Ndugu zangu,
Kipimo cha kitabu chochote ni kwanza reviews na zimechapwa wapi.
Hapa Afrika ya Mashariki kitabu cha Sykes kilifanyiwa serialization tatu katika gazeti la The East African December 1998.
John Iliffe na Jonathon Glassman walifanya review katika Cambridge Journal of African History na James Brennan alifanya review sikumbuki jina la journal.
Tanzania kitabu kilifanyiwa review na Business Times na baadhi ya magazeti.
Lakini kitabu kiliuzika sana katika tafsiri ya Kiswahili na hasa baada ya mijadala hapa JF.
Ukweli ni kuwa watu wengi waliumizwa na hii historia mpya na wengine walishangazwa kuwa iweje historia hii ilikuwa imefichwa kwa miaka yote ile.
Kilichofuata nilipata mialiko mingi ya kuzungumza ndani na nje ya Tanzania kilele ni siku nilipozungumza Northwestern University Evanston, Chicago kwani hawa ndiyo wanaongoza dunia katika historia ya Afrika na hii ilikuwa baada ya kufanya mhadhara University of Iowa.
Nilialikwa Zentrum Moderner Orient (ZMO), Berlin ambako nilizungumza na nilikaa mwezi mzima kwa kuandika paper na kuwaachia.
Hii papers inaitwa "Tanzania A Nation Without Heroes."
Siwezi kutaja kote nilipoalikwa na kuzungumza maana kwingine ni mialiko private katika miji ambayo napita kwa mengine lakini jamaa wakisikia niko mjini hunialika kwa chakula na kuniomba nizungumze.
Niliingizwa katika mradi wa Oxford University Press Nairobi wa kuandikia historia kwa ajili ya shule za msingi wakati huo huo wakijifunza Kiingereza na niliandika kitabu kimoja na cha pili ni anthology na waandishi wengine kutoka nchi nyingine za Africa.
Niliingizwa pia katika mradi wa Harvard na Oxford University Press , New York uliojulikana kama Dictionary of African Biography (DAB) uliochapa volume 6 za maisha ya Waafrika mashuhuri.
Haya yote sikuyategemea ukiachia mbali jinsi nilivyovutia watu hapa Majlis.
Watu wakijua nimeingia jamvini wanajazana kwa kufanya "bashing" nami husimana kuwajibu.
Natoa shukurani nyingi kwa JF kwani kama si wao kitabu changu na mimi nisingefahamika na watu wengi kote duniani wanakosema Kiswahili kwa kiasi hiki.
Hii imepelekea pia blog yangu
www.mohammedsaid.com kupata umaarufu mkubwa kwa "viposti" vyangu.
Nashauri ikiwa ndugu zangu mmeridhia na tuufunge sasa mjadala huu.
Ahsanteni sana.