Askari Polisi wa Dar aliyetajwa na Rais Samia arejeshwe ili kudhibiti ujambazi ni nani?

aliyekuwa ocd kigamboni , anastahili aliituliza kigamboni sasa kahamishwa sijui kapelekwa wapi
 
Huyo kamanda ni Liberatus Matheus Sabas. Jamaa ni noma, kila alipopita majambazi waliufyata. Lakini kwa ngazi aliyofikia sio sawa tena kumleta Dar itakuwa kumshusha, alishavuka hatua hizo mbali.
Nadhani mhe Rais alimaanisha kwamba IGP atengeneze makamanda wengine wa aina ile, na nimemuona akipokea agizo hilo kwa saluti.
 
Na ataendelea kuwatesa hadi kizazi chenu cha kumi!
Aaah wapi! Labda anakutesa wewe unayeshinda ukimlilia! Wengine hivi sasa tuko huru ila yeye mwenyewe huko alipo bila shaka anateseka vilivyo akichezea mateso ya milele.
JPM was one the rare African Leader species born in our time ndio maana pamoja na kwamba aliishafariki,
Ni kweli, alikuwa rare species indeed! Ni mara chache sana unakutana na binadamu mwenye roho mbaya kama mwendazake. Wengi lazima tu wanasherehekea kifo chake
JF HAIWEZI kukaa bila threads zake na ikabaki salama! That's Legacy fella!!!!
Naam, legacy kama ya Adolf Hitler ambaye pamoja na kufa na kuwa mzoga kwa miaka zaidi ya sabini bado anakumbukwa kwa uovu wake! Legacy my foot!
 
Una uelewa sana mkuu hongera.
 
Duh kunaweza kuwa na ukweli hapa.
 
Namanisha mkuu wa mkoa so bashite anaweza rudi
 
Mnajitahidi sana kumkwamisha Mama SSH na chokochoko zenu lakini hamtoweza kamwe.Mmebaki tu kulaumu hata pasipo na sababu.Tulieni dawa iwaingie..mwendazake ameshalala milele.
Tatizo sio kulala kwake, ila ni falsafa yake aliyoiacha kwenye mioyo ya watanzania wenye utimamu wa akili kuhoji mambo y msingi 😎.
Mama anaanza kupuyanga mapema mno. Moja ya jukumu kubwa alilonalo ni kufuatilia mambo kwa kina ili kuepuka kutoa majibu yanayoacha maswali ktk kutatua changamoto zinazolikabili Taifa letu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…