Asiyoyajua Yericko Nyerere katika utafiti wa historia ya Mapinduzi ya Zanzibar

Asiyoyajua Yericko Nyerere katika utafiti wa historia ya Mapinduzi ya Zanzibar

Nilitamani kujibu pale juu ulichokiandika lkn nilijipa muda kwa kua nilijua utakuja tena.

Kwa ufupi kabisa naomba uelewe maudhui ya nilichokiandika;

1. Sijapingana na ukweli wowote ambao ww umeuelezea na majina mapya mliyovumbua wkt mnatafiti historia ya mapinduzi na iliyopelekea kutunga kitabu "Kwaheri Uhuru Kwaheri Ukoloni" cha Dr Harih.

***Ambacho ni kweli sijakisoma.

2. Sijapingana na mapungufu yoyote yaliyo kwenye kitabu chochote ambacho mchambuzi huru akiamua kukichambua na kuyabaini na kuyaorodhesha na yakasomwa...Ikiwa pamoja na uchambuzi ulioufanya ktk kitabu cha Yericko.

Tumesoma na tumeona chambuzi nyingi za vitabu..na vitabu vingi vilivyofanyiwa uchambuzi vina makosa kadhaa wa kadhaa.

Ninachopingana na wewe ni;

1. Maandiko yako yote kuhusu kitabu hicho yanaonekana ni mashambulizi binafsi kwa Yericko kupitia kitabu alichokiandika.

Vinginevyo tungeona maandiko yako mengi mno ya chambuzi za vitabu mbalimbali vyenye mapungufu ya kiufundi na kimaudhui.

***Na kazi hii bila shaka ingekuongezea kipato sana.

Lkn unafanya kinyume chake. Unamshambulia MTU kupitia andiko lake.

2. Kwa kua ulifanya tafiti za mapinduzi ya Zanzibar na ktk tafiti kuna vitu mmegundua ambavyo wengine hawakuvigundua basi unataka kila anaeandika kitabu lzm akutafute na umsomeshe au umshikishe kalamu aandike kila kile ulichokijua wewe kupitia tafiti zenu. Na anaeandika kinyume na hapo basi ni mtu ambae hafai au hakuna anachojua.

Hii si sawa kwa kua kama kuna vitabu vimepotosha historia ya mapinduzi basi ni vile vilivyoko madarasani ktk mashule yetu.

Mbona hauvikosoi wala haukosoi waandishi? Inawezekana wamefaulu ktk ufundi ktk maudhui jee? Wahusika je?

USHAURI!

1. Watu wengi tunapenda kuandika vitabu lkn hatujapata elimu ya utunzi na uandishi bora wa vitabu inawezekana ni pamoja na huyo Yericko ..Hii ni fursa kwako baba.

Anzisha darasa hata la mtandaoni ili utusaidie na kwa kua wasomaji hawataonana na mwalimu hata huyo Yericko atakuja kusoma kuliko haya unayoyafanya ambayo kwangu mm naona kama wivu, choyo, husda na ulimbukeni wa kutaka watu wakuone ww unajua sana.

2. Kwa utafiti uloufanya na utaalam wa uandishi wa vitabu ulionao nadhani unaweza kuandika chochote kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar iwe Shairi,Tamthiliya, au Filamu kabisa...ie. Vita vya Uganda.

Hata kitabu ukaandika kwa ufundi mwingine wa kifasihi.

Nguvu hizi unazopoteza kumshambulia Yericko na kitabu chake ambacho bado kinanunuliwa na tuliosoma hatujatoka bure..

ANDIKA BABA, LETA KAZI ZAKO TUZISOME ILI TUONGEZE MAARIFA NA TAARIFA.
 
Ridhwani Mbaraka
Ridhwani,
Umerudi mtu mwingine kabisa.
Nimefurahi.

Unaandika katika lugha ya kistaarabu na kwa adabu.
Ahsante sana.

Nakuwekea baadhi ya niliyoandika:
  1. PUBLICATIONS/RESEARCH PAPERS/ARTICLES
  2. The Life and Times of Abdulwahid Sykes 1924 –1968 The Untold Story of the Muslim Struggle against British Colonialism in Tanganyika, Minerva Press London, 1998 translated into Kiswahili as Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes 1924-1968 Historia Iliyofichwa Kuhusu Harakati za Waislam Dhidi ya Ukoloni wa Waingereza, Phoenix Publishers, Nairobi, 2002.
  3. The Torch on Kilimanjaro, Oxford University Press, Nairobi, 2006
  4. Contributing author for an African anthology: The Mermaid of Msambweni and Other Stories, Oxford University Press 2007, Nairobi.
  5. Contributing author Dictionary of African Biography (DAB), Oxford University Press 2011, New York.
  6. Uchaguzi wa Busara, Abantu Publications 2008, Dar es Salaam.
  7. In Praise of Ancestors (1987) Africa Events (London).
  8. Abdulwahid Sykes: Founder of Political Movement (1988) Africa Events (London).
  9. Islam and Politics in Tanzania (1989) Al Haq International (Karachi)
  10. The Plight of Tanzanian Muslim (1993) Change (Dar es Salaam).
  11. Tanzania - The "Secular" Unsecular State (1995) Change (Dar es Salaam).
  12. The Question of Muslim Stagnation in Education in Tanzania - A Muslim Riddle (Paper presented at the Conference of the Global World of the Swahili Intercultural Dialogue on the Indian Ocean Zanzibar, February 20 - 23, 2003).
  13. Islamic Education and Intellectualism in Eastern Africa ‘Themes from the Pulpit in Tanganyika (Tanzania Mainland) 1800 – 2000’ (Paper presented at International Symposium on Islamic Civilisation in Eastern Africa Kampala, Uganda organised by the Islamic Conference Research Centre for Islamic History, Art and Culture (IRCICA), Istanbul and the Islamic University in Uganda, Mbale December 15th – 17th 2003).
  14. Sheikh Hassan bin Ameir - The Moving Spirit of Muslim Emancipation in Tanganyika (1950 – 1968) (Paper presented at Youth Camp Organised by Zanzibar University, World Assembly of Muslim Youth (WAMY) and Tanzania Muslim Students Association (TAMSA) 27th February – 4th March 2004).
  15. Islamic Movement and the Christian Lobby in Tanzania - the Experience of the late Prof. Kighoma Ali Malima (1938 – 1995) (Paper Presented to Tanzania Muslim Students Association (TAMSA) Sokoine University of Agriculture (SUA) Morogoro 11th April 2004).
  16. Terrorism in East Africa the Tanzanian Experience (Paper Presented at the Conference on Islam, Terrorism and African Development University of Ibadan, Nigeria 8th - 10th February 2006).
  17. Al Marhum Sheikh Kassim bin Juma bin Khamis (1940 – 1994) and the Pork Riots of 1993. (Paper Presented at the Regional Conference on Islam in Eastern Africa: Islam Encounter with the Challenges of the 21st Century 1st - 3rd August 2006, Kenyatta University, Nairobi.
  18. 14. Muslim Bible Scholars of Tanzania – The Legacy of Sheikh Ahmed Deedat (1918 – 2005) Paper Presented at the International Symposium on Islamic Civilisation in Southern Africa Organised by The Organisation of Islamic Conference Research Centre for Islamic History, Art and Culture (IRCICA) The National AWQAF Foundation of South Africa (AWQAF SA 1 – 3 September 2006 University of Johannesburg.
  19. Tanzania: A Nation Without Heroes Seminar Organised by IFRA French Institute for Research in Africa and BIEA British Institute in East Africa 23rd and 24th September 2013 at IFRA Nairobi.
Ridhwani,
Mimi ni mhariri, mfasiri na pia ni ''publisher.''
Kusoma na kuandika ndiyo maisha yangu.

Nimejifunza kusoma labda nina miaka sita na bado sijakwenda shule.

Nakueleza haya ili tuelewane na tuende vyema.
 
Mzee wangu inaonesha unapenda sana wazungusha vijana vijiwe vya kahawa na kuwapa utam wa historia nusunusu.(utani )..nadhan ungekua kwe sehemu mzuri zaidi kama ungetupa link tusome hiyo historia unayoijua kwani kwa jinsi unavyojitanabaisha ni kama weye ulishushiwa hiyo historia toka mbinguni...kama ulipata bahati ya kusimuliwa kujisifu tu bila kuiweka kama ilivyo unatuchanganya sis vijana ambao hatukupata bahati ya kuiona no bora basi hata huyo yericko nyerere alijaribu kutuonjesha hata kama haikuiva kisawasawa kama unavyojaribu kutuaminisha...nawasilisha
cmoney,
Unaweza kuanza hapo chini:
Mohamed Said: AZAM TV KIPINDI MAALUM CHA MASHUJAA WA UHURU WA TANGANYIKA
Mohamed Said: WASIFU WA ABEID AMANI KARUME AZAM TV 2015
Mohamed Said: KIPINDI AZAM TV KUMBUKUMBU YA MAPINDUZI ZANZIBAR 2016
Mohamed Said: AZAM TV: MAPINDUZI YA ZANZIBAR KUTOKA KUMBUKUMBU ZILIZOZIKWA
Mohamed Said: Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere -Azam TV
Mohamed Said: KUMBU KUMBU YA MIAKA 54 YA UHURU - AZAM TV 02
Mohamed Said: AZAM TV KIPINDI MAALUM CHA SABASABA KUASISIWA KWA TANU 1954
Mohamed Said: AZAM TV KARUME DAY: ABEID AMANI KARUME - "THE MASTERMIND" MAHOJIANO NA IRENE KILENGA

Unaweza pia kuingia hapo chini ukafanya search kwa jina au matukio:
www.mohammedsaid.com
 
Naona umeonyesha ulivyofanya kazi ktk ushauribwangu wa pili ilioutumia kama hitimisho langu.

Lkn nimepitia moja baada ya nyingine nimeona bado hujajitendea haki ww mwenyewe na sisi wasomaji.

Ulichofanya ni kidogo kuliko uwezo wako.
Kubwa ulilofanya ni hili la kumshambulia Yericko na kitabu chake kwa kumwita majina yote.

Ushauri na maneno mengine niliyoyaeleza hapo tafadhali yafanyie kazi.
Tuone Tamthilia ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa filam au kwa Audio au kitabu au kwa mashairi n.k

Aufwidersehen!
 
Sasa Said, kama kweli ww ni mzee kwanini unatumia Avatar ya kidwanzi hivi; unapenda Coke eeh?
Kilambi...
Hizo chupa zina majina yangu.
Ziangalie vizuri ni hivyo tu hakuna zaidi.

Hata hivyo coke kilikuwa kinywaji changu hadi umri uliponitupa mkono.
Zamani nilikuwa nikipenda kula Big Mac and Coke.

Mbali sana niko na nyumbani.
 
Naona umeonyesha ulivyofanya kazi ktk ushauribwangu wa pili ilioutumia kama hitimisho langu..
Lkn nimepitia moja baada ya nyingine nimeona bado hujajitendea haki ww mwenyewe na sisi wasomaji.
Ulichofanya ni kidogo kuliko uwezo wako..
Kubwa ulilofanya ni hili la kumshambulia Yericko na kitabu chake kwa kumwita majina yote.

Ushauri na maneno mengine niliyoyaeleza hapo tafadhali yafanyie kazi.
Tuone Tamthilia ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa filam au kwa Audio au kitabu au kwa mashairi n.k

Aufwidersehen!
Ridhwani...
Mimi ni mtu wa kawaida tu siwezi kila kitu.

Niwie radhi si kawaida yangu kujibu kila kitu ukiona kitu nimekinyamazia
ujue nimeona bora iwe hivyo.
  1. Visiting Scholar: (2011)
  2. University of Iowa, Iowa City, USA
  3. Northwestern University, Chicago, Illinois, USA
  4. Zentrum Moderner Orient (ZMO), Berlin, Germany
 
Ni kweli nimeingilia Mjadala, siujui umeanzaje,
Ndio maana nikakushauri kua kwa faida ya wengine kama mimi ungegweka Link tuone Yeye alisemaje,
Sijakiona hicho kitu kwenye Red.
Shark,
Msome Yericko hapo chini:
Mohamed Said: YERICKO NYERERE NA HISTORIA YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR YA 1964
Take time to READ

Anaandika mkulima wa bamia. [HASHTAG]#YerickoNyerere[/HASHTAG]

Tusipoandika historia yetu tusilaumu tukiandikiwa, Mapinduzi ya Zanzibar 1964.

...................................................................

Taifa la Zanzibar limekulia na kudumaa katika uongo, ulaghai, ghiriba, vitisho na mauaji kwa zaidi ya nusu karne. Vizazi vimelishwa uongo wa uhalisia wa mapinduzi, Sababu za Mapinduzi na wanamapinduzi halisi wa Zanzibar bila sababu za msingi, lakini kwa maslahi ya watawala wa Zanzibar kwa msaada wa watawala wa Tanganyika leo Tanzania.

Ifahamike na kueleweka kuwa bendera ya Taifa huru la Zanzibar ilipeperushwa tarehe 12 Disemba 1963. Na huu ndio uhalisia wa uhuru wa Zanzibar nje ya mapinduzi ya John Okello na Julius Nyerere na kisha Sheikh Abeid Karume kuvishwa taji la ushindi wa mezani chini ya mkono wa Julius Nyerere.

Wanamapinduzi halisi wametupwa, hawatajwi wala kukumbukwa popote na zaidi wengi wamefutwa usoni padunia. Wamevishwa wengine taji la mapinduzi ilihali hawakujua hata kilichotokea usiku wa tarehe 12 Januari 1964. Karume huyu Abeid hakujua hata mapinduzi hayo yaliandaliweje na nini kilitokea bali aliyajua mapinduzi yao (ASP) yaliyokuwa yakiratibiwa Dar es Salaam huku Mwalimu akiwalaghai kuwa yupo nao ilihali nyuma ya pazia alikuwa kiungo muhimu wa John Okello kupitia njia ya Kipumbwi kule Tanga. Ilikuwa ni mbinu ya kijasusi na Mwalimu alifanikiwa sana, ilikuwa ni lazima atumie njia hii ili Jumuiya za kimataifa na wana ASP wasitambue kuwa ni uvamizi wa kiinchi bali mapinduzi ya wazawa.

Lakini ukweli unaanzia kwenye kundi la watu 300 waliokitwaa kisiwa cha Unguja wakiongozwa na mtu asiyekuwa maarufu kipindi hicho, aliyekuwa akiitwa John Okello, John Okello alikuwa wakala maalumu wa Tawi Maalumu (TISS ya leo) na akiishi Pemba ambako alitokea Uganda miaka michache tu. Ndani ya Zanzibar Okello alipata umaarufu kwa vijana majabali, ambao wengi katika wao walikuwa ni makuli na wachukuzi wa meli zilizoingia na kutoka bandarini Zanzibar, kundi lake hili John Okello lilikutana kwa siri. Okello aliwapa matumaini ya mabadiliko watu wake hawa, wafuasi, ambao wakifanya kazi pamoja kwa muda mrefu, mara nyingine katika mazingira ya hatari, na tayari kufuata amri za kiongozi yeyote ambaye ataweza kuwalipa. Wao walikuwa waasi wanaotafuta makazi.
Mchafuko wa kisiasa ulikuwa ukiongezeka ndani ya Zanzibar na Pemba tangu kifo cha Sultani Khalifa katika mwaka 1960. Sultani Khalifa alitawala Zanzibar kwa karibu ya miaka 50, tangu mwaka 1911. Baada ya udanganyifu mkubwa kwa majimbo ya uchaguzi na mseto katika chaguzi kuu mbili za mwaka 1961 vyama vikuu vilishindwa kujipatia wingi wa kura kwa kila kimoja.

Waingereza waliondosha majeshi yao kikiwemo kikosi maalumu cha Kiarishi ambacho kilikuwa kimewekwa karibu na uwanja wa gofu na mpaka wa mji Mkongwe mapema mwaka 1963. Wakati mfalme mpya, Jemshid akipandisha bendera ya Taifa huru la Zanzibar tarehe 12 Desemba 1963, aliadhimisha uondokaji wa Gavana wa kiingereza Zanzibar na mwisho wa ukoloni Zanzibar.

Uchaguzi mwingine uliofanyika mwishoni mwa mwaka 1963 ukiipa ushindi mdogo wa kura Muungano wa vyama viwili ZNP na (chama cha kizalendo Zanzibar) na ZPPP (Chama cha watu wa Pemba na Unguja). A.S.P (Chama cha Afro shirazi) kilikuwa kiwe kipo katika Serikali iliyo na chini ya nusu ya wabunge kwa mtindo wa bunge la Kiingereza na Sultani, akiwa kama ni mtawala tu lakini sio mtawala mwenye maamuzi ya mwisho. Taifa hili la Zanzibar ambalo lilikuwa mwanchana kamili wa Jumuia ya madola na mwanachana mpya wa Umoja wa Mataifa lilidumu kwa siku 33 tu.

Majadiliano makali ya kisiasa na maandamano yalikuwa ni matukio ya kawaida siku hizo. makundi ya watu yaliyokuwa yakiimba na kusifu majina mbalimbali ya viongozi wa kisiasa, huku yakivuka vizuizi vya barabara vilivyokuwa vikilindwa na askari wa kiingereza. Vikundi mbalimbali vilijadiliana juu ya mambo mbali mbali; mfano Haki dhidi ya fursa, Wageni dhidi ya wenyeji wa zamani, Ubepari dhidi ya Ujamaa, Wafanyabiashara dhidi ya wamiliki ardhi, Waunguja dhidi ya Wapemba, Waasia dhidi ya pazia la nyuma la vita baridi na harakati za utaifa na kuondosha ukoloni ambazo zilikuwepo kipindi hiki ndani ya Afrika.

John Okello hakuwa na jawabu ya mambo haya nyeti, lakini alikuwa na kipawa cha kutambua kwamba vikundi hivi vinavyoshindana vinatoa nafasi nzuri kwa mtu wa harakati kama yeye Okello. Hata hivyo, watu kama mia waliojizatiti wangaliwez kutwaa vituo muhimu vya kienyeji vya habari na kambi za Polisi. Mara tu baada ya vituo vya habari na Kambi za polisi pamoja na silaha kudhibitiwa na John Okelo, Ni nani katika visiwa angeweza kumshinda? Je, wanasiasa wangeliungana na kumshutumu na kumpinga kwa vitendo vyake visivyo halali? Au kama alivyotaraji, wangeendelea kutoaminiana na kutuhumu kwamba kati yao ndio wanaomuunga mkono? Je, wasingelitaka kukubaliana na yeye, haraka kabla mwengineo hajafanya hivyo? John Okello alichezesha rafu usiku huo wa mwezi wa Januari.

Viongozi wa A.S.P walifadhaishwa na matendo ya Okello (wengi wao, walikuwa hata hawapo visiwani wakati huo). Walikimbilia haraka kuwaunga mkono waasi. Mamia ya wafuasi wa vyama walipigwa na butwaa juu ya wale ambao walikuwa na shuku ya kukata fundo hilo gumu la majadaliano ya kidemokrasia na kukimbilia moja kwa moja kwenye utawala. Hawa walitafuta njia ya kuiandaa jamii kwenda sambamba na kanuni zao. Kanuni siku hizo zilikuwa ni ghali sana kama sarafu ya Marekani. Ubinadamu ulikuwa ni kitu adimu sana. Baadhi ya viongozi wa ASP baada kuona kwamba serikali itakuwa haina udhibiti na uwezo kujilinda na kutokuwa na imani matokeo ya chaguzi huria zilizofanyika, viongozi hawalitafuta njia za haraka za kuhalalisha udhibiti yale ambayo yaliitwa sasa "Mapinduzi". Makundi ya watu wenye fujo yalikuwa huru. Sheria na amani zilikuwa hazipo katika mitaa ya Zanzibar.Walimiliki ardhi na wafanya biashara waliburutwa kutoka majumbani na madukani mwao, uporaji na mauaji yalienea mji mkongwe mzima. Kwa kweli mji wenyewe uliporwa.

Waarabu na Waasia , waliokuwa wakiunga mkono vyama vyingine waliuliwa kwa makundi. Kwa usiku mmoja maisha ya watu yasiyovika yalipotea na siku nyengine baadaye maelfu ya watu waliikimbia nchi pamoja na kila walichoweza kubeba.

John Okello mwenyewe alijipachika cheo cha Jemedari Mkuu akishirikiana na bataliani zake zenye fujo walianzisha utawala wa vitisho ndani ya visiwa vya Unguja na Pemba. John Okello alitangaza vitisho visivyo vya kawaida na ahadi ya kifo kwa wote watakaojaribu kumpinga yeye. John Okello aliamini alikuwa akipokea maelekezo /dokezo kutoka kwa Mungu na akionyesha uwezo usiokuwa wa kawaida kwa kutumia nambari, kwa mfano tarehe 13 Januari, 1964, alitangaza ujumbe ufuatao." Serikali sasa inaendeshwa na sisi ikiwa mtakuwa wakaidi na kukataa kutii amri, Nitachukua hatua kali mara 88 zaidi ya hatua ninazozichukua hivi sasa" na "Na ikiwa yeyote atashidnwa kutii amri ya kutotoka nje ya nyumba kama walivyofanya wengine.sitokuwa na njia nyengine lakini kutumia silaha nzito. Sisi, ni jeshi lenye nguvu ya 99,099,000". Vitisho vyake na uwezo wake wa kuvitekeleza viliwatia hofu raia, hasa makundi mbali mbali ya jamii zilizo ndogo.

Tarehe 14 Januari, 1964 alitangaza maneno haya ya kufadhaisha, “Huyu hapa ni Jemedari Mkuu wa Unguja na PembaNafikiria kuelekea kijiji cha Mtendeni kukiangamiza ikiwa watu wa hapo hawatafuata amri. Baada ya dakika 40 nitawamaliza nyote hasa Wangazija", " na kwa vijana wote wa kiarabu wanaoishi Malindi; Nitapita Malindi nikiwa nimesheheni silaha ambazo mimi mwenyewe ndie nizijuazo. Nataka kuona kila mmoja abakie na chupi na kulala chini. Nataka kuwaona wao wanaimba... Baba wa Waafrika. Mungu Mbariki yeye na malengo yake na yale ya Jemedari Mkuu" Huko mjini Dar es Salaam ndani ya kipindi cha mapinduzi kulikuwa kugumu sana, hata Julius Nyerere aliingiwa na hofu ya utawala wa mkono wa chuma wa Okello (wakala wake), sasa ikaanza kusukwa mikakati ya kumpoka mamlaka aliyokuwa nayo. Okello hakuwa na chama cha siasa hivyo Mwalimu akapendekeza liundwe baraza la mapinduzi na Okello awe mkuu wa baraza hilo ambalo ndilo litakuwa na mamlaka yote ya Zanzibar.

Okello alikubali wazo hilo ambalo kikao kilifanyikia Dar es Salaam 1/2/1964, ikakubaliwa urais apewe kiongozi wa chama cha siasa yaani Abeid Karume lakini asiwe na sauti yoyote katika Zanzibar. Baraza hilo lilijumuisha wapiganaji watiifu wa Okello ambao hawakuwa Wazanzibari asilia (Mawakala wa Tawi Maalumu leo TISS). Nao ni pamoja na Field Marshal John Okello (Mganda) na msaidizi wake, Absalom Anwi Ingen (Mjaluo kutoka Kenya). Wengine ni Saidi Washoto (Tanganyika), Mohamed Kaujore (Mmakonde wa Msumbiji) na Hamisi Darwesh (Tanganyika). Walikuwapo pia akina Abdallah Mfaranyaki (Tanganyika), Saidi Natepe (Tanganyika), Seif Bakari (Tanganyika) na Edington Kisasi (Mchaga wa Kilimanjaro-Tanganyika).

Baada ya mgawanyo huo ilikubaliwa pia Abdulahman Babu awe mkuu wa vyombo vya habari pia akiwa ni mjumbe wa baraza la mawaziri. Walikubalikubaliana kuwa tarehe 1/4/1964 warejee tena Dar e salaam kwaajili ya kumalizia mipango ya kuitawala Zanzibar. Hapo ndipo siku aliyokwenda kufutwa Okello katika ardhi ya Tanganyika na Zanzibar katika msingi na muundo wa kisiasa, viongozi na wajumbe wote wa baraza la mapinduzi walipanda ndege moja kuja Dares salaam akiwemo Mungu wa Afrika, Okello walipofika uwanja wa ndege, itifaki iligeuzwa na John Okello akaambiwa asubiri kushuka awe wa mwisho. Baada ya kushuka wajumbe wote ndani ya ndege ile, alikwenda komandoo mmoja wa Kitanganyika ambaye alikuwa mkuu wa Tawi Maalumu la Ujasusi Tanganyika Bwana Emilio Mzena, Alimwamuru Okello asalimishe silaha yake na kisha kumwamuru rubani aipaishe ndege kuelekea Nairobi. Kenyatta alimwambia Nyerere kuwa mtu huyo (Okello) sio wa Kenya hivyo ndege ikaelekezwa Uganda ambako alibwagwa na historia yake ikaishia hapo. John Gideon Okello alizaliwa 1937, katika Wilaya ya Lango nchini, Uganda na alifariki mwaka 1971 kijijini kwao Lango Uganda alikokwenda kutupwa na Julius Nyerere na Karume. Kifo chake kimeacha majonzi kwa wanamapinduzi, kwani licha ya kuwa Baba halisi wa Taifa la Zanzibar kwa Mapinduzi matukufu ya Zanzibar lakini Waafro + Shiraz hawa wamemezeshwa uongo kuwa Karume ndie baba yao.

Okello kafa masikini hata msiba wake umehudhuriwa na ndugu tu bila heshima yoyote ya kiukombozi.Huku nyuma kazi ya propaganda ya kubadili ukweli kuwa uongo na uongo kuwa ukweli ilisimamiwa na Babu, alipiga propaganda kupitia radio kuwa akiyefanya mapinduzi ni Karume na ASP, hata chama chake cha UMMA Party hakukisemea tena. Wakati unyanyasaji uliposima jamii za tamaduni tofauti za Zanzibar zilikuwa zimeparaganyika. Taifa la chama kimoja lilitangazwa. Lakini bado Taifa hili likihofia uwezekano wa kufufuka upinzani kutoka kwa wapinzani waliokimbia nchi. Wateka mapinduzi hawa baadaye walijihakikishia udhibiti zaidi baada ya kusaini mkataba wa muungano wa Tanganyika.

Hii ingeruhusu maelfu ya marafiki wa kisiasa wa Tanganyika kuingilia kati upinzani wowote wa baadaye katika visiwa hivi. Askari polisi wa Zanzibar walibadilishwa kwa askari polisi kutoka Tanganyika ambao ni watiifu kwa chama na pazia la siasa za utengano ziliwakumba wazanzibari ambazo zilitakiwa kudumu kwa zaidi ya miaka 20. Kwa lugha rahisi tunaweza kusema mapinduzi yalipinduliwa.

Leo hii siasa hizi za utengano hazipo tena, kumalizika kwa vita vya baridi na kuelekea kwa uchumi wa kisasa umeweza kuifungulia Zanzibar milango kwa ulimwengu wa nje. Uchaguzi wa vyama vingi ulifanyika mwaka 1995, 2000, 2010 na 2015 katika uchaguzi uliosiginwa na mamlaka za Tanganyika. Viongozi walaghai na wenye kujali hali zao siasa za wameibuka Tanzania na hii imewafanya wakimbizi waliokimbia wakati wa mapinduzi kurejea visiwani kwa jicho la tatu. Uvumilivu na amani wa watu wa aina tofauti, ambayo ni tabia ya maisha ya wazanzibari, sasa hivi unajitahidi kurejea katika mitaa ya mji Mkongwe, Katika uga huu wa kisiasa ni kuwa matakwa ya Wazanzibar katika siasa mpya bado yanafinyangwa bila sababu za msingi.

Tutumie muda wetu kumuenzi mwanamapinduzi wetu Che Guevara wa Afrika, Field Marshal John Okello baba wa Taifa la Zanziba.

Makala hii inatoka katika kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi.

0715865544
0755865544

Na Yericko Nyerere
 
Mzee wangu Mohamed Said kwanza Shikamooo!

Kabla hatujaendelea na mjadala huu, naomba kujua, umekisoma kitabu cha Ujasusi wa Kidol na Kiuchumi chenye sura 6, kurasa 715, vielelezo 368, nyaraka siri 88, nyaraka huru 20????

Je umeelewa dhima ya kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi?

Naomba kujua hilo ili nianzie hapo kukujibu hoja zako zote
 
Mjadala wa mapinduzi ya Zanzibar kwa muktadha wa Mohamed Said unaacha maswali

Kwa muda mrefu nimemuuliza Mohamed, maandiko yake yanaonyesha mapinduzi kuchagizwa kutoka nje ya Zanzibar na si kwa ridhaa ya Wazanzibar. Kwa mantiki hiyo mapinduzi yana 'Uharamu'

Januari 12 Wznz wanasherehekea Mapinduzi wanayotaita 'matukufu'
Kwa jicho la Mohamed hayakuwa na 'uhalali' achilia mbali damu iliyomwagika

Je, Mohamed anawaeleza nini Wazanzibar inapofika Januari 12?
Wanasherehekea 'haramu' au 'halali' yenye Uharamu?
 
Hizo picha unazocopy kwa msisitizo wa hoja zako zitapendezesha kitabu chako kuliko hivi unavyofanya...Na kubwa zaidi Yericko hajaandika ya Zanzibar peke yake.Ameandika na mengine mengi kuhusu Tanganyika na maeneo mengine na huo ndio muundo wa kitabu chake.

WATU WEUSI TUNA TABU SANA AISEE!!
Mkuu, huyu Mzee ameandika vitabu kadhaa, na nilishasoma vitabu vyake viwili...cha mwisho ni kile cha Ukweli uliofichwa kuhusu wapigania uhuru wa Tanganyika, akieleza mengi sana na % kubwa ni ya kweli.

Lakini lengo kubwa ni kuujuza umma kuwa TANU ilianzishwa na wazee wa kiislam na waislam ndio Khasaa waliopigania uhuru wa nchi hii ila hawakuthaminika na hawatajwi katika historia. Ukimsoma zaidi atakuletea habari za Nyerere na mfumo Kristo.

Kifupi Mzee Mohammed ni Mdini sana na ni wazi kuwa Mapinduzi ya Zanzibar kwa sehemu kubwa yaliongozwa na mganda John Okell[/] lakini kwakuwa ni Mgalatia huwezi kusikia akizungumzwa sana...lakini Wakristo wala hawajali vitu vidogo hivyo.
 
Back
Top Bottom