Unaposema mbona hadi leo huku Pwani watu wana akili kama za "Boko Haram" (sifhamu unamaanisha nini hasa), you sound like huko Bara mambo swafiiii kabisa… watu wamebukua ile mbaya; jambo ambalo si kweli!! Let's be honest here… hivi ukiondoa Mkoa wa Kilimanjaro, Mbeya na Kagera, ni bara gani huko mnakosema watu wamebukua ile mbaya? Singida kwa akina Tundu Lissu na Mwigulu Nchemba? Mnzaungumzia Mwanza? Au Geita?Au Simiyu? Au Shinyanga? Huko Bara kwa Wakristo mnakosema watu wamebukua ile mbaya ni wapi? Au Rukwa? Au Dodoma? Kigoma? Are you talking of Ruvuma? Hivi ndugu zangu Wahehe nao wanaweza kututambia watu wa Pwani kwamba nao wamebukua ile mbaya?! Hivi kweli wale Wamasai na Wasonjo wa Arusha wamebukua wale kweli? Hivi kule Kiteto kweli watu wamebukua kule kiasi cha kuwaona watu wa Pwani ni Masakala wasioenda shule kwavile ni Waislamu? Ni Wakristo wa bara ipi hiyo ndugu zangu ambao wamebukua kiasi cha kutamba kila siku?!! Au huko nako wamejaza Waislmu wanaoishia kwenda madrasa?
Turudi huku Pwani! Tofauti na nyie wenzetu mnaojigamba mmepiga buku kweli kweli wakati majority ya Wakristo hawajui hata kusoma na kuandika, wenzenu angalau tunakiri kwamba kwa upande wetu kuna tatizo bila kujali kwamba kila mmoja atakuwa na mtazamo kuhusu chanzo cha tatizo! Sasa tukija kwenye hoja kwamba mbona hadi leo watu wa Pwani bado kabisa, ukweli ni huu hapa chini!!! Tuwiane radhi, wakati mwenzetu Diamond amejaaliwa kipaji cha muziki, wengine tumejaaliwa kipaji cha kuandika... tukianza maneno yanakuja tu... yanakuja tu, ukitanabhai, umejaza kurasa!!!
Tundelee!
Msingi wa mfumo wa sasa wa Taifa hili uliwekwa na Wakoloni wa Kijerumani na Kiingereza! Kama nilivyosema hapo awali, hawa wakalazimika kujenga mashule si kwa sababu waliwapenda wale waliowaingiza kwenye Ukristo bali walihitaji labor force inayofahamu elimu ya Kimagharibi! Tofauti na Waraabu, Wazungu walikuwa ni Watawala kwahiyo walilazimika kufanya hivyo! Kosa kubwa ambalo walifanya, tena kwa makusudi, ni kuacha elimu itolewe na Wamisionari kwenye nchi ambayo tayari ilikuwa na watu wa Imani nyingine. Tusisahau, Wamisionari hawa walikuwa ni Mawakala tu Wakoloni. Aidha, waliacha kwa makusudi elimu itolewe na Wamisionari kwavile walifahamu Utawala wao wa kikoloni usingekuwa rafiki kwa wananchi kwahiyo endapo elimu hiyo ingetolewa na serikali yenyewe ambayo hawakuwa na utu, kulikuwa na uwezekano mkubwa kwa wananchi kuisusia kwa kuona ni elimu ya madhalimu! Isitoshe, by that time wala hawakuwa na ufahamu na umuhimu wa hiyo elimu kwahiyo ilibidi itolewe na watu wa kuaminika! Kwa kufahamu hilo, wakaamua kuacha jukumu hilo kwa kanisa, watu wenye kauli ya upole na upendo!
Sasa, ile hali ya kuiacha elimu itolewe na Makanisa tayari ikawa-exclude Waislamu kwavile tayari hawa walishalishwa propaganda za dini nyingine… hili lina effect mpaka leo; iwe ni kwa Waislamu au Wakristo! Leo hii hapa BAKWATA wawe na bonge la shule lenye maendeleo mazuri kitaalamu, wapo Wakristo watakaoacha kupeleka watoto wao huko kwavile tu ni ya Ki-Islamu… seuze wazee wa miaka mia moja iliyopita!!!!!! Ndio maana hata hapa, unaweza kumsikia Mkristo akisema anavyowachukia Waislamu lakini muulize wamewahi kumfanya nini; HAKUNA!
Sasa basi, msingi huo ukaja kurithiwa na serikali ya weusi ambayo ilitangaza kufuta ubaguzi wa Kidini! Lakini haya yanafanyika wakati tayari kuna msingi umeshajengwa! Babu yake NasDaz alizaliwa wakati wa Ukoloni… huyu hakupelekwa shule kv alishaambiwa hao Wazungu waliokuja wanalisha watu nguruwe!! Huyu Babu yangu nae akapata mwanae miaka michache kabla au baada ya uhuru! Kwahiyo ingawaje unamtangazia mtu kwamba elimu hii inatolewa kwa wote, bado unawatangazia watu wasiofahamu umuhimu wake! Tena hata huko kutangaza sijui walikuwa wanatangaza tangaza vipi wakati nchi yenyewe iikuwa ndo hivyo tu!
Kutokana na hilo, mtoto wa babu yangu nae hakupelekwa shule! Mtoto huyu alipokua mkubwa, harakati za maisha zikamfanya atembee huku na huko jambo ambalo baba ake hakufanya! Katika kutembea huko, akakutana na wenzake kama yeye ambao baba zao nao hawakupata shule lakini vilevile wakakutana na wenzao ambao wazazi wao walikumbwa na mfumo wa elimu ya Magharibi! Haya kwa kiasi kikubwa yalitokea miaka ya sabini kuja themanini! Kwahiyo ingawaje wazazi wetu nao hawakupata shule, kutembea kukawafanya wagundue alah, kumbe kusoma ni muhimu namna hii!!! Kama ilivyo desturi ya mabadiliko kuchelewa kushika kasi, hawa baada ya wao nao kupata watoto kuna wengine wakapeleka watoto wao shule na wengine hawakupeleka shule… hii ndio nature ya mabadiliko!!! Lakini hata wale ambao walipeleka watoto wao shule, bado hawakufahamu vizuri management ya mwanafunzi kwavile hata wao wenyewe hawakusoma! Kwahiyo, mtoto alikuwa akimaliza darasa la saba, ndo imetoka hiyo, labda Mungu apende awe alifaulu!! Lakini yule ambae mzazi wake alienda shule, hata akifeli, mzazi wake atatafuta namna nyingine coz' tayari anafahamu management ya mwanafunzi iko vipi!!!
Sasa na yule mtoto aliyeishia darasa la saba kwavile anakumbana na changamoto kadhaa za maisha na labda kusafiri zaidi au kukutana na watu wengi zaidi kuliko wazazi wake, it's obvious harakati hizi zitampa msukomo tofauti na kufahamu kwamba darasa la saba si lolote si chochote! Huyu atajitahidi mtoto wake asiishie darasa la saba!!
Kwa bahati mbaya, hii ni system itakayochukua miongo na sio miaka hadi kui-break ile circle! Kama ingekuwa ni genes, ni kwamba zile original genes zinakuwa neutralized from generation to generation to the point kwamba majority ya watoto wazazi wao watakuwa ni graduates! Kutokana na hilo, ndio maana naona ni vichekesho humu jamvini Wakristo wanavyojigamba wamepiga shule wakati majority, mama na baba zao wameishia darasa la saba na wengine hata kuta za darasa hawajui zinafananaje!!!!