Askari mstaafu: Walichofanya Mdee na wenzake pale Segerea ni sawa na Gari kugonga Treni kwenye "Railway cross Road"

Nj Ni kweli Polepole alikwenda pale na watu je alikiuka taratibu za kuingia gerezani? Alitumia mabavu? Kusema ni kifungu kipi kimevunjwa subiri hati ya mashitaka itoke kwa mwanasheria. Ila usimpuuze huyu mzee maana gari moshi ligongwa na gari...Pia usimdharau maana humjui.
 
Jeshini hawafanyi kazi kwa hisia ni Kanuni, Taratibu na Amri, ukishindwa kufuata kanuni na taratibu unapewa amri usipotii ni kukusurutisha na kipigo juu kufuata amri.

Sent using Jamii Forums mobile app

..Nakubaliana na wewe.

..lakini Magereza hawakutumia kanuni na taratibu wakati ccm wanamtoa Dr.Mashinji na walipojaribu kumtoa Mch.Msigwa.

..Magereza wangewaruhusu CDM kumtoa mwenyekiti wao kwa utaratibu uliotumiwa na CCM kumtoa Dr.Mashinji tabu yote hii isingetokea.

..Zoezi hili lilikwenda vizuri kwa vyama vyote kwanini liharibiwe dakika za mwisho, wakati mfungwa wa mwisho, Mh.Mbowe, anatolewa?
 
Wee mjing### unahangaika sana
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bwashee mtu akikusimulia jambo usimuache bila kumuuliza hivyo vifungu, ukimuacha na kukimbilia kutundika uzi huku na sisi wasomaji tutakuuliza wewe juu ya vifungu hivyo.
Kifungu cha Railway cross Road mbona kinajulikana bwashee!
 
Uzuri tabia zao zinajulikana kuanzia bungeni kwa kupenda kulazimisha mambo.

Sugu aliwahi kubebwa msobe msobe na askari kumtoa ndani ya ukumbi wa bunge na walipofika nje walimtupa kama gunia na kumtimbatimba

Askari hafundishwi kazi na raia bwashee!

..chanzo cha yote haya ni UPENDELEO kwa ccm.

..kukumbushia ya bungeni unazidi kutetea hoja yangu.

..rejea tukio la Mh.Mnyika kutolewa bungeni na askari na baadae kuadhibiwa na Spika.

..Mh.Mnyika alikuwa anamlalamikia Spika kwa kutomchukulia hatua mbunge wa ccm aliyemtukana.

..lakini kilichotokea ni Spika kumuadhibu Mnyika.

..Again, tatizo na chanzo cha yote haya ni UPENDELEO kwa chama cha mapinduzi.
 
Mimi sijawahi kuwaita CHADEMA nyumbu! Lakini kwa hoja yako hii ya CCM walienda kumlaki Mashinji hivyo lazima CHADEMA wamwendee Mbowe basi sisemi kama ni nyumbu au siyo!
 
Hizo amri wanazo toa wanatoa bila kuwepo sheria inayowaruhusu kutoa amri zao hizo?.
 
tulishawajua tangu zamani,serekali ya CCM mkosaji ni mpinzani siku zote,hata kama atafanya kilekile ambacho CCM wanakifanya, wapinzani ndiowataonekana kuwa wamevunja sheria wakati wamepita njia ileile na kufanya kilekile kilichofanywa na CCM.
 
Hii tabia ya kupenda kukandamizana ni moja ya sababu kubwa hatuendelei.

Na mkiendelea kusifia ujinga hivi mtakuwa masikini wajinga daima.

Sent from my typewriter using Tapatalk

Exactly,

Mkuu Kiranga bila kujali itikadi yoyote miaka ya karibuni kumeibuka aina ya reasoning ya “kimbayuwayu” ambapo huwa tunadhani maendeleo na usawa/ustawi wa binafamu vinahawanyika.
 
Exactly,

Mkuu Kiranga bila kujali itikadi yoyote miaka ya karibuni kumeibuka aina ya reasoning ya “kimbayuwayu” ambapo huwa tunadhani maendeleo na usawa/ustawi wa binafamu vinahawanyika.
Kuna wajinga wanasifia kuvunjwa kwa haki magerezani leo.

Kama vile wanajua kesho yao itakuwa vipi.

Sent from my typewriter using Tapatalk
 
Hayo ni matumizi mabaya ya dola aliyosema bashiru. Waliochana sare ya askari ni mapandikizi ya ccm.
Toka lini au ulisikia wapi siasa zinaenda kufanywa gerezani tatizo la upinzani wanataka sana watanzania na dunia nzima iwaonee huruma au wahalalishe uvunjaji wa sheria kisa tu ni wanasiasa wana haki ya kufanya demokrasia !
 
Eti hawana mikakati, kama watu wananyimwa haki yao ya kikatiba kufanya kazi za kisiasa jaribu kutumia akili hata kwa asilimia moja
 
Na pole pole je?
 
Akili za kiafrika katika ubora wake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…