengo ambao ndio sahihi kwa maendeleo ya nchi hii. Tumeona kundi la mtandao la wale tunawaita wahuni unaodhaminiwa na mfanyabiashara Rostam Azziz ukirejea, mtu ambaye kashfa karibu zote kubwa za uhujumu uchumi nchini zimemuhusu.
Mama mwanzo alisafiri na huyo mtu hatari kwa uhuru wetu eti ni mwekezaji mkubwa. Huyo mtu taarifa tunazoona huko nje ni jasusi wa wamarekani. Nchi haiwezi kuendelea kwa kukubali wanamtandao wa Rostam Azziz kuongoza nchi.
Watanzania tuwe wamoja kurejesha nchi mkononi mwa wazalendo ili tupange maendeleo kwa namna ya kufaidika na uchumi wa nchi yetu.