Ndugu WanaMajlis,
Napenda sana JF pawe mahali pa kuelimishina.
Ili kitabu hufika Library of Congress si kwa mwandishi kukipeleka.
Kitabu kinafika Library of Congress kwa kawaida kutoka kwa Publisher.
Library of Congress wakipata kitabu wanakifanyia ''classification,'' na
kukipa namba (identification) ili iwe wepesi kukitambua kinapohitajika
na msomaji.
Hii classification inafuata na somo katika kitabu mathan ''politics, history,
religion,'' nk.
Hii ''classification,'' inakuwa katika mikondo mingi kama vile ''Politics,
African, Politics, Middle East,'' nk.
''History, Political History,'' nk.
Kazi ya kupokea vitabu inakuwa imerahisihwa na ''publisher,'' kwa kuwa
''publisher'' kwa mfano Oxford hawezi kuchapa kitabu cha ovyo kwa hiyo
Library of Congress ikipokea kitabu kutoka Oxford University Press, Nairobi
au Kuala Lumpur wanakuwa tayari wana uhakika na hicho kitabu.
Kitabu kinakuwa kichafanyiwa ''vetting,'' na Oxford University Press kwani
Oxford ina jina katika uchapaji wa vitabu.
Kazi itakayofanya Library of Congress ni ''classification'' na ''cataloging.''
Haiwapati kazi ya kuangalia kitabu kimeandikwaje.
Haiwezekani mtu akaandika kitabu chake mwenyewe, akakichapa mwenyewe
kisha akakipeleka Library of Congress kikapokelewa na kufanyiwa classification.
Kitabu kinaweza kufika Amazon kwa kuwa hawa ni watu wa biashara lakini kufika
Library of Congress kikawekwa maktaba huu ni muhali.
Maktaba hii iliyopo Washington DC ndiyo maktaba inayoongoza duniani na ina
viwango na heshima ya pekee.
Nimekuwa na uhusiano na Library of Congress toka miaka ya mwishoni 1980s na
nikapewa uanachama wa maktaba hii kupitia United States Information Services
(USIS) na tulikuwa wanachama wachache sana kutoka Tanzania.
USIS walitoa heshima hii kwa watafiti na waandishi wachache sana.
Library of Congress, Washington DC