yericko nyerere sijui unakumbuka ulikuja kuniuzia hicho kitabu ilala amana ofisini kwangu na nikampigia mzee Mohamed Said ukaongee nae nia yngu kubwa nilikuwa nataka uende kuongeza elimu hakika unaitaji kuivishwa zaidi na magwiji km mzee Mohamed Said sio kukalia ubishi km ndugu zetu wa lumumba jaribu kumsoma vizuri mzee wetu utamuelewa nia yke kujaribu kutaka kkujenga zaidi kijana wake lkn naona unataka kuleta ushindani sio na sababu hakika ww ni Kichochi uwezi kuingia kwenye kundi la ninga jaribu kkubari kukoselewa...
Nikushukuru sana mzee wangu kwakunikumbusha vema,
Mohamed Said ni mmoja ya watu muhimu walionifundisha historia, nitakuwa mjinga sana nisipomshukuru na kumheshimu mzee huyu, na katika kitabu changu nimemtaja kama mmoja ya watu muhimu ambao vitabu vyao nimevirejea....
Kitabu tunachokabidhiana hapo kwenye picha ni kitabu cha majaribio tu kikiwa na sura 4 na kurasa 200 tu, lengo la kukichapa ilikuwa ni ushauri wa vyombo vya dola kuona mapokeo ya umma, baada ya mapokeo kuwa mazuri kilihaririwa upya na kuchapwa upya kikiwa na sura 6, kurasa 715, vilelezo 366, vielelezo siri 88, vielelezo huru 34, nyaraka 18 nk....
Kitabu hiki toleo la pili kimechimba historia ya mapinduzi kwa undani wake, hata yale Mzee Mohamed Said na wengine hawakuyajua yamo...
Kimechimba juu ya Abeid Karume, mauaji yake na mapito ya Zanzibar hadi leo hii.
Nje ya hapo kitabu kimebadili kabisa ngano za Mohamed Said juu ya historia ya Uhuru wa Tanganyika, Yale asiyoyapenda Mohamed yote yameletwa pamoja, hasa hasa uratibu na ushiriki wa Kanisa katoliki kupitia shirika lake la kijasusi la Jeisuti juu ya Uhuru wa Tanganyika...
Mambo haya ni mapya kwa Mohamed Said na wengine....ni lazima alipuke kwa hofu...
Mwaka 2013 tulikutana hapa jamvini katika mjadala uliochukua mwaka mzima hapa mimi nikikosoa ngano za Mzee Mohamed juu ya Uhuru akiunasibisha na uislamu wa Dar na kuwatenga waamini wengine kabisa... Nilimuonya kuwa mimi nitazifuta ngano zake na kusimama kwenye mlengo mwingine kabisa... Naam nimefanya hivyo... Leo watu wamejua nani alikuwa nyuma ya uhuru, nani alikuwa nyuma ya Julius Nyerere, nani alikuwa kiungo muhimu mpaka uhuru....
Haya ni mageni kwa Mohamed, mlipuko wake niliutaraji, hapa analipuka huku bado kabisa hata kitabu hajakisoma kabisa, ila anaona hizi dondoo tu ameanza kuja na kejeli na matusi lukuki dhidi yangu...
Kitabu kimeshapata sifa ya kitaifa na kimataifa, yeye amesema hakinunuliki, sijui anataka aje niwe namuonyesha kuwa huyu kanunua na yule kanunua....
Wataalamu na wasomi leo wanapendekeza nitunukiwe shahada mbili za uzamivu kwa kuandika kitabu kimoja tu, na wamefurahishwa sana katika historia na ujasusi.... Leo mzee wa ngano za kariakoo anakuja na matusi juu...
Katika madai ya Mzee Mohamed anasema kwamba nimenakili yaliyoandikwa, ukweli nikuwa wa wale waliobahatika kukisoma kitabu changu wataona maandishi yote yakunakili yanamarejeo na nyaraka mwishoni nyuma ya kitabu... Labda uwe mvivu na mwenye wivu uliovuka mipaka kama wa mzee Mohamed Said.
Nikushauri kama ulivyotushauri sisi kipindi kile 2013 kwamba historia yako tuipinge kwa kuandika kitabu, nawe ni wakati wakupinga kitabu cha Ujasusi wa Kidola naKiuchumi kwakuandika kitabu, nje ya hapo ni porojo tu mzee.... Na zaidi unanisaidia sana kunadi kitabu... Weekend nitakutafuta tupate sharubati na vibansi pamoja