Asilimia 60 ya maafa ya mafuriko Dar es Salaam yanatokana na uzembe wa serikali, Raisi Samia akubali ukweli huu

Ukanda wote wa Pwani ya Bahari 50Km kutoka ufukweni itengenezwe Master plan yenye kufuata Topographic Survey ikijumuisha majengo gani yakae wapi lakini pia miundombinu gani inahitaji katika utunzaji mazingira.
Tatizo nilionalo kwa sasa ni uchafuzi wa mazingira kwa kiasi kikubwa unaosababisha miundombinu ya kupitisha maji kuziba hivyo maji kuchukua mikondo mingine kupita.
Hata hivyo Ujenzi holela bila kufuata ushauri wa wataalamu ni tatizo lingine la kuifanyia kazi kwa haraka.
Ni vizuri bajeti za kujenga kingo za vijito na mito mikubwa inayopita katikati ya miji mikubwa ikatengwa kama ilivyo miundombinu mingine ili kutunza mazingira lakini pia kuzuia mafuriko ya mara kwa mara.
Ni vyema kwa Secretariate za Mikoa zikaunda timu za wataalamu ngazi ya Mkoa kwa kushirikisha wataalamu wa sekta binafsi walau kupata sanifu yakinifu ili Serikali kuu/Wizara husika zikatenga bajeti.
 
Sometimes hii nch tunalaumu mno serikali,
Watu wanajenga kwenye mikondo ya maji, wengine hadi wanatoa rushwa ili wajenge, then yakija mafuriko wanakimbilia kusema serikali, hahah
Ni nani wa kusimamia sheria za mazingira?
 
hayo madude mradi wa mtu, hayatoi pale. anaombea mvua tu
 
Huyo popoma kichwani uji hawezi elewa ulicho shauri
 
Machapisho kama adhimu hupata wachangiaji wachache kuliko ya Uchumba wa Manara.
Kiukweli hatutaki tuu kushughulikia changamoto zetu kikamilifu... Data base tokea Enzi za ukoloni 1957 ambazo tayari zilikuwa zinaonyesha maeneo ya maji, mikondo mpaka mapito ya maji... Swali sasa kwa nini havifuatiliwi? Je hii nchi haina planners?? Mwisho niseme pia mfumo wa uongozi, hasa huko mikoani na mawilayani, ambako kila kitu kidogo unamuona DC, mara RC badala ya kuona wataalam husika wakiwajibika ndiyo kabisa limeuwa ubunifu na utaalamu... Sasa hivi huko mawilayani eti unakuta afisa mifugo au kilimo anasimamia ujenzi wa madarasa au nyumba za walimu???
 
Hivi umemuelewa mtoa mada? Hajazungumzia mtu mmoja mmoja, anazungumzia jiji lililopakana na bahari kuwa na mafuriko wapi na wapi?

Okay, watu watahama, je madaraja yanayokatika nayo yatahama?
Je barabara ya jangwani nayo itahama?
 
Hivi umemuelewa mtoa mada? Hajazungumzia mtu mmoja mmoja, anazungumzia jiji lililopakana na bahari kuwa na mafuriko wapi na wapi?

Okay, watu watahama, je madaraja yanayokatika nayo yatahama?
Je barabara ya jangwani nayo itahama?
 
Sometimes hii nch tunalaumu mno serikali,
Watu wanajenga kwenye mikondo ya maji, wengine hadi wanatoa rushwa ili wajenge, then yakija mafuriko wanakimbilia kusema serikali, hahah
Hivi unaelewa ulichoandika!?
 
Wanapojenga serikali inakuwa wapi, imelala? Na utakuta wengi wana vibali vya serikali. Ndio maana tunasema bottom-line yote haya ni uzembe wa serikali, japo kuna 20% ya lawama kwa hao watu, na 20% kwa natural disasters
Yani Kuna watu sio Huwa vichwa vinawaza nn !!!Yani anaiondoa serikali eti
 
Iyo yote inatokana na poor infrastructure inayochangiwa na poor sewage system ambayo inachangia maji kutuama kwenye eneo moja
 
Serikali inaongoza vilaza wa namna gani wasiojua wajibu wao wala kujali usalama wao hata kidogo??

Kuna vitu sio vya kuilaumu serikali mkuu, japo ni kweli ina makosa lakini uhai wako wa kuulinda ni wewe kwanza kabla ya hiyo serikali.

Wakati huu unasema ina kosa hili na hile tayari vyombo vimesombwa na maji, nyumba nzima ina maji na sio kua hukua unajua. Unajua kabisa na sio mara ya kwanza .

Ni december tu hapo, mvua imepiga nyumba zimejaa maji lakini watu hawachukui tahadhari hata kidogo.

Mzee kabla ya serikali ni wewe kwanza, Dar hamna ushirikiano kabisa, barabara za mtaani au hata nje ya nyumba nyingi za watu ni chafu, barabara za mitaa hazipitiki, uchafu unarundwa sehemu yoyote, madimbwi yanayoweza kufukiwa hata na watu wachache hayafukiwi, wapuuzi wanaongeza tu ukubwa wa dimbwo kwa kupita na magri yao vioo juu, wanasubiri serikali.
 
Sometimes hii nch tunalaumu mno serikali,
Watu wanajenga kwenye mikondo ya maji, wengine hadi wanatoa rushwa ili wajenge, then yakija mafuriko wanakimbilia kusema serikali, hahah
Mpaka wajenge na serikali inaona mpaka wanahamia maana yake nn
 
Na sahv serikali wala hawahangaiki
Na watu wa mabondeni huko

Ova
 
Unapotaka haki wajibika kwanza beba jukumu la usalama wako wewe mwenyewe kama kichaa anaona moto na anakwepa sisi tulio timamu tunakwama wapi kuyatambua maeneo hatarishi kuishi kuna watu walihamishwa wakapewa na maeneo ya kujenga wakazunguka wakarudi palepale walipoambiwa si salama now mnataka serikali yaleyale ya mwanzo?Tusiwe wasahaulifu kiasi hicho
NB:KUSIKIA KWA KENGE NI MPAKA ATOKE DAMU
 
Wengine hujibu kwa fahari kuwa wameshazowea mafuriko na hawahami. Wanasema ni tatizo la siku moja baadaye wanasafisha nyumba zao na maisha yanaendelea.
 
Wanapojenga serikali inakuwa wapi, imelala? Na utakuta wengi wana vibali vya serikali. Ndio maana tunasema bottom-line yote haya ni uzembe wa serikali, japo kuna 20% ya lawama kwa hao watu, na 20% kwa natural disasters
Shida akili zetu pia haziko sawa. Wakisema tusijenge tunalaumu, wakisema tuhame tunalalama kila kitu sisi tunaonewa
Tunataka kuishi kwa kuonewa huruma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…