Mkuu
peno hasegawa, wengi humu tunajuana ki jeiefu jeiefu lakini hatujuani background, mimi kwanza ni mwanafamilia ya wale "jamaa zetu" kwa baba na mama!, na baada ya JKT, niliunganisha direct JWTZ, ndipo nikaja kwenda TSJ!, hivyo mimi licha ya kuwa ni mwandishi wa habari wa kujitegemea na mtangazaji wa kujitegemea, pia ni mjeda!.
Kwenye majeshi yote matatu, yaani JWTZ, Polisi na wale "jamaa zetu", huwa wana watu wanaitwa,snipers, hawa ni sharp shooters ambao they can never miss a target, kwa jeshi la magereza, uhamiaji na Zimamoto sijui pia kama nao wana snipers.
Kazi ya hawa snipers ni moja tuu, a smooth elimination!, hii hufanyika kwenye operations zao zinazoitwa ama overt ama covert, ila ili hii elimination ifanyike lazima Amiri Jeshi Mkuu, aithinishe ile covert operation.
Ila ikitokea a very dangerous situations ambapo kusubiri authorization ya elimination from competent authorities, will warrants more security risks, then Mkuu wa operation hiyo anaweza kutoa elimination order ma snipers wakatimiza elimination, kisha kuandika maelezo kwe report kwa nini he authorized hiyo elimination.
Majeshi yote ni territorial, yana kitu kinachoitwa territorial jurisdiction, askari wowote hawezi kuvuka territory yake bila kitu kinachoitwa movement order!, hivyo polisi wa Dar hawezi kwenda Moshi bila idhini, ila kwenye covert operation hakuna cha territory ni unakwenda popote, and sometimes kwa askari wa mipakani sometimes unavuka border kufanya tikio nchi jirani ilimradi ulikamilishe na kurejea bila kujulikana!.
Eliminations hufanyika kunapotokea mtu yoyote anapokuwa ni a threat to national security hivyo anapaswa kuondoshwa ASAP!.
Hii elimination hufanywa kwa watu wa aina mbili
1. Outsiders na huitwa outside job
2. Insiders na huitwa an inside job
Outsiders ni watu wa nje ya mfumo rasmi
Watu hawa outside elimination ni watu kama
1. Majambazi ya hatari, ambayo wamefanya matukio mengi ya ujambazi na kila yakiwekewa mtego, yanapiga tukio na kupotea hiyo yanakuwa hayakamatiki hivyo picha zao zinakuwa seculeted kwenye security corridors zote kwa mtu huyu akionekana popote, msijaribu kumkamata, do him away!.
Hili la Polisi kuruhusiwa 'kuwanyanganya' silaha majambazi na kupandishwa vyeo limekaaje?
2. Mtu akipata wazimu akashika silaha na kuanza ku shoot randomly, kum contain mtu kama huyu, snipers wanatumwa kumuwahi kabla hajaleta madhara zaidi, kama lile tukio la ubalozi wa Ufaransa na Hamza Hassan
View: https://www.youtube.com/live/u7H-rawlsE0?si=vKQZ0Q6FOKx2Y8Ef hii ilikuwa ni overt operations, operations nyingi za hawa jamaa ni covert operations.
3. Wanasiasa ambao the status quo inawaona wakiachwa, wata pose risks kwa the status quo, hivyo they have to be eliminated, hivi ndio kama ilivyowatokea wanasiasa mbalimbali wa upinzani kote duniani, yule Paulo Mrefu, huwa anawafuta hadi wale walioikimbia nchi yake, anawatumia watu kumalizana nao huko huko walipo. Mfano mzuri ni tukio la shambulio la Lissu
Shambulio la Lissu: Wajue wasiojulikana watakaojulikana na 'Wasiojulikana' ambao kamwe, hawatajulikana
3. Waandishi wa habari za uchunguzi ambao wanaibua madudu ya ajabu ya serikali hivyo kupose risks kwa status quo kama Azory Gwanda na Ben Saanane
Waandishi wa Habari na Kupotea/Vifo vya Kutatanisha, Toka Katabalo, Saanane, Gwanda, Mwangosi, Isango. Ni Ama Tuombe Mungu Atunusuru ama...
4. Wanaharakati hatari kwa status quo kama Mchungaji Mtikila. Baada ya kushinda ile kesi ya mgombea binafsi, alipanga kufungua shauri jingine kukazia ile hukumu, they did him away in ana accident look a like!.
Kwa inside jobs
1. Askari wakiwa vitani, askari anayewasaliti, they do him away ASAP
2. Dissidents wa ndani ya chama, watu powerful ndani ya chama au serikali halafu they have gone astray, they do them away kama Horace Kolimba,
3. Wale jamaa zetu, wakitumwa a very dangerous mission, wakiisha ifanikisha, ili to seal the loopholes, Idara inaweza kuamua to silence them by doing them away!.
4. Powerful people ambao wame fall out of grace of the status quo, mfano Imran Kombe, kwanza they'll try zile ordinary means kama anthrax, polonium or accident look a like, ikishindikana ndio unatumia snipers.
Snipers kama wa Imran Kombe, ili kuepusha soo, unawakamata, unawashitaki ili serikali iepuke kuchafuka, Mahakama inawahukumu, wanaonekana wamekwenda jela, halafu hakuna gereza limewapokea, wanapelekwa uhamishoni kwa kutumia kitu kama witness protection strategy with new names new countries, new jobs na kuendelea na maisha huko, aliko kifungo kikiisha anarejea nyumbani, majina yao hayaondolewi kwenye payroll.
P.