Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Jeshi la polisi mkoani Iringa linamsaka Askari wa Jeshi hilo aliyefahamika kwa jina la Sajenti Rogers wa Kituo cha Polisi Ipogolo na Askari wa jeshi la Akiba aitwaye Thomas Mkembela kwa tuhuma za kumuua Nashon Kiyeyeu mwenye umri wa miaka 23, Mkazi wa Nyamuhanga, Manispaa ya Iringa aliyekuwa anatuhumiwa kwa wizi wa simu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa SACP Alan Bukumbi amesema Disemba 14, Sajenti Rogers alipokea taarifa kutoka kwa mwananchi ambaye hakumtaja jina kuwa mtuhumiwa Nashon alimwibia simu yake.
Ameeleza kuwa bila kutoa taarifa kituoni, Sajenti Rogers kwa kushirikiana na Mgambo huyo walimkamata mtuhumiwa na inadaiwa walimpiga na walipoona amepoteza fahamu, walimpeleka hospitali moja binafsi na baadaye kumhamishia, hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa ambako ilibainika mtuhumiwa, Nashon Kiyeyeu alikuwa ameshafariki.