RugambwaYT
JF-Expert Member
- Jan 11, 2014
- 1,397
- 1,899
Kwa kweli watu wanaonunua brand new cars (wengi tunaziita 0 km) wanafaidi saana. Yaani unakuta gari ni safi, kila kitu kiko on point, miguu imekaa vizuri, seat ni safi, rangi imetulia hakuna scratch hata moja, taa zote zinang'ara, yaani mpaka tairi ni mpya. Sasa ukute ni gari la Mjerumani kama hilo E class nililobahatika kuliona ndio usipime. That was my first time around a brand new car, ila nimegundua kwa kweli sisi tunaonunua used cars za miaka 10 iliyopita na zaidi, tunamiss vitu vingi saana.

