Asilimia 60 ya maafa ya mafuriko Dar es Salaam yanatokana na uzembe wa serikali, Raisi Samia akubali ukweli huu

Unajua, watu kutohama mambondeni kwa kutii agizo la serikali ni uzembe pia wa serikali. Mbona Ngorongoro wamehama?
Mkuu, wew umeamua kutafuta mchawi,
Ila mchawi wa kweli ni hao watu wanaopata mafuriko kila mwaka na hawahami,
 
LIVINSTONE/KIPATA
Pita mtaa wa Livingstone na KIpata uone jinsi barabara zilivyochafuliwa na mkandarasi
Miezi mitatu iliyopita greda na katapila zilipita na kuchimba chimba kisha wakaachia mashimo yanayojaa maji. Mpakaa leo hawajafika na hatujui ni kazi gani itafanyika na lini. Shida kwa wapita njia naa kwa magari
Afisa mtendaji yupo, mwenyekiti wa mtaa yupo, mbunge yupo na diwani yupo - WOTE WAKO KIMYA BILA YA MAELEZO -
Hii ni Dar inayoendeshwa na vigogo. Bila shaka mabilioni yamepigwa hapa
 

Kwa kujua au kutokujua watu wanashindwa kuelewa kuwa makazi ya jiji la Dar es salaam yapo kwenye mteremko wa vilima vya Pugu na Kisarawe.

Haya ni maeneo yenye kupata mvua nyingi kwa mwaka. Hata mvua isiponyesha Dar es salaam, maji kutoka vilima hivi yatatutesa tu.

Maji kutoka maeneo haya LAZIMA yaende/yafike baharia. Ili yafike ni lazima kuwe na njia za kuwezesha kupita.

Tumeshiriki kwenye makosa haya:

1: Kwa kuwa na serikali isiyowajibika vyema kwa mambo muhimu. Hatuiwajibishi serikali na hatuoni wajibu huo, nayo imelala.

2: Serikali yenyewe kutosimamia mambo muhimu. Kuhakikisha maeneo yasiruhusiwa hayaguswi, taratibu zote na tahadhali zinazingatiwa kwa wanaoishi, kufanya shughuli zao kwenye maeneo haya.

3: Mtu mmoja mmoja:
A: Kukata miti hovyo(miti kupunguza spidi ya maji, huzuia baadhi ya uchafu kutokushuka na huzuia udongo usiondoke kwa wingi ambavyo huziba njia za maji).

B: Kulima kilimo kisichozingatia aina ya eneo/mteremko(kuacha ardhi wazi bila kufuata matungazi, hapa maji huondoka kwa wingi, spidi kali na kubeba udongo).

C: Kujenga ndani ya njia za maji(tunafanua njia za.maji kuwa finyu au kutafita njia mpya, ambapo gharama ni kwa kila aliye kwenye eno lisiloruhusiwa).

NB: Maji hayasahau njia yake na ukiyazuia lazima ulioe gharama ya kuyatafutia njia au yakuondoe wewe.
 
Anayejenga miundombinu ni serikali, yenye uwezo wa kuzuia watu wasijenge mabondeni, njia za maji ni serikali, anayeweza kubadilisha makosa yaliyofanywa zamani Ni serikali,watu wanapoilaumu serikali halafu wewe unamtetea mtu eti ni waliotangulia, kwa hio serikali haihusiki kwa lolote,

Kumbuka mtu akijenga mkondo wa maji haathiriki yeye peke yake ni jamii nzima, kuendela kumlaumu yule mtu ni kusema hakuna serikali
 
bado kidogo utaanza laumu Mungu 🐒
 
Kwa hili siungi mkono! Siku zote Serikali imetahadharisha watu sana mf. Watu wasijenge mabondeni, na waliojenga wahame, lakini watu hawasikii!
Serikali ikisema itumie nguvu kuwahamisha, wananchi wanakuja juu!
Serikali inaona bora ikae kimya!
 
Sometimes hii nch tunalaumu mno serikali,
Watu wanajenga kwenye mikondo ya maji, wengine hadi wanatoa rushwa ili wajenge, then yakija mafuriko wanakimbilia kusema serikali, hahah


Uko sahihi sana.

Lawama kwa Serikali zimekua nyingi hata kwa mambo tunayosababisha wenyewe. Ni aibu!
 


Mvua ni baraka.

Ahsante.
 



KUTOA RUSHWA na KUPOKEA RUSHWA yote ni makosa ya Jinai.

Wahusika wote wawili ni wahujumu uchumi na Mahakama ya Mafisadi inawahusu.
 


Sasa hizo gharama za upumbavu na uzembe wanazilipia hao waliojenga kwenye njia za maji, wakiwemo watumishi wa serikali wenye makazi huko.



Karma is simply flawlessly beautiful.
 


Serikali hii hii ikiwabana kidogo ili kuwaweka kwenye mstari ulionyooka mnapiga kelele mpaka Mtaa wa saba Washington wanawasikia?!


Kwenye hili Serikali naona imeamua kumuachia mtoto wembe achezee itamsaidia kutibu vidonda.
 
Na ukiona mwanao kachukua kamba anaenda kujiny'onga utasema mwacheni, anajua madhara ya kujinyonga, wewe sio wa kulaumiwa, sivyo?
Mtoto anayetaka kujiua ni suala la muda tu labda umfungie kwenye pipa.
 

Umenena kwa kweli!tatizo wa kukusikiliza sasa!
 
Kuna mifano haina uhalisia, anayejenga ni binadamu mtu mzima mwenye utashi wa kung'amua jema na baya sio mtoto.

Kila siku Serikali inawaambia hameni hamtaki, wewe unataka nini zaidi ya maafa?.
Mwanao maana yake mtoto mdogo?
 
100% lawama kwa hao watu, kwa hio wao serikali ikisema kitu hawatumii akili ?
Sasa kama kila mtu anatumia akili, kwa nini tuna serikali? Si tuache tu kila mtu anatumia akili mambo yataenda. Hata hao trafiki barabarani waondolewe, maana kila dereva ana akili!
 
Sometimes hii nch tunalaumu mno serikali,
Watu wanajenga kwenye mikondo ya maji, wengine hadi wanatoa rushwa ili wajenge, then yakija mafuriko wanakimbilia kusema serikali, hahah
Nani amawapa vibali vya ujenzi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…