Askari wa barabarani kazi bado ngumu

Askari wa barabarani kazi bado ngumu

Hakuna anayejali

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2023
Posts
418
Reaction score
526
Elimu ya matumizi ya zebra na taa za kuongoza magari na waenda kea miguu bado haijawafika wananchi wengi hasa kwenye Manispaa mbalimbali, walau kwenye majiji watu wanaelewa.

Ongezeni jitihada ya elimu hii live in majority siyo mnatumia vyombo vya habari tu. Leo nimepita mahala taa ya kuzuia watu imewaka lakini mtembea kwa miguu anavuka, yaani bila busara ya dereva wa basi tungeongea mengine.

Watanzania wengi si tu hawajuwi matumizi ya zebra pia tuna uvivu wa kusoma.
 
Ugumu zaidi upo kwa boda boda waendesha pkpk ni janga kubwa sana .
 
Boda na bajaji wavunjasheria wakubwa.ukikusanya dereva boda na bajaji20 wanaoelewa mambo haya hata8hawafiki.
 
Ni kweli elimu inahitajika sana, kuna siku nilikuwa nakunywa kahawa pale Vigwaza Jamaa mmoja mjinga alikuwa badala ya kusema Zebra Cross au alama za Pundamilia yeye alikuwa akisema ni "alama za Magufuli kwa Wanyonge kuvukia balabala"

Nikamuambia hizo alama ziko tokea kitambo tokea Mkoloni,, akawaka sana na kuniambia mimi ni mtetezi wa Mabeberu.

Hii Nchi ina mamilioni ya Wajinga wapewe Darasa.
 
Elimu ya matumizi ya zebra na taa za kuongoza magari na waenda kea miguu bado haijawafika wananchi wengi hasa kwenye Manispaa mbalimbali, walau kwenye majiji watu wanaelewa.

Ongezeni jitihada ya elimu hii live in majority siyo mnatumia vyombo vya habari tu. Leo nimepita mahala taa ya kuzuia watu imewaka lakini mtembea kwa miguu anavuka, yaani bila busara ya dereva wa basi tungeongea mengine.

Watanzania wengi si tu hawajuwi matumizi ya zebra pia tuna uvivu wa kusoma.
Shida iliyopo ni kama usemavyo kuwa mamlaka zenye hilo jukumu zinatumia muda mwingi kujipambanua kwenye media badala ya kutumia media kutoa elimu kwa umma
 
Back
Top Bottom