Asili na Maana ya Jina/majina ya sehemu mbalimbali Tanzania

Asante mkuu kwa nyongeza hiyo
 
Wakuu kwa wenyeji au wadau na wajuzi wa mambo. Je, nini asili au maana ya Jina Geita ambao ni mkoa kwa sasa.
Binafsi mpaka sasa najua nadharia mbili juu ya maana au asili ya mkoa wa geita.

1-Nadharia ya Wajerumani.
-wajerumani walikuja tanzania kufanya utafiti wa madini ya dhahabu hivyo waliweka kituo maeneo hayo(kwa sasa Geita) ndipo project hiyo wakaita Gold Exploration In Tanganyika(GEITA) na ndipo mwanzo wa mkoa huo kubaki ukitumia jina la project hiyo ya Geita.

2- Nadharia ya kabila
Kwa upande wa pili Geita imetokana na neno la kisubwa(kwa nadharia moja) yenye maana ya neno Keita yaani kuuwa (kwa kisubwa). Hivyo hapo zamani watu waliokuwa wakipita milimani kuingia Geita walikuwa wakifia njiani hivyo wenyeji wakawa wanasema Akabanga Keita Abhantu yenye maana Mlima unauwa wafu (kwa kisubwa). Hivyo Neno Keita wazungu walishindwa kuita Keita wakaita Geita na ndiyo ikawa mwanzo wa neno Geita.

Je, kwa wajuzi wanaweza weka hapa asili ya Neno hilo kwa kuongeza Nadharia nyingine kama ipo au watujuze nadharia ipi ndio halisi kati ya hizo?.

Cc: SHIMBA YA BUYENZE
 
Reactions: Lee
Mjerumani hawezi kuipa project yake jina la kiingereza. Namba 1 inakataa labda kama ulimaanisha uingereza
Shukurani mkuu hapo nilimanisha wajerumani wenyewe.
Pengine nadharia hiyo itakuwa haina ukweli.
 
Wazungu si ndio wamewaweka kwenye ramani [emoji23][emoji23]
 
Aisee
Aisee!Nadhani tuliwaamini sana hata Mbeya,sehemu moja kule Chunya mzungu alisema making a loss!wao wakasema amesema Makongolosi!Ndo jina mpaka sasa!
 

Makambako maana yake Madume ya Ng’ombe!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…