Asili ya Mwanadamu ni Mchukia Dhuluma. Serikali Dhulumati Itatengeneza Maadui Wengi Sana Dhidi Yake kwa Kukumbatia Dhuluma

Asili ya Mwanadamu ni Mchukia Dhuluma. Serikali Dhulumati Itatengeneza Maadui Wengi Sana Dhidi Yake kwa Kukumbatia Dhuluma

Hamatan

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2020
Posts
7,840
Reaction score
18,115
Asili ga binadamu ni kupenda haki, mwanadamu kupenda dhuluma ni kitu ambacho huwa kinapandikizwa na kutengenezwa. Kazi ya kupandikiza dhuluma huwa ni ngumu sana na huwa haishindi kwa sababu inapingana na asili ya binadamu.

Siku zote, mwanadamu ambaye dhamira yake haijaharibiwa, husimama na anayedhulumiwa, ndiyo maana watu kama Tundu Lisu wanapendwa na mamilioni ya Watanzania, kwa sababu wanajua na wanaamini kuwa anaonewa na kudhulumiwa HAKI.

Serikali hii kwa kuamua kuwa Serikali dhulumati, imechagua upande mgumu sana wa vita, na kamwe haitafanikiwa kulifanya kundi lolote, lote kwa ujumla wake kuwa kundi la kuunga mkono dhuluma na mauaji.

1. Wamejitahidi sana kuwafanya polisi kusimama na kundi lao dhulumati, lakini wapo polisi ambao hawaungi mkono uharamia unaoendelea.

2. Wamejitahidi sana kulazimisha jeshi liwe upande wao, upande dhulumati, lakini bado wapo wengi hawaungi mkono, na kuna wakati watainuka na kupinga kwa uwazi.

3. Wamelazimisha CCM nzima na wanaCCM wote waunge mkono dhuluma na mauaji, lakini wapo wanaCCM wengi hawakubaliani kabisa na mauaji, utekaji na dhuluma.

5. Wametafuta mbinu ya kuwafanya waislam wawe upande wa kuunga mkono mauaji na dhuluma kupitia wale mashekhe bandia wa BAKWATA, lakini waumini wengi wa kiislam wamejitenga na huo udhalimu.

6. Katika kufanikisha sera yao ya mauaji, utekaji na dhuluma, wameviteka baadhi ya vyama vya siasa na kuvifanya vyama chawa vya CCM ili viunge mkono mauaji, utekaji na dhuluma nyingine kwa ujumla, lakini hata ndani ya hivyo vyama walivyovitengeneza, kuna wanachama wengi hawaungi mkono mauaji, utekaji na dhuluma nyingine, ndiyo maana hata viongozi wa vyama hivyo wamekosa ujasiri wa kuunga mkono uharamia unaoendelea kama walivyokuwa wakifanya hapo mwanzo.

NB: Kitu chochote kinachoenda kinyume na asili ya mwanadamu kukifanya kifanikiwe, lazima nguvu na gharama kubwa itumike, na hata kikifanikiwa, kamwe hakiwezi kudumu. Kwa hiyo, hizi dhuluma za watawala wanazozifanya za kutengeneza tume bandia za uchaguzi, uporaji wa mamlaka ya wananchi kuwachagua viongozi wanaowataka, kuteka watu, kuwaua wanaopinga dhuluma, teuzi za upendeleo kwa wanafamilia wao, kutengeneza chuki za kidini, kamwe haviwezi kudumu kwa sababu vyote ni kinyume cha asili ya mwanadamu. Lazima wataangukia pua, na hata huo ushindi wa kutengeneza hawataufurahia wala kudumu nao.

Mshindi wa kweli katika kila jambo kusimama katika HAKI. Na HAKI siku zote ina thawabu kubwa kwa maisha ya sasa na ya umilele. Lakini dhuluma wazifanyazo watawala wa sasa ni laana watakayoishi nao sasa na hata milele. Na ili laana hiyo wasiikwepe, shetani atazidi kuitia kiburi mioyo yao, hadi laana iwafike.

Wafurahi sana na washukuru kwa yote wale wanaosimama katika HAKI au kuitafuta HAKI, iwe kwaajili yao au kwaajili ya wengine.

Watawala tubuni, geuzeni mioyo yenu, tupeni mioyo yenu ya uovu, igeukieni haki ili muupokee msamaha. La sivyo subirini laana ambayo hamtaweza kuikwepa.
 
Back
Top Bottom