Taarifa za kukamatwa kwa mwenyekiti wa Chadema Tundu Lissu jana usiku ni ishara kuwa sasa CCM imeingiwa na hofu kubwa kwa jinsi uongozi mpya wa Chadema unavyoungwa mkono katika hoja yao ya No Reform No Election. Taarifa mpya ya mchana huu ya kukamatwa kwa Makamu Mwenyekiti wa Chadema ni dhahiri kuwa kuwa CCM imezidiwa na hoja za chama hiki hivyo kuamua kulitumia Jeshi la Polisi kuwakamata viongozi wake wakuu na kuwaweka kizuizini kwa muda usiojulika hivyo kutengeneza ombwe la uongozi katika chama hicho.
Ni dhahirii sasa CCM imeamua kutumia mabavu ya vyombo vya dola kuondoa uongozi uliochaguliwa kidemokrasia na kutengeneza njia ya kumrudisha mtu wao ambaye wana agano naye la kupoozesha magaeuzi ili aongoze tena Chadema. Mbinu hii chafu amabyo CCM inaamini itawasaidia kupunguza moto wa No Reform No Election ndiyo kwanza inathibitisha kuwa ni kweli CCM inatumia bunduki na mabomu ya polisi kujibu hoja za kisiasa .