Asilimia kubwa ya Watanzania wanatumia nguvu za giza katika Biashara, Ajira na Harakati za Maisha Kiujumla

Asilimia kubwa ya Watanzania wanatumia nguvu za giza katika Biashara, Ajira na Harakati za Maisha Kiujumla

KWA utafiti ipo hivi 40,40,20 yaani 40% wanaamini ushirikina, 40% wanaamini katika Mungu, 20% wanaelea awaamini katika ushirikina wala Mungu bali mapambano yao.
 
Hiyo timing iwe na haki na wala usiweke dhulma ndani yake. Kama kukwepa kodi, kuminya ujira wa vibarua, kuminywa bei wakati wa kununua, na kuuza zaidi ya mara 3 ya garama ya mzigo.
Inawezekana,mfano kwenye real estate, kwenye biashara za kupanda miti. Nk
 
Ni kweli kabisa hiyo percentage.
Kuna wakati watu nao waheshimu Sana walifuata eti wakasema Kama unataka Mambo yako yanyoke kibiashara twende tukupeleke kwa mtaalamu wanamuaminia..Mimi kwa Imani yangu ya kikristo niliwachana live nkawambia siwezi fanya jambo Hilo in my life ...mmoja wao anayetaka kunipeleka huko ukimwangalia Hana achievement yoyote ..kama wewe ni mfanyabiashara unauza na kununua utagundua unakochukua Mali Tajiri ni fully ushirkina hata wateja wako wengi full ushirikina.....kama kweli ni mkristo fanya ibada si kitoto otherwise utakuwa unawafanyia watu kazi

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Ukiingia dukani kwa mtu kakuta kawasha udi ujue Kuna kitu kisichoonekana anafuga kinachosimamia biashara yake
 
Kwenye siasa, uchawi 100%

Biashara uchawi upo kwa 75% waliobaki hawajielewi wamuamini Mungu au waingie kwa sangoma[emoji23][emoji23][emoji28][emoji28]

Kwenye Ajira uchawi unatumika kupandisha vyeo, kulinda vyeo na kurudisha kazini wadau waliotimuliwa.

Mahakamani huko 90% na zaidi kuna mauza uza kibao ya ushirikina. na umeua wengi sana kwenye kesi kama za Mirathi

Kwenye mapenzi huko 90% ya kina mama wanatulisha vitu vizito sana ili tuwapende na kuwasikiliza..

90% ya kesi za mirathi humalizwa na ushirikina. Jikute wewe ndio unapinga wadau wasiuze mali utajikuta jalalani unaokota kopo

Narudi
Inasikitisha, sielewi kwa nini biashara isiende bila uchawi!
 
Ni kweli sababu ya ignorance. Lakini still majority ni masikini pamoja na kuutumia kwenye biashara
 
Ushirikina ungekuwa unasaidia 98% ya watanzania wasingekuwa masikini.
Ungekuwa unasaidia mwafrika asingechukuliwa utumwani wala kutawaliwa.
Zaidi ya propaganda uchawi hauna nguvu kihivyo, uchawi umebebwa zaidi na propaganda.
 
Kwa utafiti wangu juu ya uchawi na mafanikio ya biashara ni 40,40,20.
Yaani asilimia 40 utumia ushirikina, 40 uamini katika Mungu na 20 mafanikio yao hayajatokana na upande wowote kwa maana hawaamini ktk upande wowote kiimani.
 
Hivi kwann mechi nying za simba na yanga ni droo au ushindi wa goli moja, kuna namna apo 🤔
 
Kwenye kiwanda cha mziki na bongo movie ndo hatari, inasemekana asilimia 99 walozi.. inasikitisha na kukatisha tamaa
 
90% ya watz ni washirikina na 90% ni dhoofu hali wanachapwa vibaya na life, SAsa kwann wasitumie huo ushirikina kufanikiwa. Vyovyote vile hata wale wanaosemekana wanatumia ushirikina ukiwastudy hawapo mbali sana na kanuni za kufanikiwa kiuchumi ambazo yeyeto tu yule akizitumia ufanikiwa. Hao wakinga, wachaga, wapemba, waarabu, nk wanaoonekana wamefaulu hawapo mbali na kanuni hizo za uchumi ambazo Wayahudi ndio waasisi wake.
NAZO NI
1.Imani kwa Mungu
2.Saidianeni ninyi kwa nini
3.Wafunze watoto utafutaji wangali wadogo
4.Weka akiba kidogo kidogo Ili ziwe nyingi uwekeze
5.Acha anasa
6.Kuwaheshimu wateja
7.Uza kwa bei ya chini uuze kwa wingi upate faida nyingi
8.Uza kilicho bora
9.Nk

Yeyeto ufanikiwa akizifuata hata bila kuambiwa na mganga, mganga ucheza na saikolojia za watu tu hata masharti wawapayo watu ayachezi mbali sana na kanuni za kufanikiwa. Still bado akili ya mwanadamu Ina nguvu kuliko hata huo uchawi na ushirikina,sema tu wavivu kuiitumia thus tunategemea waganga, mitume na manabii watusaidie wao utumia ujinga wetu kufanikiwa.
 
Uchawi hauna umuhimu katika kutoboa life, huku uswahilini watu wanaroga Sana but still wana-suffer katika Extreme poverty

Mungu na kuishi katika utakatifu hizo ndo njia sahihi.
 
Back
Top Bottom