Askari Polisi Mwita Milumbe adaiwa kuteswa na kuuwawa, Ndugu waomba msaada

Mawele

Platinum Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
1,161
Reaction score
4,251


​

POLISI MWITA MILUMBE ATESWA NA KUUWAWA , NDUGU WAONBA MSAADA.

Habari ya kazi kaka Mwaipaya. Mimi, kama mmoja wa wanafamilia, tunaomba msaada wa kutupazia sauti kuhusu Jeshi la Polisi Tanzania.Mkoani Tanga kuna unyama wamefanyiwa mdogo wangu kwa kutokukubali kuwa upande wa mauaji na utekaji wao.

Amekuwa akipinga mpaka akahamishwa kituo cha kazi kutoka Dar es Salaam, Ukonga, kwenda Tanga.Jeshi la Polisi lilimshikilia ndugu yangu, Mwita Mecky Milumbe, mwenye force namba H.1796, kuanzia tarehe 21 mpaka tarehe 28, tulipopata simu kutoka kwa watu wa karibu naye wa kituo cha Tanga kuwa amefariki kwa kujinyonga.

Lakini hajajinyonga. Wamempeleka msituni, wamemtesa sana wakiwa wamemfunga pingu, ikiwa ni pamoja na kumkata visigino, kumkata pua, kung’oa kucha, kumtoboa macho na kumuingizia chupa sehemu za haja. Kisha wakamrudisha mahabusu na kumtundika kwa T-shirt yake.Mtu aliyetuandalia taarifa alituambia tusimtaje kwa kuwa tutamuharibia kwa viongozi wake.

Naomba msaada wako kutupazia hili. Yote haya ni kwa sababu ya kupinga utekaji ambao walikuwa wanatakiwa kuufanya yeye kama mmoja wa Special Field Force Unit.Mpaka sasa wametukabidhi mwili, lakini wamezuia simu zake na wamekatalia kushiriki kwa chochote katika mazishi.Msiba upo Kitunda Mwanagati, njia panda ya kwenda Kibeberu.

Ukiwa hapo panapoitwa Nyangasa, kama unaenda Mwanagati, ukiuliza kwa Mama Mwita utaelekezwa. Mama yake ni maarufu kwa kufuga nguruwe.Polisi walileta tu mwili na wakaondoka jana jioni Tarehe 30.8.2026 saa 10, na hakubaki hata mmoja.

​
Pia soma:Polisi Tanga: Askari Mwita alifariki kwa Kujinyonga, Uchunguzi unaendelea
 
Kumuingiza Chupa.
Kung'oa Kucha.
Kukata visigino.
Kutoboa Macho.

Ukishiriki moja usipinge kumi mapya utakayoletewa.
Ndiyoo, Kaa subiri Simu ili uone picha na uzisikie sauti kinyume na hapo usiporuhusiwa kuwaona utaskia sauti ambazo hutazisikia daima.
Mapigo na Mwendo.
 
Mimi nahisi, huyu kosa lake ni kumpa maji Kazungu Bakari Kazungu(kada wa CCM) kipindi walipomteka. Nadhani huyu CCM alitakiwa wamuue hawakumuua. So kutokana na misimamo yake wakaona atavujisha siri.

Huyu Abdul anawadanganya. Wote mnaohusika na mauaji ya ndugu zetu mtajulikana. Ni jambo la muda tu
 
Uskute mnapindisha stori! Mbona ana sura ya utekaji!
Mimi mwenyewe nikionaga askari kapanda ana mibavu ntakuwa ninamashaka na wale watekaji, haiwe
Siku wakikufikia ndio utajua wanajuana wenyewe
Mkuu mimi likija suala la polisi kuumizana wao kwa wao hata sishtuki aiseeee kwa sababu Mwanza mdogo wangu alikuwa ni mmoja ya waliokuwa kwenye Banda la mpira waliomiminiwa risasi na hao polisi bila huruma ni Bora wangemchukua wakamfunga maisha tukawa tunamtembelea hata Kila mwisho wa mwaka
 



Habari ya kazi kaka. Mimi, kama mmoja wa wanafamilia, tunaomba msaada wa kutupazia sauti kuhusu Jeshi la Polisi Tanzania.

Mkoani Tanga kuna unyama wamefanyiwa mdogo wangu kwa kutokukubali kuwa upande wa mauaji na utekaji wao. Amekuwa akipinga mpaka akahamishwa kituo cha kazi kutoka Dar es Salaam, Ukonga, kwenda Tanga.

Jeshi la Polisi lilimshikilia ndugu yangu, Mwita Mecky Milumbe, mwenye force namba H.1796, kuanzia tarehe 21 mpaka tarehe 28, tulipopata simu kutoka kwa watu wa karibu naye wa kituo cha Tanga kuwa amefariki kwa kujinyonga.

Lakini hajajinyonga. Wamempeleka msituni, wamemtesa sana wakiwa wamemfunga pingu, ikiwa ni pamoja na kumkata visigino, kumkata pua, kung’oa kucha, kumtoboa macho na kumuingizia chupa sehemu za haja. Kisha wakamrudisha mahabusu na kumtundika kwa T-shirt yake.

Mtu aliyetuandalia taarifa alituambia tusimtaje kwa kuwa tutamuharibia kwa viongozi wake.

Naomba msaada wako kutupazia hili. Yote haya ni kwa sababu ya kupinga utekaji ambao walikuwa wanatakiwa kuufanya yeye kama mmoja wa Special Field Force Unit.

Mpaka sasa wametukabidhi mwili, lakini wamezuia simu zake na wamekatalia kushiriki kwa chochote katika mazishi.

Msiba upo Kitunda Mwanagati, njia panda ya kwenda Kibeberu. Ukiwa hapo panapoitwa Nyangasa, kama unaenda Mwanagati, ukiuliza kwa Mama Mwita utaelekezwa. Mama yake ni maarufu kwa kufuga nguruwe.

Polisi walileta tu mwili na wakaondoka jana jioni Tarehe 30.8.2026 saa 10, na hakubaki hata mmoja.
 
 

Attachments

  • IMG-20260829-WA0027.jpg
    326.2 KB · Views: 15
  • 1000024076.jpg
    45.1 KB · Views: 12
  • IMG-20260827-WA0003.jpg
    82 KB · Views: 13
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…