Askari wa TANAPA 3, Askari wa TFS 6 pamoja na migambo 4 mbaroni kwa tuhuma za mauaji ya watu 4 Kagera

Askari wa TANAPA 3, Askari wa TFS 6 pamoja na migambo 4 mbaroni kwa tuhuma za mauaji ya watu 4 Kagera

Mawele

Platinum Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
1,161
Reaction score
4,251
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kagera linawashikilia askari wa Wanyama pori (TANAPA) watatu, askari wa Maliasili ( TFS) sita na askari Mgambo wanne kwa tuhuma za mauaji ya watu wanne (04) yaliyotokea huko katika kijiji cha Kanyamika kata ya Karambi Tarafa ya Kimwani Wilaya ya Muleba Mkoa wa Kagera.

Tukio hilo limetokea Oktoba 17, 2026 majira 10:00 hrs huko katika maeneo ya Kanyamika barabara kuu ya Muleba kwenda Biharamulo, kijiji cha Kanyamika Kata ya Karambi ambapo askari hao walikuwa doria katika pori la hifadhi ya Misitu ya Ruiga wakiwa na gari lenye namba za usajili 02 JU 354 aina ya Toyota Landcruiser likiendeshwa na dereva askari wa Wanyama pori TNP. SRIII 3585 Mituni Haji, (26) akiwa na wenzake 1. TNP.4081 SRIII Faustin William Mboko, (25), 2. TNP.1686 SGT. Kingmar Mewama, (40), 3. WSR 7869 A Fluomena Romani France, (28), 4. TNP. CRIII Erick David Muya, (25), 5. TNP. SRIII Yusuph Idd Kweya, (26).

Wengine ni TNP. CRIII Emmanuel Sheki Zabron, (25), 7. TNP. CRII Yusto David, (22), 8. BKP Josiah Msafiri Mahenge, (26), 9. MG. 621987 Farouk Bashiru Mahamudu, (24), 10. MG. 659921 Baraka Sadoki Kabulo (28), 11. MG. 660012 Regan Bwemelo Nikodem, (24), 12. MG.65989 Alanus Beyanga Chowe (35) na 13. Andrew Charles Kwiyega (32) dereva wa TFS, wakiwa na silaha aina ya AK 47 tatu waliwashambulia watu waliokuwa wamebeba mkaa kwenye pikipiki zipatazo kumi baada ya watu hao kukataa kukamatwa na kujaribu kuwanyang'anya silaha askari hao ambao walikuwa doria katika maeneo hayo na kusababisha kutokea vifo vya watu watatu 04 ambao ni Osward Yuster (38), mkazi wa Ngote, Pius Charles (40), mkazi wa Magata na Charles Michael (35), mkazi wa Ngote na Edgar Elias Lukangula (44), mkazi wa Butembo ambaye amefariki dunia akiwa anapatiwa matibabu katika hospitali ya Rufaa mkoa wa Kagera Oktoba 18, 2026 majira ya alfajiri.

Aidha, katika tukio hilo kulitokea vurugu zilizofanywa na wabeba mkaa hao na kusababisha uharibifu wa gari la Serikali mali ya wakala wa Misitu (TFS) lenye namba za usajili 02 JU 0354 aina ya Toyota Landcruiser ambalo limeharibiwa kioo cha mbele na vya pembeni kwenye milango. Kufuatia tukio Jeshi la Polisi limekamata Pikipiki 10, mkaa magunia 22, Mapanga 05, Kofia ngumu 02, Makoti mawili, Silaha aina ya AK 47 tatu, Maganda ya risasi za AK 47 matano pamoja na gari moja aina ya Toyota Landcruiser lenye namba za usajili 02 JU 0354 mali ya Wakala wa Misitu (TFS),

Jeshi la Polisi mkoa wa Kagera limeshachukua hatua kuhusiana na tukio hilo ikiwa ni pamoja na kuwakamata watuhumiwa wote kwa ajili ya uchunguzi wa tukio hilo.

Jeshi la Polisi mkoa wa Kagera linaendelea kutoa wito kwa wananchi wote kutii sheria bila shuruti na kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi pale wanapokutana na askari au mamlaka iliyopewa dhamana ya kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria za nchi.

Screenshot 2026-10-19 at 10-32-20 Instagram.png

1792395403299.png
 
Jeshi la Polisi mkoani Kagera linawashikilia askari watatu wa Wanyamapori (TANAPA), askari wa Maliasili sita na askari mgambo wanne kwa tuhuma za mauaji ya watu wanne yaliyotokea katika Kijiji cha Kanyamika Kata ya Karambi Wilaya ya Muleba mkoani humo Oktoba 17, 2026.

Polisi wamesema askari wakati wakiwa katika doria katika pori la hifadhi ya misitu ya Ruiga wakiwa na silaha aina ya AK 47 tatu, waliwashambulia watu waliokuwa wamebeba mkaa kwenye pikipiki zipatazo 10 baada ya watu hao kukataa kukamatwa na kujaribu kuwanyang'anya silaha askari.
 
HILI SWALA LA ASKARI KUMKAMATA ASKARI MWENZIE SIONI KAMA LINA UWAJIBIKAJI KABISA...YAANI SIMBA UKAMUWEKE KWENYE ZIZI LA SIMBA KWA KOSA LA KUMLA NYATI UTEGEMEE SIMBA ATATAFUNWA NA SIMBA...HAPA KATIBA MPYA INAUMUHIMU...TUNATAKA MREKESHO WA HILI SWALA.
 
Danganya toto hizo, toka lin askari kukamata askari wenzao!

Kwanza taarifa yenyewe inawatuhumu marehem et "walikataa kukamatwa na wakataka kuwanyang'anya silaha polisi"

Halaf tunaambiwa et gari limeharibiwa viba (et vimepasuliwa vioo)!

Mbona hakuna askar alikufa wala kujeruhiwa kama kulikuwa na mapambano?

Ifike wakat watanzania tuamke usingzin!
 
Kwahiyo nan alikuarifu Askari lazima afe?

Kuna sehemu raia tunachanganya vitu,huwezi kutaka kufanya vurugu halafu uachiwe haipo hata nyumbani kwako mtoto akileta makuzi lazima umuonyeshe mipaka
 
Nimeanza kupata ukakasi pale tu wabeba mkaa walipotaka kuwanyang'anya askali siraha nikajua,hualibifu wa gari nikajua tayar utetez umeanza
 
Au baada ya kuona wamefanya waliyo yafanya ikabidi wavipasue wenyewe kuficha ushahidi
 
HILI SWALA LA ASKARI KUMKAMATA ASKARI MWENZIE SIONI KAMA LINA UWAJIBIKAJI KABISA...YAANI SIMBA UKAMUWEKE KWENYE ZIZI LA SIMBA KWA KOSA LA KUMLA NYATI UTEGEMEE SIMBA ATATAFUNWA NA SIMBA...HAPA KATIBA MPYA INAUMUHIMU...TUNATAKA MREKESHO WA HILI SWALA.
Kwenye hiyo katiba mpya askari alifanya jinai atakamatwa na nani?
 
Kwenye hiyo katiba mpya askari alifanya jinai atakamatwa na nani?
kuna chombo maalumu ambacho kitaundwa kwa ajili ya kushulika na askari kwasababu tumeona udhaifu wa KATIBA hii askari wanalindana we huwezi kupeka kesi ya ngedere kwa ngedere halafu utarajie matokeo lazima pawepo na uwanja mpana wa uwazi. Sorry haya ni maoni usije ukaniteka..Kwenye habari hapo juu nani anathibitisha hao watu wa mkaa waliwashambulia askari?Je, askari anachunguzwa na nani?.Refa ni nani?.
 
Back
Top Bottom