kulingana na vyanzo vya kale na vya kiushahidi.
Hii ndiyo sehemu ya kale yenye taarifa za kale kuonyesha wamewahi kuwepo watu na belief system yale kuliko hata hao Misri kama inavyoaminishwa na mainstream historia.
Hapa ni GOBEKLI TEPE, Uturuki ambapo pako mwambao mmoja na Sumeria. Hii makadirio yake ni miaka 12000 -6000 iliyopita.
(Japo mimi ni muumini wa biblical creation na naamini kuna errors nyingi katika dating system ila vyote yangu viumbwe ni miaka kama 6000 tu ). Lakini pamoja na Yote bado Egypt kiushahidi sio ya kwanza kwa kuanzisha unayoyasema.
Mwisho wa Yote, ukaribiano wa ibada za Jua, miungu kati ya Sumeria, egypt, china, india na ufanano woote wa ibada za jua na za kimizimu duniani kote bila kuwasiliana kwa wahusika ni Ushahidi kiwa chanzo chao ni kimoja.
Na sisi tunaoamini Uwezo wa Mungu, Na ukweli kwamba taifa pekee lenye uwezo wa kutunza historia yake ni wayahudi. Na Mungu wa wayahudi ndiye Mungu Muumba wa dunia nzima. Ametutaarifu hilo kuwa yote yalianzia Siku chache kabla ya Gharika.
Pia hakuna hitimisho la moja kwa moja kuwa belief system ilianzia Misri kisa kaushahidi kamoja kakihistoria huku kuna maelfu kama sio mamilioni ya sites bado zinafukulukiwa mkuu.
View attachment 868725
Historia inayoumana na Bibilia huwa naiita HISTORIA TaKATIFU. hivyo ancient idolatry imeanzia hukohuko Babeli enzi za wakina nimrod. Yawezekana Misri ilikuja kuwa maarufu zaidi baadaye na kupata umaarufu, na kupeleka upagani ugiriki, kisha waroma wakauingiza duniani kwa mara ya pili japo upo ushahidi mwingine wa direct link kati ya babylonian dieties kuingia huko italy kwa kupitia moja kwa moja huko babel inagawa asilimia kubwa ni kutokea misri.
Nadhani konachoupa misri umaarufu ni kiwa chuo kikuu cha uchawi na upagani duniani hasa pale alexandria.
pale ndio kulikuwa mwisho wa maneno. hata juzijuzi napolion alipeleka majeshi yake na wataalam kwenda kuchota maarifa pale.
mwisho wa siku, hakuna jipya chini ya jua yaliyopo yanasyosumbua watu katikaulimwengu wa ibada yaliwahi kuwepo na yalianzia babeli. Na dunia inarudi babeli kwa mujibu wa Ufunuo 18:1-4.
Kama ile sanamu ya Daniel 2 ndotoya mfalme wa babeli kuhusu Historia ya dunia na falme yake. Yesu anakuja kuisambaratisha dunia asimamishe Ufalme wake wa milele. Sisi wengine ni mabalozi wa ufalme ujao, ndio maana tunawasisitiza watu wajiandikishe uraia wa ufalme wa Mungu maana huu unapita pamoja na uasi wake.