Asiyetakiwa ni Waziri Mkuu Majaliwa, kila kitu kimepangwa, ajiandae kuachia ngazi

Asiyetakiwa ni Waziri Mkuu Majaliwa, kila kitu kimepangwa, ajiandae kuachia ngazi

Kalemani takataka kwako ksbb labda ya malengo yako. Lakini kwa masikini alikuwa bonge la mtu kwa Tanesco.

Kipindi chake tu ndio umeme ulishaanza kuwa historia kukatwa. Ameondoka tu upigaji wa akina February ukarudi kwa kasi. Kipindi cha Kalemani tu kuunganishiwa umeme ilikuwa ni elfu 27000 tu. Haijawahi kutokea kwa yoyote,hata walivyomtoa wakapeleka kwenye laki 4 kasoro,na hawakuwa na sababu zaidi ya kusema haiwezekani. Yeye akawajibu inawezekana kulipia 27000 tu na kila kitu kikawa sawa.

Maana yake hata hizi laki 4 kasoro hazina tija ksbb wangesema laki 4 na umeme unakuwa sawa,lakini ndio umerudi enzi ambazo hatujawahi kuzipitia.

Fikiria Magu alimtoa lakini akamrudisha tena.
Kale alikuwa anapigwa figisu na wapigaji aliwazuia kujipigia. Ndio maana walivyoingia tu wao wakamchomoa na upigaji ukarudi
Kalemani ndio waziri pekee Alie iweza wizara ya nishati
 
Reforms na Rebuilding ya mama Samia si mchezo. Mliozowea kuishi kimazowea mtakuja na kila hoja ya kijinga.

Majaliwa niliwahi kuandika uzi kuhusu yeye siku nyingi sana.

Binafsi, bila kutafuna maneno namuona Kassim Majaliwa Majaliwa kuwa ni mnafik na ameshindwa kabisa yake.

Haiwezekani Halmashauri zote na idara zote nyeti zilizochini yake ziwe na madudu nanyupo hapo kwa miaka.

Majaliwa anaufahamu wizi wote unaoendelea serikalini na anaufumbia macho au kwa makusudi, usaliti, au kwa kuwabhayupo "competent".


Madudu yanayoongeleWa bungeni ilikuwa inataiiwa Majaliwa awachie ngazi yeye mwenyewe kabla hajaambiwa na mtu.

Dudu moja tu lilimfanya Lowassa awachue ngazi.

Yeye, wizra zake zina madudu kila namna, kwa ufupi mlMajaliwa kazi imemshinda.
Leo umeandika kwa haraka sna na kwa kuchapia
 
Binafsi sioni kama wanataka wamtoe ila CCM ni wajanja sana wanamtengenezea njia Majaliwa ya Urais.

Washaona hawana wakumsimamisha na mtu pekee alie katika system anae eleweka utendaji kazi wake ni PM.

Chakufanya ili wakamilishe mchezo wao, wanafanya kama kwa JPM kabla hajawa waziri, wanamchonganisha na wana CCM wengine abaki ONE MAN ARMY halafu wakishafanikiwa kumchonganisha.

Wanamtupa kwa wananchi, ambao kwa asilimia 90 wataona PM anafaaa, Chaguzi za Rais zikifika Jina CCM wanatoa jina la MAJALIWA. hakika lazima wapite na kijiji cha kura.

CCM ni moja ya chama ambacho kinapomuandaa Rais wake kinamfanya Adui wa chama adui wa wa ilani yake halafu kinaangalia respond ya wananchi.

Katika yanayoendelea sitoshangaa sana nikisikia Majaliwa kajiuzuru halafu akaja tena teuliwa kuchukua fomu ya urais kwa kulazimishwa.

Msiwaangalie CCM kama malofa hiki chama kina mfumo wa 4 4 2 ukikiangalia juu juu huwezi kielewa.
HAPO NIMEJARIBU KUKUELEWAA!
 
Khassim mpaka 2025 atakuwa na 10yrs kazini, sikumbuki kama tuna historia ya PM aliyedumu kazini zaidi ya 10yrs.

Sidhani pia kama tuna historia ya PM ambaye baadaye alikuwa Rais.
PM Khassim ni muslim, sidhani kama 2030 tutahitaji tena Raisi Muslim kwa hizi taratibu zetu.

Msilolijua wengi, Taifa mpaka sasa linaongozwa na mfumo wa kimafia nyuma ya pazia ulioanzishwa na yule dogo pale before 1995, hata pale dom 1995 mchonga alilijua hilo, dogo ni mafia toka akiwa dogo pale Saigoni..
Huyu Khassim ni sehemu ya uzao wa Saigon ni kijana wao ndio vile tu hesabu zao ni ndefu sana na wengi hatuzijui.
Juzi naona dogo kamtaja mentor wake six.
 
Ankoli Maja at first glance ndiyo ile timu ya "top officials" wale ambao hawakutaka tuongozwe na Beijing power. Zipo za chini chini kwamba Ankoli Maja, Mita ya Luku, Mzee wa Mate UDSM na Kichwa nazi cha Kongwa walitaka kuzuia kwa makusudi "peaceful transition of power" baada ya Mseminari kujikunja kwenye mchango wa kitanda kwa kubanwa kifua. Ankoli kwa kuwa yeye ndie alikuwa anawajibu wa kuandaa zoezi chapchap kwa kushirikisha vyombo vya ulinzi, nasikia alilichelewesha mchakato, miruzi ikawa mingi na ndipo Gen Mabe akang'aka, yaani akafoka kinoma, povu jingi na Katibu Mkuu kiongozi akapewa muda la sivyo, wazee wa mabaka mabaka wafanye yao, maana Chuma kilipojua hakitoboi, kilimwita Gen Mabe na Kardinali Jino kwamba wafuate katiba waache ufala, ila Mhutu wa Buhigwe Kigoma awe Makamu ni lazima watake wasitake.

Bila Gen Mabe tungeshasikia ya kusikia, maana Spy Chief alikuwa kundi la kukataa mchakato na kule msoga Mzee wa tabasamu, Ruksa, Mtoto wao wa visiwani wakataka tufate katiba inchi apewe Manzi kiishe. Mbeijing anawajua na wote kimewaramba kawatoa kwenye "spot light" yaani "Platform".

Ankoli anafahamu japo nampongeza ana "play smart" maana akijifanya kichwa maji anapewa uwanja wa lazima chap "uwanja wa futi sita urefu, futi tatu upana, futi sita kina".
 
Wamtoe Majaliwa halafu watu wa kusini tuwakirishwe na nani serikalini? Majaliwa ni kiunganishi kizuri sana cha ccm na serikali yake na watu wa kanda ya kusini. Kama mnataka kuunda serikali ya wakaskazini peke yenu, basi mwondoeni Majaliwa. Yatakayowatokea kwenye uchaguzi msije mkatulaumu sisi.
Waambie ni kusini na nyanda za juu kusini,kale kamama hatukaelewi
 
Wala sio jk!!ni wenye nchi Yao DS ndio hawkumtaka coz angeingia yangekua yale yale ya upigaji ya awamu ya nne halafu vurugu tu za visasi na wizi!!

Kumbuka kampeni zake zilifadhiliwa na wafanyabiashara wale ambao angewalipa fadhila na u Mungu mtu ungetamalaki nchini!!

Hata hivyo mlutheri asingeingia ikulu pia Bado wale jamaa wasingekubali!!
Hao DS hawakumuona huyu aliyepo sasa!!!?? Ni upuuzi tu hakuna cha DS wala nini. Ile kamati ya maadili ya MCC ndo wanaopanga nani awe namba moja na hakuna zaidi ya hapo.
 
Wamtoe Majaliwa halafu watu wa kusini tuwakirishwe na nani serikalini? Majaliwa ni kiunganishi kizuri sana cha ccm na serikali yake na watu wa kanda ya kusini. Kama mnataka kuunda serikali ya wakaskazini peke yenu, basi mwondoeni Majaliwa. Yatakayowatokea kwenye uchaguzi msije mkatulaumu sisi.
Kwani Nape ni wa wapi!?
 
Back
Top Bottom