HOJA Askari Polisi Wastaafu tulipwe stahiki zinazoendana na uhalisia, kiasi tunachopewa ni kidogo sana

HOJA Askari Polisi Wastaafu tulipwe stahiki zinazoendana na uhalisia, kiasi tunachopewa ni kidogo sana

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Sisi askari wastaafu tunaeleza haya kwa uchungu mkubwa sana kero na dhuluma inayotupata wastaafu kutoka kwa viongozi wetu.

Hivi karibuni kuna Viongozi walisema kwamba sisi tunaolalamika kwamba tulishindwa "kujiandaa" kabla ya kustaafu!

Wanasema eti tulipostafu tulishindwa kujiandaa wakati tulipoingia uraiani. Hiyo kauli ina maana gani? Kujiandaa wanamaanisha nini kuchukua rushwa au? Wanataka askari ashindwe kutenda ukweli na uaminifu kazini kwake kwa sababu tu anaambiwa "alishindwa kujiandaa"?

Kuna waliofanya kazi Serikalini kwa zaidi ya miaka 30 lakini wanakuja kupewa shilingi milioni 29! Kisha nyingine wanasema watatupa taratibu, badala ya kutulipa fedha zetu zote kwa pamoja baada ya kulitumikia taifa hili kwa miaka zaidi yote hiyo, wanatupa fedha hizo kidogo kidogo, wanakata na kukokotoa wanavyotaka wao!

Wanatupa labda laki tatu na nusu au laki mbili, tena kwa kusuasua kila mwezi. Hivi hizo pesa ndogondogo zinasaidia nini kwa mtu aliyestaafu ambaye bado ana watoto wanaosoma na wanahitaji ada na mahitaji mengine?

Mtu amepambana na kulitumikia taifa miaka 34 au zaidi, halafu leo anapewa shilingi milioni 29 kidogo kidogo kana kwamba wanatufanyia biashara na fedha zetu!

Hali hii inatufanya wastaafu wengi tuishi kwa shida na dhiki kubwa, na wengine wanajikuta wanakufa kwa mawazo na shinikizo la damu, au hata kujinyonga kwa sababu ya maisha magumu huku haki zao zikiwa zimeshikiliwa.

Tena ukitaka kujitokeza kuongea na kulalamika, unakabiliwa na vitisho na hofu ya kutekwa au kufanyiwa mambo mabaya! Ndio maana askari wengi wadogo wanaumia na kulia kimya kimya lakini viongozi wa juu hawajali kwa sababu wao wana mifuko mikubwa.

Wito wangu na ombi letu kubwa kwa serikali na uongozi wa Jeshi la Polisi na Jeshi la Magereza kote nchini (ikiwemo Mkoani Manyara na Tanzania nzima): Tulipeni stahiki zetu zote kwa mkupuo mmoja bila kutukata wala kutulipa kidogo kidogo!

Tulipeni pesa zetu zote tulizozifanyia kazi kwa jasho na uaminifu wetu ili tukazitumie kujikimu na kusomesha familia zetu.
Mimi nashauri wawapunguzie zaidi. Kwani hela mnazovuna kupitia rushwa ni nyingi mno.
 
Hii ni baada ya kikokotoo maana yake kusingekuwa na kikotoo wangekuwa wana uhafadhali sana
Miaka 30 unapata m29? Hata darasa la saba sidhani kama anapaata hii......ukiingia na elimu ndogo unatakiwa ujibusti taratibu sasa ukilala tu kwenye malindo mbaka unazeeka ni tatizoo
 
Hizi lawama zingefika chamani, na hapo uliposema umelitumikia taifa ungesema umeitumikia CCM maana wamesema nyie ni mali yao
 

Na Tunampango Wa Kupunguza Hata Hicho Unachoona Ni Kidogo...
Na Nakuhakikishia Lakufanya Kamwe Hamna...
​
 
Sisi Askari Wastaafu tunaeleza haya kwa uchungu mkubwa sana, hivi karibuni kuna Viongozi walisema sisi tunaolalamika kwamba tulishindwa "kujiandaa" kabla ya kustaafu!

Wanasema eti tulipostaafu tulishindwa kujiandaa wakati tulipokuwa tukikaribia kuingia uraiani. Hiyo kauli ina maana gani? Kujiandaa wanamaanisha nini kuchukua rushwa au? Kwa mshahara upi? Wanataka askari ashindwe kutenda ukweli na uaminifu kazini kwake sababu tu anaambiwa "alishindwa kujiandaa"?

Kuna waliofanya kazi Serikalini kwa zaidi ya miaka 30 lakini wanakuja kupewa shilingi milioni 29! Kisha nyingine wanasema watatupa taratibu, badala ya kutulipa fedha zetu zote kwa pamoja baada ya kulitumikia taifa hili kwa miaka zaidi yote hiyo, wanatupa fedha hizo kidogo kidogo, wanakata na kukokotoa wanavyotaka wao!

Wenzetu huo Dar es Salaam walilalamika mara kadhaa kuhusu hili lakini hakuna hatua zilizochukuliwa. Wengi wetu wanasita kujitokeza kuzungumza hadharani sababu kuna matukio ya watu kupote ambayo tunayasikia, hivyo tunanun'gunika tu chinichini.

Wanatupa labda laki tatu na nusu au laki mbili, tena kwa kusuasua kila mwezi. Hivi hizo pesa ndogondogo zinasaidia nini kwa mtu aliyestaafu ambaye bado ana watoto wanaosoma na wanahitaji ada na mahitaji mengine?

Mtu amepambana na kulitumikia Taifa miaka 34 au zaidi, halafu leo anapewa Shilingi Milioni 29 kidogo kidogo kana kwamba wanatufanyia biashara na fedha zetu!

Hali hii inatufanya wastaafu wengi tuishi kwa shida na dhiki kubwa, na wengine wanajikuta wanakufa kwa mawazo na shinikizo la damu, au hata kujinyonga kwa sababu ya maisha magumu huku haki zao zikiwa zimeshikiliwa.

Tena ukitaka kujitokeza kuongea na kulalamika, unakabiliwa na vitisho au kufanyiwa mambo mabaya! Ndiyo maana askari wengi wadogo wanaumia na kulia kimya kimya lakini viongozi wetu wa juu (Askari) hawajali kwa sababu wao wana mifuko mikubwa.

Wito wangu na ombi letu kubwa kwa Serikali na uongozi wa Jeshi la Polisi na Jeshi la Magereza kote nchini (ikiwemo Mkoani Manyara na Tanzania nzima): Tulipeni stahiki zetu zote kwa mkupuo mmoja bila kutukata wala kutulipa kidogo kidogo!

Tulipeni pesa zetu zote tulizozifanyia kazi kwa jasho na uaminifu wetu ili tukazitumie kujikimu na kusomesha familia zetu.
Mbwa kala mbwa... Dhuluma, utapeli, rushwa, kubambika kesi watu.

KAZI Ina LAANA

Ndio mkome mkomae
 
Mobutu sseseko aliwaambia askari wake,,,,"mnalia mishahara midogo huku bunduki mnazo au hazina risasi" 😂😂😄😄
 
Safi sana ni kweli umeshindwa kujiandaa unatulilia sisi hatuna ata mamlaka japo katiba inatambua raia tuna mamlaka ila ya karatasi.
 
Back
Top Bottom