Askari wa Israel wavua magwanda,wakimbia wakiacha wenzao waungue kwenye kifaru

Askari wa Israel wavua magwanda,wakimbia wakiacha wenzao waungue kwenye kifaru

Katika hali ya kuzimwa data na umeme Gaza kuna mengi tunayokosa kuyaona.Hata hivyo machache yanayovuja kwa shida inaonesha vita huko ni kali kuliko ule ukali uliotarajiwa na jeshi la IDF.
Mara kadhaa jeshi hilo limeshatangaza kuingia katikati ya Gaza lakini baadae ikaonesha kuwa bado wako pembeni kabisa wakitumia makombora ya kutoka kwenye ndege zao za kisasa.
Katika moja ya vidio zilizotolewa kwa shida na wapiganaji wa Hamas imeonesha kifaru cha Israel kikiripuka baada ya kupigwa na silaha hafifu.Baada ya hapo mmoja wa waendeshaji kifaru hicho akachomoka kwa nyuma huku akivua magwanda yake na kukimbia akiwaacha waenzake waungue ndani ya kifaru hicho.
Pembeni ya kifaru hicho vipo vyengine kadhaa vilivyotelekezwa baada ya ama kuharibiwa au askari wake kuamua kuviacha tu na kukimbia.
View attachment 2810206
Mtatengeneza picha za kila aina awamu hii ila mwisho wenu ndio huu🤣🤣🤣🤣
 
Israel kishashindwa hii vita toka siku ya kwanza, iliobakia anapambana na wagonjwa na watoto mahospitalini.

Sasa hivi yeye apigane na wagonjwa Gaza vijana wanamdunguwa kutokea nje.

Muisraeli Kaingizwa anapotakiwa awepo.
Umri wako haipendezwi na story za vijiweni.Watu wamejificha kwenye mahandaki kama panya wanapata wapi uwezo wa kudungua?Kinachowapa pumzi ni wale mateka wa israel tofauti na hapo wangeshapuliziwa sumu humo kwenye mashimo na kufutika.Magaidi lazima wafe hakuna namna nyingine.Vipi jana mliwakumbuka watu wa Sudan kwenye swala,au hao hawawahusu?
 
Urusi amepata hasara gani?wakati amechukua maeneo.

Hukuona namna alivyopoteza wanajeshi + tanks zake nyingi pamoja na magari ya kijeshi yaliyoingia ndani ya Ukraine na kulipuliwa...

Baadaye akaongeza nguvu ya wanamgambo wa Wagner ili kuweza pigana vita ya mtaani...
 
Elon musk kaongea Vizuri tu, Hamas ni Idea sio watu, mtoto alieuliwa baba yake Leo ndio Hamas wa Kesho, huwezi kupigana na idea kwa kuua watu.
Kwa hiyo ulitaka israel auliwe watu wake 1,400 akae asipigane kwa sababu hamas ni idea?Wacha kutu ile chuma mura
 
Kwa hiyo ulitaka israel auliwe watu wake 1,400 akae asipigane kwa sababu hamas ni idea?Wacha kutu ile chuma mura
Hesabu za Israel ni za kitapeli sana.Kila siku wanadurusu na kubadili namba.Sasa wanasema ni 1200 tu.Hata askari wao waliouliwa hawawezi kutoa namba halisi.
 
Bro umeandika ukionyesha upande gani ulipo. Nilishasema na leo nirudie hakuna vita rahisi. Hamas kwa sasa ni tofauti kabisa na.ile ya miaka kumi iliyopita.
Kwenye vita ngumu kama hii matukio kama hayo ya kushtukiza ni lazima yatokee. Kuhusu Israel hawajaingia Katikati ya Gaza ni uongo wapo katikati ya Gaza, natazama hapa sasa hivi kuna mapigano yanaendelea kuzunguka hosp ya Al shif.
Sasa jiulize Israel inapigana na wagonjwa? Madaktari na manesi? Bila shaka ni Hamas walioweka ngome kwenye hizo hospitali.
Kwenye hilo gate la hospitali hakuna mtu kutoka . Kuna mmoja alijaribu kutoka akiwa na mke na watoto wameuliwa wote.
Tazama Aljazira wako live.
Kumbuka aljazira iko based na Hamas.

Shida wanatumika video za uongo wakati, kiongozi wa Hamas Al Sinwar kajificha Al Shifa. Israel akiibeba hiyo Hospitali mapigano yataisha rasmi.
 
Kwa Sasa mmekimbilia kwenye video game. Show ipo Al Shifa Hamas imekataza watu wasitoke. Ukikimbia unalimwa Shaba. Ngoja tuone mwisho itakuwaje.
 
Wewe jamaa muongo unaleta video ya Syria miaka hiyo. Acheni uongo usio na maana show ipo Al Shifa. Baada ya hapo ndipo mazungumzo yataanza.
 
Kwa hiyo ulitaka israel auliwe watu wake 1,400 akae asipigane kwa sababu hamas ni idea?Wacha kutu ile chuma mura
Tatizo huangalii tatizo, kama ni movie umeanza katikati halafu unajudge.

Kwanini Hamas waue 1400? Hilo ndio swali ulitakiwa ujiulize.
 
Tutawaua tu ..no way
Wewe nani anakujuwa?,myahudi akiwaona nyie ndiyo anawatemea makohozi.

Bisha.
Wewe mwanamke ,huna huruma na watoto w kipalestina wanaosababisha kifo na hamas kwa ajili udini wako.
Jiulize hiyo hospitali ya Al shifa IDF inapigana na wagonjwa, au madkatari na wauguzi. Uwe na huruma na watoto wa wenzao.
Kwani kabla ya Hamas kupata upenyo watoto walikuwa hawauliwi?
 
Katika hali ya kuzimwa data na umeme Gaza kuna mengi tunayokosa kuyaona.Hata hivyo machache yanayovuja kwa shida inaonesha vita huko ni kali kuliko ule ukali uliotarajiwa na jeshi la IDF.
Mara kadhaa jeshi hilo limeshatangaza kuingia katikati ya Gaza lakini baadae ikaonesha kuwa bado wako pembeni kabisa wakitumia makombora ya kutoka kwenye ndege zao za kisasa.
Katika moja ya vidio zilizotolewa kwa shida na wapiganaji wa Hamas imeonesha kifaru cha Israel kikiripuka baada ya kupigwa na silaha hafifu.Baada ya hapo mmoja wa waendeshaji kifaru hicho akachomoka kwa nyuma huku akivua magwanda yake na kukimbia akiwaacha waenzake waungue ndani ya kifaru hicho.
Pembeni ya kifaru hicho vipo vyengine kadhaa vilivyotelekezwa baada ya ama kuharibiwa au askari wake kuamua kuviacha tu na kukimbia.
View attachment 2810206
Lkn HAMAS lazima wachapwe tu
 
huyu jamaa wa ajabu sana, anashangaa askari kukimbia huku akivua nguo, hajui kama akibaki na nguo atateketea kwa moto. ulitaka abaki mlemle aungue? au arudi kumwokea mwenzake ambaye anajua hawezi kufanikiwa kumwokoa, na yeye si atakufa na wakati huohuo adui yupo kwenye range ampige risasi? sema israel nao hao vijana wameenda huko ni wadogo, wapo kwenye 20s, wapo vitani wanafikiria magirlfriend wao wamewaacha uraiani pengine. jeshi lao wengi ni vijana wadogo jambo ambalo pia ni zuri kwasababu ni hazina kwa taifa. na wengine wameitwa tu toka mataifa mbalimbali kwasababu wayahudi wote duniani lazima huwa wana kipindi wanaenda kutumikia jeshini israel na kurudi nchini kwao, wengine hawapo vizuri ndio maana tunasema kama isingekuwa zana za kisasa, israel wangesumbuka zaidi ya hapo kwa hamas.
Mtatafta kila sababu
 
Back
Top Bottom