Mimi siumii namtakia Mema Mama kwasababu mimi ni muumini wa Falsafa si watu ila natamani mama akaze buti na akifanikiwa Imefanikiwa Nchi yangu Tanzania, watu wanamchukulia poa mama naona. Pia mitandaoni kila siku kuna nini? Kwamba mama hana vyombo, "utasikia nimesikia mitandaoni" Idara zetu zile za juu ziko wapi kumpa mama Taarifa? Mitandao ni mizuri kwamba inaweza toa taarifa ambayo si biasi but kuna muda mitandao inatoa taarifa ambazo ni biasi. Narudia tena, Molali ya Askari na hasa wa Juu inategemea sana Mama wanamsoma vipi? Naona kama bado anachukuliwa poa au bado hajaeleweka hasa dira yake kuhusu mambo ya kukomesha ujambazi. Nchi hii inahitaji ushujaa kidogo, kuna watu (baadhi) ni wagumu kuelewa.
Sitapenda Mazuri waliyoyafanya na Hayati akiwa top yapotee yaani arudi nyuma halafu watanzania waanze sema ona tumerudi nyuma. Natamani Watanzania waseme, ona tumesonga mbele zaidi ya tulipokuwa. Itakuwa Raha kwa nchi yetu Tanzania.