POLISI MWITA MILUMBE ATESWA NA KUUWAWA , NDUGU WAONBA MSAADA.
Habari ya kazi kaka Mwaipaya. Mimi, kama mmoja wa wanafamilia, tunaomba msaada wa kutupazia sauti kuhusu Jeshi la Polisi Tanzania.Mkoani Tanga kuna unyama wamefanyiwa mdogo wangu kwa kutokukubali kuwa upande wa mauaji na utekaji wao.
Amekuwa akipinga mpaka akahamishwa kituo cha kazi kutoka Dar es Salaam, Ukonga, kwenda Tanga.Jeshi la Polisi lilimshikilia ndugu yangu, Mwita Mecky Milumbe, mwenye force namba H.1796, kuanzia tarehe 21 mpaka tarehe 28, tulipopata simu kutoka kwa watu wa karibu naye wa kituo cha Tanga kuwa amefariki kwa kujinyonga.
Lakini hajajinyonga. Wamempeleka msituni, wamemtesa sana wakiwa wamemfunga pingu, ikiwa ni pamoja na kumkata visigino, kumkata pua, kung’oa kucha, kumtoboa macho na kumuingizia chupa sehemu za haja. Kisha wakamrudisha mahabusu na kumtundika kwa T-shirt yake.Mtu aliyetuandalia taarifa alituambia tusimtaje kwa kuwa tutamuharibia kwa viongozi wake.
Naomba msaada wako kutupazia hili. Yote haya ni kwa sababu ya kupinga utekaji ambao walikuwa wanatakiwa kuufanya yeye kama mmoja wa Special Field Force Unit.Mpaka sasa wametukabidhi mwili, lakini wamezuia simu zake na wamekatalia kushiriki kwa chochote katika mazishi.Msiba upo Kitunda Mwanagati, njia panda ya kwenda Kibeberu.
Ukiwa hapo panapoitwa Nyangasa, kama unaenda Mwanagati, ukiuliza kwa Mama Mwita utaelekezwa. Mama yake ni maarufu kwa kufuga nguruwe.Polisi walileta tu mwili na wakaondoka jana jioni Tarehe 30.8.2026 saa 10, na hakubaki hata mmoja.