Askari wa JWTZ Atuhumiwa Kwa Mauaji ya Mke Wake wa Ndoa Huku Akijaribu Yeye Mwenyewe Kujiua Bila Mafanikio

Askari wa JWTZ Atuhumiwa Kwa Mauaji ya Mke Wake wa Ndoa Huku Akijaribu Yeye Mwenyewe Kujiua Bila Mafanikio

Sifanyi huo ufala. Yule balozi wa china si analipwa. Mimi nikigundua mke wangu ananisaliti na mtu mwenye pesa na huyo mwenye pesa akanipatia pesa wakati anamtumia, kiroho safi nachukua mpunga nafanya mambo yangu.....


Sasa mimi hiyo takataka ya kazi gani napokea mpunga tu safi maisha yaendelee
Wewe jamaa weee😆
 
Mkuu achana na hilo Bumunda (Pumbavu) kwani linadhani hadi Mwanaume kufikia Kuchukua hatua hiyo hakuvumilia na hajaumizwa vya Kutosha.

Cc: Mmassy JM
Mbona wewe hukumuua 'mgoni wako' ulipochapiwa mama watoto wako?

Ungemuua then ukawe mke wa nyapala segerea uhitimishe uvumilivu wako.
 
Sasa ukishaua unapata faida gani ya kudumu?
Bwana Mmasy, wengi wa wauaji wa case kama hizi huwa hawaui kwa kupanga.

Inakuwa jambo la hamaki kutokana na maudhi ya upande wa pili.

Wanaokuwa na muda wa kutafakari hasara na faida huwa hawaui...na hao tuko wengi.
 
Wewe jamaa weee[emoji38]
Kabisa yaani. Ukiendekeza hisia na mwanamke malaya utachanganyikiwa. Mwanamke wa kumheshimu ni yule anaekuheshimu na kukulindia heshima yako wewe tu..... Hawa wengine chezea unavyoweza maana wameamua kuwa takataka watreat kama takataka.
 
Askari huyo wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) anayeenda kwa jina la Daniel Warioba alijaribu kujiua kwa kunywa sumu baada ya tukio hilo lakini hakufanikiwa.

Uchunguzi wa tukio hilo la kutisha lililotokea Mlandizi Mkoani Pwani bado unaendelea na taarifa kamili itatolewa na mamlaka husika ambayo ni Jeshi la Polisi

Inadaiwa Kuwa chanzo cha tukio la kikatili ni mfarakano uliochangiwa pamoja na mambo mengine wivu wa kimapenzi baina ya wanandoa hao

Mtuhumiwa huyo kwa Sasa anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano zaidi ya tukio hilo.

Tunatoa pole kwa familia ya Mwendazake aliyehudumu kama Mwalimu Katika uhai wake

=====

Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linamshikilia Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Koplo Daniel Warioba (43) kutoka Kikosi cha 92 TJ kwa tuhuma za kumuua Mke wake Joyce Ismail (35) ambaye ni Mwalimu wa Shule ya Msingi Ruvu Darajani

Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa, aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia jana huu katika eneo la Janga, Wilaya ya Kipolisi Mlandizi.

Kamanda Wankyo alisema askari huyo anadaiwa kumchoma mke wake na kitu chenye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili na kumsababishia kifo.

Kwa mujibu wa Kamanda Wankyo, baada ya kutekeleza mauaji hayo, mtuhumiwa anadaiwa alitaka kunywa sumu kwa lengo la kujiua.

Wankyo alisema polisi wamemkamata mtuhumiwa huyo na anaendelea kupata matibabu katika Hospitali ya Rufani ya Mkoa ya Tumbi, huku chanzo cha tukio hilo kikiendelea kuchunguzwa.
BODA -BODA wanakula sana wake za watu, hili suala halita ishia hapa, yaaniwanawake wanagongwa kwa kupewa lift za bodaboda, sasa maskini huyu mwalimu ili awahi lazma apande boda, jamaa anamgusa gusa akilainika anazama anatoka, anazama anatoka.
 
Bwana Mmasy, wengi wa wauaji wa case kama hizi huwa hawaui kwa kupanga.

Inakuwa jambo la hamaki kutokana na maudhi ya upande wa pili.

Wanaokuwa na muda wa kutafakari hasara na faida huwa hawaui...na hao tuko wengi.
sure, sisi majaji tunasema caught flagrento delicto with no time to heat of passion,
 
Jinga kabisa shida ya askari wenye namba ndongo JNSO ubabe wa kingese
 
Kabla sijakujibu hilo swali hebu nijiridhishe na upeo wako juu ya haya maswala ya usaliti katika mahusiano.

Umeshawahi kuwa na mke unamhudumia kwa upendo na haumletei ujinga halafu unakuja kujua wazi wazi kuwa anamahusiano na mtu nje unamkamata na ushahidi badala ya kujali hisia zako anabakia kusema wewe unakuwa busy hauna muda nae ndio maana kajikuta anafanya hayo mambo.

Umeshawahi kukutana na hiyo hali wewe kama wewe usinambie story za mtu mwingine?!

Jibu swali langu
 
Haya mambo kama hujawahi pitia utaongea kirahisi sanaa ilaa inauma sanaa mwanamke kusaliti hata kama mwanaume una mademu kadhaa wa siri ilaa sio mke wako uliyemuoa akucheat. Kiufupi inahitaji moyo wa kijasiri kulipokea hilo. Wanawake mlioolewa tulieni katika ndoa na ukitaka kubadil ladha basi kuwa makini

Sent from my TECNO CF7 using JamiiForums mobile app
Dawa ni kuwakomesha nyie si hamtulii kabisa na ndoa zenu
 
Back
Top Bottom