Askari JWTZ mwenye asili ya Rwanda atoroka jeshini!

Askari JWTZ mwenye asili ya Rwanda atoroka jeshini!

Status
Not open for further replies.
Aisee, ebu fuatilia vizuri au tusubiri taarifa ya jeeshi ndo tuweze kujadili maana mi naona mamluki zaidi ni huyu jamaa aliyeweka hii thread, hana uhakika, nyaraka za jeshi usifikiri ni kama vitabu vya M pesa.

Ila hata kama ni hivo sishangai kwani snowden mbona katoboa siri za nchi yake USA...?sema kwakuwa Rwanda ndo hivo haipendwi chochote kitasemwa tu.
 
Kuwa mwanajeshi hakumaanishi kujua siri za nchi Hata usalama wa taifa sio wote wanafahamu siri za nchi. Wanafahamu siri za kazi zao sio siri za nchi.
 
Ndiyo tatizo la kukubali kila takataka inayoomba kuwa raia kukubaliwa!! Hii inaonyesha wahusika hawafanyi inteligensia inayotakiwa!! Hii RUSHWA!!!
Nakubaliana na wewe mkuu,hili la kumpa mtu uraia bila kuangalia historia yake limetufikisha hapa tulipo,wamfuatilie kama Edward snowden
 
Du, ipo kazi! Ila kama ni kweli Jeshi wafanye scrutinizing kwa waajiriwa wote, najua kuna gharama kwa hili ila itasaidia sana kuweza kuwatambua nani mamluki!
Kuna Pastor mmoja alishawahi tamka kwamba nchi jirani imeingiza wanajeshi kwa nchi yetu, je swala hulo lilifanyiwa kazi ama liliachwa tu juujuu likielea?


Cosmo
Mimi nilisema siku nyingi kwamba kiburi cha Kagame si bure. Ana watu wa kutosha sana ndani ya jeshi letu la wananchi ndiyo maana anapata kiburi kiasi hicho. Na hii itatugharimu sana katika mahusiano yetu na hawa majirani. Na ile kauli ya kwamba atatafuta angle nzuri ampige Kikwete, ninapata hofu kwamba isijekuwa ni style kama ile aliyomuulia Laurent Kabila. Maana Kagame hana dogo.

Na akiua kwa style ile ya Kabila sijui hata tutapata wapi vielelezo vya kumshitaki au kumshambulia Kagame. Stay tuned guys, tusishangae kwamba hata walinzi wa Kikwete ni Wanyarwanda.
 
Nadhani sasa, hata hivi vitambulisho vya Taifa, wasubiri kwanza mpaka tupekuane mmoja mmoja, tufahamiane nani ni nani. Hila kwa hulka ya viongizi hawa na chama hiki kichafu, haya mambo yatapita bila uzalendo wowote.

Hawa watu wa aina hii wapo wengi hata TBC na HAZINA, wapo mbona!!!.
 
makubwa haya lazima tujipange mbona wapo viongozi wengi tu warundi
 
Mtikila alishasema Kagame ana "wanajeshi wake kwenye JWTZ", watu wakampuuza, sasa huu ni mfano mmoja wapo tu....

Mambo ya Intelligensia yana siri kubwa ambazo wakati mwingine hatuwezi kuzielewa kirahisi.Tunaweza kuwa na wanyarwanda ndani ya Jeshi na bado tukawatumia haohao kusecure information kutoka kwao.

Kumbuka NSA leaker Edward Snowden wa marekani ambaye ameomba asylum nchini Russia. Watu wanaojua Intelligensia vizuri wanajua kinachoendela na usidhani Marekani ni wajinga kiasi hicho, pale ni kwamba mtu kuna task amepewa. Hivyo hata ikitokea hapa kwetu, tunakimbilia kuilaumu Intelligensia yetu bila kujua kinachoendelea.

How sure ni Intelligency personnel wangapi wa Tanzania wapo katika nchi mbalimbali Duniani? achilia mbali hiyo Rwanda? sometimes tusipende kubeza vyombo vyetu vya usalama maana wanajua wanachokifanya.Kwani Mtikila ni mtu wa usalama wa Taifa? jiulize hizo habari anazipata wapi? kama Mtikila anafahamu, anapata habari kwa watu wa ndani wanaojua kinachoendelea na pengine hawampatii habari yakinifu kwa kuwa siyo kila mwana-usalama anaelewe kila kinachoendelea unless awe ngazi ya juu.

Na wewe katika maisha yako ya kila siku lazima ujiwekee self-intelligency na hasa pale unapokuwa na madaraka kazini, kiongozi wa siasa au kuwa na mali nyingi, utundu wa kudodosa mazingira yanayokuzunguka ni jambo muhimu. Hivyo ondoeni hofu isiyokuwa ya lazima katika hili.
 
Kuishi vema na mjirani ndiyo suluhisho bora kwa migogoro

Sisa za visasi ni hatari siku zote. Nazo ni za Kikwete na ccm

Mnashangaa ya mwanajeshi, mbona katibu mkuu ccm ni:-
-Msomali
-fisadi mkuu wa maliasili zetu hususan tembo

Simwingine ni KINANA
 
alikuwa akifanya kazi katika kitengo chateknolojia ya mawasiliano ya kijeshi (IT).

Kwa mujibu ya gazeti la mtanzania alikuwa department ya IT jeshin, na alikuwa ni ofisa wa rank ya luten kanali..so ni mtu mkubwa na kama alikuwa mole wa Rwanda manake ametuma information nyingi na nyeti sana.

Anaweza kuwa na access ya database ya JWTZ na kujua idadi ya askari na silaha, pia deployment ya makambi na strength za kila kajbi. Pia anauwezo wa kujua strategic areas katika jeshi. Ni kitengo sensitive sana. Department ya IT ni kama moyo wa jeshi manake kila kitu kinakuwa pale kwenye database.
 
Kuishi vema na mjirani ndiyo suluhisho bora kwa migogoro

Sisa za visasi ni hatari siku zote. Nazo ni za Kikwete na ccm

Mnashangaa ya mwanajeshi, mbona katibu mkuu ccm ni:-
-Msomali
-fisadi mkuu wa maliasili zetu hususan tembo

Simwingine ni KINANA

Licha ya Kuwa Katibu wa CCM, Huyo alishakuwa Mwanajeshi mwenye cheo kikubwa tu Jeshini
 
Kama alikuwa private hawezi kuwa na Siri zozote za maana, unless Kama alikuwa na cheo cha juu!
https://www.jamiiforums.com/jamii-intelligence/507158-ofisa-jwtz-ahofiwa-kutorokea-rwanda.html
Tulishasema humu JF kuwa hata Jukwaa hili wamo sembuse Ikulu
Jmani hawa watu sio wzuri yaani ni lazima watarudi kwao au kuueneza Ukabila tofauti na mmasai, Mjaluo Mchagga nk Mbantu yeyote si Mtutsi!!!!!!!!!!!!!!
Bado tutamkumbuika Mtikila
Maana tukisema ukweli watu wanadai mna ukabila
 
Kazi ndogo hiyo, sanasana anajisumbua tutamkamata popote alipo labda asiende chooni.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom