Asili na Maana ya Jina/majina ya sehemu mbalimbali Tanzania

Asili na Maana ya Jina/majina ya sehemu mbalimbali Tanzania

Kwa kifupi, jikumbushe pia na mbinu waliyotumia wakoloni kudhalilisha tamaduni zetu na kubadili kabisa 'mind set' za watawaliwa.

Dini, tamaduni, mila na desturi za waAfrika wazawa zikatwezwa na kuonekana kila cha mzungu ni cha maana hata kama alikosea.

Na huo ukoloni wa kifikra unaendelea hadi leo vichwani mwa waAfrika walio wengi, kuona kila cha mzungu iwe dini, lugha, tamaduni nk nk hata kama kimekosewa, kuwa ndivyo vilivyo bora na mahususi hata kama ni vibaya na havitufai!
Asante mkuu kwa nyongeza hiyo
 
Wakuu kwa wenyeji au wadau na wajuzi wa mambo. Je, nini asili au maana ya Jina Geita ambao ni mkoa kwa sasa.
Binafsi mpaka sasa najua nadharia mbili juu ya maana au asili ya mkoa wa geita.

1-Nadharia ya Wajerumani.
-wajerumani walikuja tanzania kufanya utafiti wa madini ya dhahabu hivyo waliweka kituo maeneo hayo(kwa sasa Geita) ndipo project hiyo wakaita Gold Exploration In Tanganyika(GEITA) na ndipo mwanzo wa mkoa huo kubaki ukitumia jina la project hiyo ya Geita.

2- Nadharia ya kabila
Kwa upande wa pili Geita imetokana na neno la kisubwa(kwa nadharia moja) yenye maana ya neno Keita yaani kuuwa (kwa kisubwa). Hivyo hapo zamani watu waliokuwa wakipita milimani kuingia Geita walikuwa wakifia njiani hivyo wenyeji wakawa wanasema Akabanga Keita Abhantu yenye maana Mlima unauwa wafu (kwa kisubwa). Hivyo Neno Keita wazungu walishindwa kuita Keita wakaita Geita na ndiyo ikawa mwanzo wa neno Geita.

Je, kwa wajuzi wanaweza weka hapa asili ya Neno hilo kwa kuongeza Nadharia nyingine kama ipo au watujuze nadharia ipi ndio halisi kati ya hizo?.

Cc: SHIMBA YA BUYENZE
 
  • Thanks
Reactions: Lee
Mjerumani hawezi kuipa project yake jina la kiingereza. Namba 1 inakataa labda kama ulimaanisha uingereza
Shukurani mkuu hapo nilimanisha wajerumani wenyewe.
Pengine nadharia hiyo itakuwa haina ukweli.
 
Wazungu si ndio wamewaweka kwenye ramani [emoji23][emoji23]
 
Wakuu bila shaka uzima upo. Basi nashukuru pia poleni kwa wale uzima unapelea.
Leo nimeamua kuja mbele yenu kuuliza kwa nini Wazungu tu? Naamu hii inamaana ya kuomba msaada wa majibu kwenu.
Ukifuatilia Asili au Maana ya Maneno ya majina ya maeneo mengi hapa nchini utakuta na majina hayo asili yake au maana mzungu kuhusika ndani yake.
Mifano;
1- Asili ya Neno Geita.
Geita imetokana na neno la kisubwa(kwa nadharia moja) yenye maana ya neno Keita yaani kuuwa (kwa kisubwa). Hivyo hapo zamani watu waliokuwa wakipita milimani kuingia Geita walikuwa wakifia njiani hivyo wenyeji wakawa wanasema Akabanga Keita Abhantu yenye maana Mlima unauwa wafu (kwa kisubwa). Hivyo Neno Keita wazungu walishindwa kuita wakaita Geita na ndiyo ikawa mwanzo wa neno Geita.

2- Asili ya neno Kilimanjaro
Zamani ilikuwa ikiitwa (kilima kyar'yu)kwa kabila la kichaga yaani kilima chetu. Wazungu wakashindwa kutamka (kyar'yu)yaani chetu ndo wakaanza kuita kilimanjaro mpaka likazoeleka hivyo na hapo ikawa mwanzo wa neno Kilimanjaro.

3- Asili ya neno Lukuledi mkoani Ruvuma
Lukuledi ni moja ya eneo lililopo mkoani Ruvuma asili yake ni kwamba maeneo hayo kulikuwa na mto hivyo wanawake walipenda kuoga maeneo ya mto, sasa wazungu wakipita pale wanaanza kuongea Look Ladies hivyo na sisi Wabongo tukajua Hilo eneo bila shaka ni Look Ladies hivyo kwa vile kizungu hakikueleweka wao walijua ni Lukuladi sawa na Look Ladies na hapo ikawa mwanzo wa jina hilo.

4- Asili ya Jina kolomije- Mkoani Mwanza
Kuna mzungu alikuwa anaitwa J. Hivyo kwa jinsi alivyokuwa alijitambulisha akawa anawambia call me J akimaanisha niite J(kw kiswahili), basi hilo eneo likaitwa kolomije na wenyeji walio Kuwa wakijua mzungu huyo anasema eneo hilo ni Kolomije yaani call me J.

Pia kuna maeneo mengine ambayo uwepo wake ni chanzo cha wazungu.

Je, bila wazungu tusingekuwa na majina ya maeneo yetu au kabla ya mzungu sisi hatukutambua umuhimu wa majina ya maeneo.

Wenu Kasomi naomba majibu pia unaweza share stori ya chanzo cha eneo.
Aisee

Aisee!Nadhani tuliwaamini sana hata Mbeya,sehemu moja kule Chunya mzungu alisema making a loss!wao wakasema amesema Makongolosi!Ndo jina mpaka sasa!
 
Hivi umepata kujiuliza unapopita katika mitaa mbalimbali ya mjini Dar au mji mwingine wowote Tanzania, jina la mtaa au eneo husika limetokana na nini?

Kwa mfano, Kijito Nyama limetokana na nini? Au Mlalakuwa, Au Mtoni kwa Aziz Ali n.k, n.k. Labda utadhani imetokea tu ... just ipo ipo, hapana! Baadhi ya majina ya mitaa yana historia ndefu na yenye kukumbukwa hata kwa vizazi vijavyo.

Hapa napenda kuwahabarisha maana ya mtaa au eneo la nje kidogo ya jiji la Dar liitwalo Gongo la Mboto.Jina hili limetokana na nini? Nakumbuka nilipata kusimuliwa na mwalimu wangu mmoja miaka ile pale Tambaza Sekondari nikiwa kidato cha pili.

Alisema palikuwa na mzee mmoja mashuhuri ambaye alipata kuishi katika eneo hilo.Huyu jamaa alikuwa mkulima. Jina lake aliitwa Mboto. Siku moja alijilawa kwenda katika konde lake kwa ajili ya kujipatia riziki.

Wakati ule, maeneo yale yalikuwa na giza la mapori na vichaka kadhaa. Jioni yake asirudi nyumbani. Kesho yake hadi mchana Mboto haonekani.

Mbiu ikapigwa watu wakakusanyika,kilichofuata ni msako mkali wa kumtafuta mzee huyu.Baada ya siku kadhaa wakakuta nyayo za mnyama mkubwa mithili ya Simba na ishara ya purukushani kadhaa.

Walipochunguza zaidi wakafanikiwa kukuta Gongo ambalo alipenda kutembea nalo mzee huyu.Wakahisi kuwa Mboto huenda amekutwa na maafa ya kuliwa na Simba. Walichokiona pale ni Gongo lake,Ndipo hilo eneo hadi leo lajulikana kama Gongo la Mboto.

Tuhabarishane maana ya maneno mengine kama Msasani, Mikocheni,Mto wa Mbu n.k.

Makambako maana yake Madume ya Ng’ombe!
 
Back
Top Bottom