Utasikia wanasifia fisadi aliyeiba mali za umma kuwa mjanja na ametoboa.
Wanadanganywa na maigizo ya wanasiasa ambayo hayawezi kuwasaidia .Eti Makonda nyota imewaka.
Watoto wao wanavuta bangi na madawa ya kulevya na kuwa mashoga kisa tu kuiga maisha ya Usa.
Pumbavu kabisa.
Ujue tatizo linatokana na nini; accountability Kwa Mwanasia hapa kwetu ina mchakato mgumu sana.
Yaani kum-hold account muhusika wa rushwa hasa mwanasiasa kuna ugumu kwasababu wakum-hold ni mpiga kura.
Mfano waziri akipata kashifa ya rushwa anaondolewa uwaziri lkn anabaki na Ubunge.
Msimu wa uchaguzi ukifika inabidi wapiga kura wamuadhibu huyu Mbunge kwa kutomchagua.
Matokeo yake, naye anajipanga anatafta hela za kutosha, unakuta mpiga kura anapewa laki mpaka tano.
Anapewa laki tatu kwanza anaambiwa ukishaona tumeshinda njoo uchukue laki 2 yako.
What do you expect? Mm Nina njaa, mwanangu anahitaji chakula, Sina pakukimbilia, ukiniambia huyu Mbunge nisimchague ni mla rushwa sitakuelewa!
Hivyo, unagundua kuwa Umasikini ndo chanzo Cha yote haya!
Dhana ya uwajibikaji (Accountability) Kwa Afrika ni ngumu sana braza kutokana na muundo wetu wa siasa za kimapokeo!