We jamaa ni mgumu kuelewa! Anachoeleza mleta mada ni loopholes zilizopo kwenye mfumo wa elimu zinazomfanya mwanafunzi awe incompetent kwenye kujiajiri au kuajiriwa kwa kifupi elimu haimpi mwanga wa kujiongeza na hata akijiongeza anafanya mambo yake shaghala baghala ilimradi siku ziende
Km ukipata fursa kwenda nairobi tembelea ma shoe shine wao uone jinsi walivyo very smart na proffessional wanaendesha biashara zao kisasa na kisomi tofauti na huku kwetu
Sent from my SM-A013G using
JamiiForums mobile app
Uwajibikaji binafsi unauweka upande upi?
Kwamba elimu ya Kenya inazalisha shoeshiners smart & professional? Huu mfano umemaanisha ama unatania?
Kila binaadam anawajibika kuwajibika kwenye nafasi yake yeye mwenyewe binafsi.
Wazazi, walezi, ndugu, Jamaa na Marafiki na jamii kwa ujumla kila mmoja asimamie misingi ya utu na uhalisia wa matokeo ya maamuzi yetu ya aina yoyote kuhusiana na chochote.
Watoto na vijana wetu mitaani wanajilea.
Sisi wote wanawake kwa wanaume tumejikita katika utafutaji.
Starehe zetu na matendo yetu yamekua Sawa na matangazo ya hadhara Kisa utandawazi. Watoto wanaona wanajifunza na kufuata mkondo.
Wazazi wamewekeza hali na mali katika muonekano wa kidunia. Wazazi hawataki kugharamika kwa hali na Mali kwenye elimu na makuzi ya watoto wao.
Wazazi wengi hawafuatilii mienendo ya watoto wao na wengine hata hawajui shule wanazosoma watoto?
Na walimu wengi wa siku hizi nao wala hawawajibiki kufuatilia wala kutoa taarifa kuhusu mienendo ya wanafunzi.
Hakuna ushirikiano wa dhati kati ya walimu na wazazi kwa maeneo mengi bado.
Watoto walelewe na nani atakayewafunza njia zetu na asili yetu?
Jamii inaruhusu matendo ya hovyo kwa wao kushiriki na pia wengine kufumbia macho halafu matokeo lawama wanatupiwa Serikali/CCM?
Kwani hao CCM ni majini? Si ni watu tunaoishi nao huku mitaani? Nao si sehemu ya ndugu na Jamaa zetu? Tena wengine wameamua kuwa Machawa wao sasa kwanini tusiwe na jamii ya hovyo?
Waalimu wengi sana ni wanachama wa hiyo CCM. Waalimu wengi sana wako kwenye “Mfumo” wamefanya nini zaidi ya kujaza mifuko yao?
Uwajibikaji ni kipimo cha Utu.