Mzee wangu inaonesha unapenda sana wazungusha vijana vijiwe vya kahawa na kuwapa utam wa historia nusunusu.(utani )..nadhan ungekua kwe sehemu mzuri zaidi kama ungetupa link tusome hiyo historia unayoijua kwani kwa jinsi unavyojitanabaisha ni kama weye ulishushiwa hiyo historia toka mbinguni...kama ulipata bahati ya kusimuliwa kujisifu tu bila kuiweka kama ilivyo unatuchanganya sis vijana ambao hatukupata bahati ya kuiona no bora basi hata huyo yericko nyerere alijaribu kutuonjesha hata kama haikuiva kisawasawa kama unavyojaribu kutuaminisha...nawasilisha
Ndugu zangu,
Hebu someni hayo hapo chini kuna mengi mtatambua:
KUTOKA JF: HISTORIA YA TANU KAMA ILIVYOANDIKWA NA YERICKO NYERERE
Mohamed Said January 18, 2017 0
↑
.............Jukumu la kuandaa nchi hizo kupata uhuru liliratibiwa na shirika hilo la kijasusi kwa ustadi mkubwa bila baadhi ya makoloni kujua, lakini lilikumbana na kikinza hasa kufuatia mnyumbuliko wa kiimani ndani ya
ukristu kufuatia nguvu ya
Cambrige (Anglikana), mgogoro huo ulikuzwa kwakuwa Anglikana nao tayari walikuwa wameaandaa taasisi yao waliyoiita Fabian
Sociaty maalumu kwaajili ya kuwaandaa vijana wa
kiafrika kukabidhiwa nchi zao, Barani Afrika Jeisuiti ilibadili mbinu
kwakuwa dola la Kiingereza lilikuwa kikwazo kwa sehemu fulani, haikujikita kwenye dola isipokuwa ilisimama katika muundo wa shirika
lifanya shughuli zake ndani ya Kanisa. Dhamiri ilikuwa lazima itimie, kama
ilivyosemwna huko mwanzo kuwa hawa ndio wabobevu wa elimu ya juu kwa kila nyanja na ndio wanaotawala ulimwengu, hivyo vikwazo havikukwamisha wao kufikia malengo.
Katika Tanganyika chini ya Udhamini wa Jumuiko la Kimataifa, kulikuwa na harakati za hapa na pale za kudai haki za kiraia kwa wenyeji. Ifahamike kuwa vyama vya harakati hizo Tanganyika vilikuwa vingi sana, na vipo vilivyokuwa vikipingana vyenyewe kwa vyenyewe.
Mwaka 1927 hadi 1929 kanisa Katoliki nchini chini Joseph Gabriel Zelger, lilibainika kuingiza siasa katika utendaji kazi zake, kitendo hiki kiliwakwaza wakuu wa mamlaka ya kikoloni na kupelekea majasusi wakikoloni wapendekeze aachishwe uongozi wa kanisa nchini. Ni kweli tarehe 12
februari 1929 Zelger alistaafu
wadhifawake kwa lazima. Ni mwaka
huohuo wa 1927 ndio Chama cha African Assosiotion (AA) kilianzishwa na Gavana Sir
David Cameron
maaluma kwaajili ya kuratibu sherehe za watu weusi huko pembeni ya mji huko
mtaa wa Stanley (leo Lumumba) na kuwapa ofisi mahali leo wanapojiita TANU ilizaliwa. Lakini historia ya Tanganyika haiwataji waasisi wa AA, Rais wa kwanza Mwalimu Cesil Matola (msomi wa mwanzo kabisa enzi za
mjerumani kutoka kabila la Wayao), katibu mkuu wa kwanza
Klest Sykes (Mzulu Baba yake alikuwa mateka wa kikoloni toka Afrika Kusini), Mwekahazina Ali Ramadhan (
mzaramo na mvuvi maarufu wa pwani la Azania).
Hao ndio mwaka 1927 waliounda
Chama cha kwanza kabisa cha kutetea maslahi ya weusi Tanganyika na shughuli zake zilikuwa ni kuratibu sherehe za
waafrika tu. (Chama cha walevi kwa lugha nyingine). Mwaka 1933 Mwalimu
Cesil Matola alifariki na nafasi yake ikakaimiwa na katibu mkuu wa chama hicho bwana
Klest, mpaka ilipofika mwaka 1948 yakatokea mapinduzi yaliyoongozwa na mtoto wa
Klest aliyeitwa Abdulwahid Sykes huyu alikuwa ametoka kupigana
vita vya pili vya dunia huko Burma, na aliporudi alikuwa na mawazo ya ujana toka vitani, akampindua baba yake kwa
kumpiga ngumi puani, mapinduzi yaliyoitwa “ondoa wazee”. Kisha AA ikabadilishwa jina na kuitwa TAA, Rais wake wa Kwanza akawa Dr Vedasto Kyaruzi (Mhaya), huyu
ndie dakitari wa binadamu wa kwanza kabisa wa
kiafrika Tanganyika, Katibu mkuu akawa Abdulwahid Sykes na Mweka hazina akawa Dosa Azizi, utawala huo ulienda mpaka mwaka 1953 uchaguzi ulipofanyika na Nyerere akashinda pale kwenye ukumbi wa
Anautoglo Mnazimoja leo, mwaka 1954 Nyerere akabadili jina la chama na kuwa TANU jina ambalo lilibuniwa na Abdulwahid Sykes, TANU ilikwenda mpaka mwaka 1977 na kisha kikazaliwa chama kiitwacho CCM baada ya Muungano wa ASP na TANU.
Kisa hiki cha kufukuzwa kwa Kasisi huyu Bw. Zelger kinasema, Kanisa lilianzisha mafundisho yenye kuchochea fikra za kimaasi, nalilifanikiwa kuandaa wakufunzi maalumu kwenda katika majimbo yote ya kihuduma Tanganyika, hilo lilipelekea kuleta mtafaruku na dola ya mkoloni wa kiingereza ambapo ilimgharimu kiongozi huyu wa kiroho kuachia madaraka yake. Alipoingia askofu Edger Aristide Maranta mwaka 1930, ikiwa kama vile mwendelezo wa mtangulizi wake, Askofu Maranda alianzisha harakati za kuwashawishi viongozi wengine wa majimbo kuendeleza kutoa mafundisho yenye kumfanya mtanganyika ajitambue na adai uhuru wake, mfano, 23 mei 1938 wakati makanisa saba ya Kilutheri yakiwa kwenye hatua za mwanzo za mchakato wa kuungana, Askofu maranda aliomba kuhudhuria kikao cha tarehe 8 mwezi wa sita kilichofanyika Mjini Arusha, Askofu Maranda aliudokeza mpango ule wa siri wa katoliki katika kikao hicho, japokuwa kulikuwa na hofu ya kutoaminiana, lakini uthabiti wa malengo hayo ulijipembua baadae na kuwa wamafaa, ushahidi wa nyaraka za kumbukumbu za mkutano huo unaeleza.
Juhudi za kanisa kupigania mkataba wa Versailles ziliendelea kushika kasi huku zikiendeshwa kwa siri sana kwamfumo wa neno la kiroho, na ilipofikia miaka ya 1950+ kanisa sasa lilikuwa tayari linanguvu ya ushawishi kufuatia mafanikio ya harakati za kanisa katika nyanja za ukombozi barani afrika. Wakati hayo yakiendelea tayari kanisa kupitia shirika lake la kijasusi lilikuwa limewekeza kwa nguvu kubwa kumtafuta mtu imara mwenye weledi na vipawa atakayejengwa ili aje kuongoza nchi. Mtihani mkubwa kwa kanisa ilikuwa ni namna gani linaweza kuingia rasmi kudai uhuru wa Tanganyika. Katika kipindi hiki tangu harakati za kanisa zianze, Askofu Maranta pamoja na mapadre wa baadhi ya mikoa, walikuwa tayari ameshafanya juhudi kadhaa za kukutana na Mashehe waliokuwa na ushawishi mkubwa, mfano 05/02/1948, Askofu Maranda alikutana Shehe Issa bin Amir kiongozi wa kiroho katika msikiti wa Ilala - mchikichini.
Shehe Issa Bin Amir alizaliwa 1846 katika viunga vya Mzizima, mchikichini na kuhudumu katika wadhifa wa shekhe katika msikiti uliokuwa hapohapo viwanja vya nyumbani kwake na alifariki mwaka 1953 akiwa na umri 107, Shehe Issa Bin Amir kwa kabila alikuwa Mzaramo na akiishi hadi kifo chake Mchikichini pale nyuma ya kilipo kiwanda cha bia leo (TBL). Shehe Issa Bin Amir rafiki kipenzi wa Padre Maranta na mzee wa hekima za kilele cha zama hizo, mtu aliyekuwa kiungo muhimu kati ya uislamu na ukristu, Mtu ambae Mwalimu Cesil Matola rais wa kwanza wa AA na Klest Sykes katibu mkuu wakwanza wa AA, na wanachama wengine waliokuwa AA walimheshimu sana kwa hekima zake na mmoja wa wasisi wa Jumuiko la Uislamu Afrika Mashariki (EAMWS) Mazungumzo yao yalihusu harakati za ukombozi, Shehe Issa alimshauri Askofu kuwa ikiwa makanisa na misikiti yanapigwa marufuku na mkoloni kujihusisha na siasa za ukombozi basi watafute baadhi ya vyama vya harakati za ukombozi na waviunge mkono, wazo hilo lilimvutia Askofu lakini akajenga hofu kama je ndani ya vyama hivyo watapata vijana wasomi?.
Siku chache baada ya makutano yake na Shehe Issa, Askofu Maranta aliletewa mapendekezo kutoka kwa Attilio Beltramino kasisi wa katoliki aliyehudumu kule Iringa, mapendekezo ya kasisi huyu yalikuwa ni, Umishonari makao makuu uruhusu udurufu wa biblia zisomeke kwa makabila ya wahusika wa eneo, ndani ya biblia hizo yaongezwe mafundisho ya haki ya kujitambua na kujitawala wenyewe. Pendekezo hili lilimvutia sana Maranta hivyo akalipa baraka zake, kwa hakika lilifanikiwa na ndio lilizaa hisia kali za mwamko wa kudai uhuru, mfano biblia ya lugha ya kihehe ilikuwa inaeleza wazi athari za kutawaliwa.
Harakati za Ukombozi za Mwalimu Nyerere akiwa na nguvu mpya ya kifikra toka Chuo kikuu, zililivutia kanisa na uungaji mkono ukachagizwa, mfano mwaka 1953 wakati TAA kikiwa chama chenye nguvu kufuatia mabadiliko ya 1948 toka AA kwenda TAA. Askofu Maranta alimwalika ofisini kwake Mwalimu Nyerere, walizungumza mengi lakini kubwa nikuwa alimsifu kwa juhudi za kujipambanua bila kuwaogopa wakoloni, akamweleza jinsi kanisa linavyounga mkono juhudi za ukombozi wa Tanganyika, kisha akamshauri kuwa ajaribu kuvishawishi baadhi ya vyama vya harakati za kiraia viungane ili kuvipa nguvu ya kudai uhuru na kanisa litasaidia.
Wazo la Askofu Maranta lilimkaa Mwalimu Nyerere na mwaka 1954, alianza juhudi za kuwaunganisha vijana wenzake wa kariakoo ambao walikuwa ndani ya TAA na wenye nguvu ya ushawishi lakini wakikabiliwa na matatizo makubwa mawili katika lengo lao ambayo ni Elimu na Woga. Ikumbukwe kuwa mwaka 1953 baada ya harakati za ukombozi kupamba moto na kamata kamata ya wanaukombozi, Askofu Edger Aristide Maranta alihamishiwa Zanzibar na nafasi yake ikachukuliwa na Vicar Apostolic, lakini bado aliendelea kuwa mshauri imara wa Mwalimu Nyerere. Jambo la kushangaza kama si kufurahisha, mwaka huohuo mwezi wa 8, Edger Aristide Maranta alirudishwa tena Dar es Saalam, na sasa mbinyo dhidi ya ukoloni ukashika mkondo wake.
Mnamo tarehe 07/07/1954, Vijana (wazee wa kariakoo) wakiongozwa na Julius Kambarage Nyerere, walikubaliana wazo la kuhuisha chama kutoka TAA kwenda TANU, chini ya uratibu wa karibu wa Wajeisut (Askofu Maranta) na Waislamu (Shehe Issa bin Amir) ijapokuwa alikuwa amefariki mwaka mmoja nyuma, lakini hekima za Shehe huyu zilisaidia. Na zaidi ni kuwa safari ya kwanza ya Mwalimu Nyerere ya kwenda UNO 05/03/1955 Kanisa Katoliki lilitoa msaada kwa chama cha TANU wa tiketi ya ndege ya kwenda na kurudi, lilifanya hivyo kupitia shirika lake la Maryknoll Sisters la New York Marekani,
Si hivyo tu bali katika moja ya utani wa Mwalimu wenye ukweli ndani yake aliwahi kusema kuwa makasisi Walsh na Art Wille wa Shirika la Maryknoll ni maboss wake, akikumbuka malipo ya shilingi 600 angali ameacha kazi ya ualimu akiwa kijijini Butiama.Kuna ushahidi wa kihistoria pia unaochagiza habari hizi kwamba majasusi wa Kanisa walimuandaa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kuja kuwa kiongoza Tanganyika mpya................
Kutoka kwenye kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi.
Unaweza kupakua hapa
www.simgazeti.com
Saa hebu someni niliyoandika kuhusu kitabu cha Yericko:
Wanamajlis,
Bandiko hili limeshawahi kuletwa hapa na nilieleza kuwa kuna makosa mengi.
Inaelekea mwandishi hakubali kuwa kuna makosa.
Kazi ya kisomi inahitaji rejea ili kuthibitisha kinachoelezwa.
Walimu wetu siku zile Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam wakituasa kutoandika
''barua,'' yaani kuandika mada ya kisomi bila rejea.
Hicho hapo juu ni ''barua,'' siyo mada ya kisomi.
African Association haikuasisiwa 1927 bali 1929.
Anaweza kufanya rejea katika, ''Modern Tanzanians,''
John Iliffe (Ed) makala
ya
Daisy Sykes Buruku, ''
Kleist Sykes The Townsman,'' akipenda hata amsome
Mohamed Said, ''The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924-1968)...''
Kleist
Sykes: Pioneer and Man of Ideas 1894 - 1949.''
Akipenda zaidi anaweza kuingia katika Dictionary of Africa Biography, Oxford
University Press 2011, aangalie
Kleist Sykes.
Anasema African Association iliassisiwa Stanley Street si kweli kwani wakati huo
1920s hiyo nyumba ya harakati za siasa ya
Kleist hapo mtaani ilikuwa bado kabisa
haijajengwa.
Nyumba hiyo ilijengwa 1942.
AA iliasisiwa Mission Quarter nyumbani kwa
Cecil Matola Mtaa wa Masasi, nyumba
hii baadae ilinunuliwa na
John Rupia.
Kuna mengi ya kutunga mfano wa
Nyerere kukusanya ''vijana wenzake wa Kariakoo,''
nk. nk. hakuna ukweli wowote
Nyerere hakupatapo kuishi Kariakoo ila kwa muda
mfupi sana 1955 alipokaa nyumbani kwa
Abdul Sykes Stanley Street baada ya kuacha
kazi ya ualimu.
Atakae kujua TANU iliasisiwa vipi sharti kwanza aijue Kamati ya Siasa katika TAA.
Waliokuwa katika kamati ya ndani ya kuasisi TANU ni wajumbe wa TAA Political Subcommittee
wajumbe walikuwa
Mufti Sheikh Hassan bin Amir, Sheikh Said Chaurembo, Abdulwahid
Sykes, Dr. Vedasto Kyaruzi, Steven Mhando, Hamza Mwapachu na
John Rupia.
Safari ya
Mwalimu Nyerere ya kwanza 1955 ilighariimiwa na TANU yenyewe na mratibu
wa safari ile aliyekuwa akikusanya fedha alikuwa
Idd Faiz Mafongo aliyekuwa mweka
hazina wa TANU na Al Jamiatuli Islamiyya fi Tanganyika.
Hebu kwanza tusimame hapa.
Lakini kwa kulisaidia jamvi lau kwa ukumbusho kwa kuwa mada hii ilishajadiliwa miaka mingi
iliyopita nawaomba waingie hapo chini wasome niliyopata kuandika kuhusu historia ya
Tanganyika:
Mohamed Said: LIWALI AHMED SALEH NA SHEIKH SAID CHAUREMBO
Mohamed Said: KUTOKA JF: MAMA DAISY NA HISTORIA YA CHIEF DAVID KIDAHA MAKWAIA
Mohamed Said: KUMBUKUMBU ZA IDDI TOSIRI MWANACHAMA WA TANU KADI NO. 24
Mohamed Said: LAMECK BUGOHE MUASISI WA TANU 1954 KAFARIKI NA KUZIKWA KIMYA KIMYA
Mohamed Said: ZUBERI MWINSHEHE MANGA MTEMVU MZALENDO ALIYEKUWA NA MSIMAMO MKALI WA “AFRIKA KWA WAAFRIKA”
Mohamed Said: Abbas Kleist Sykes 1929 -
Mohamed Said: Idd Faiz Mafongo Mweka Hazina wa Safari ya Nyerere UNO 1955
Mohamed Said: MCHANGO WA MUFTI SHEIKH HASSAN BIN AMEIR KATIKA KUPIGANIA UHURU WA TANGANYIKA MAHOJIANO KATI YA SHEIKH RASHID SALIM NA MOHAMED SAID RADIO NUR ZANZIBAR
Mohamed Said: KUTOKA FB: VITUKO VYA YERICKO ''NYERERE''
Mohamed Said: KUTOKA JF: HISTORIA YA TANU - DK. VEDASTO KYARUZI, KASELLA BANTU NA JULIUS NYERERE
Mohamed Said: Ijue Historia ya Kweli ya Kuasisiwa kwa TANU
Mohamed Said: KUMBUKUMBU YA MASHUJAA WA UHURU WA TANGANYIKA RASHID ALI MELI
Mohamed Said: AZAM TV KIPINDI MAALUM CHA MASHUJAA WA UHURU WA TANGANYIKA
Mohamed Said: KUTOKA JF: SHEIKH HASSAN BIN AMIR ALIVYOIONGOZA TANU KUWA CHAMA CHA KISEKULA
Mohamed Said: KLEIST SYKES (1894 - 1949) KATIKA DICTIONARY OF AFRICAN BIOGRAPHY (DAB) OXFORD UNIVERSITY PRESS, NEW YORK
Wanamajlis,
Hizo hapo juu ni zaidi ya kurasa 100 za kusoma pamoja na audio za kusikiliza
na video za kuangalia.
Si lazima upitie zote chagua moja mbili tatu utakuwa ushajifunza kitu.
Waswahili tuna msemo na
Mzee Ali Hassan Mwinyi akipenda kuutumia,
''Muongo muongoze.''
Chembelecho
Maalim Faiza: Elimu bila Khiyana.
Huyu
Jonathon Glassman ni professor wa historia Northwestern University
Evanston, Chicago alinialika nikazungumze chuoni kwake juu ya historia ya
TANU na uhuru wa Tanganyika.
Nilizungumza katika Ukumbi wa
Eduardo Mondlane.
Glassman alifanya pitioa la kitabu changu katika Cambridge Journal of African
History Vol. 42 Issue 1 March 2001 halikadhalika
John Iliffe.
historia