PreGE2025 Askari watawanya Watu mkutano wa CHADEMA Songea, mabomu ya machozi yarushwa, Polisi wawabeba Heche na Lema

PreGE2025 Askari watawanya Watu mkutano wa CHADEMA Songea, mabomu ya machozi yarushwa, Polisi wawabeba Heche na Lema

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Makamu Mwenyekiti na viongozi wengine wa CHADEMA wapo Kituo cha Polisi Songea baada ya Jeshi hilo kupeleka wito wa kuhitajika kituoni hapo.

Nini sababu ya Kuitwa Mchana huu?

Je, Watachomoka salama?
View attachment 3298911
Jioni ya leo Heche alikuwa afanye Mkutano wa hadhara Songea Mjini.
Miye sikuamini sana slogan ya No reform No election, ina impact kiasi hiki !!!!!
 
Huko ndiko anatoka katibu mkuu wa Chama Dola mnategemea nini,hayo ndio majibu.Halafu wanaotenda hayo utawakuta ibadani na wanawekwa nafasi za mbele.Uovu ni uovu tu haijalishi jina la mtendaji hapo Emanuel amezingua
 
Hizi jitihada zingekuwa zinaelekezwa kwenye maendeleo na kukamata wezi serikalini mbona hata Dubai wangesubiri....hahaha..
Kila CAG akija wizi tu lakini wanashangaana tu..
 
Kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania na sheria za nchi, uchaguzi ni msingi wa demokrasia na haki ya kikatiba (Kwa mfano, Katiba ya Tanzania ya 1977, Kifungu cha 5 na 21).

Kutoa vitisho vya "kuharibu uchaguzi" au kuanzisha "uasi" ni uvunjifu wa sheria za Tanzania, kama vile:
(1) Kanuni ya Jinai (Penal Code): Vifungu namba 38 (kuchochea fujo- sedition), 40 (kuchochea machafuko-inciting unrest), au 41 (kuashiria kusudi la kuvunja utulivu wa umma-conspiracies to breach public peace) vinaweza kutumika kuwashitaki wanaotangaza mambo hayo.

(2) Sheria za Usalama wa Taifa: Kuchochea uasi kunaweza kuchukuliwa kama udhalilishaji wa mamlaka ya Serikali, na kusababisha kukamatwa, mashtaka, na hukumu ya jela ikiwa wata patikana na hatia.

(3) Msajili wa Vyama vya Siasa, Kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa (Namba 5 ya 1992), ana wajibu wa kuhakikisha vyama vinazingatia Katiba na sheria za nchi. Ikiwa chama au wanachama wake kinatangaza mambo yanayokiuka Katiba (kama vile kukataa uchaguzi kwa njia za vurugu), Msajili anaweza:
  • Kutoa onyo la kisheria
  • Kufuta chama kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa, Kifungu cha 11(2)(e), ikiwa kinaendelea kukiuka masharti ya kikatiba.
Hiyo katiba inafuatwa Kwa Wapinzani pekee. Yule bumunda Dalali wa Mpox mmemfanya nini?
 
Mwasifiga unatuletea Katiba ya TANU ambayo Mama yenu anaiita kakitabu Non functional n useless letters..... Waifuate wao Kwanza ndio sisi tufuate
 
Taarifa za kukamatwa kwa mwenyekiti wa Chadema Tundu Lissu jana usiku ni ishara kuwa sasa CCM imeingiwa na hofu kubwa kwa jinsi uongozi mpya wa Chadema unavyoungwa mkono katika hoja yao ya No Reform No Election. Taarifa mpya ya mchana huu ya kukamatwa kwa Makamu Mwenyekiti wa Chadema ni dhahiri kuwa kuwa CCM imezidiwa na hoja za chama hiki hivyo kuamua kulitumia Jeshi la Polisi kuwakamata viongozi wake wakuu na kuwaweka kizuizini kwa muda usiojulika hivyo kutengeneza ombwe la uongozi katika chama hicho.

Ni dhahirii sasa CCM imeamua kutumia mabavu ya vyombo vya dola kuondoa uongozi uliochaguliwa kidemokrasia na kutengeneza njia ya kumrudisha mtu wao ambaye wana agano naye la kupoozesha magaeuzi ili aongoze tena Chadema. Mbinu hii chafu amabyo CCM inaamini itawasaidia kupunguza moto wa No Reform No Election ndiyo kwanza inathibitisha kuwa ni kweli CCM inatumia bunduki na mabomu ya polisi kujibu hoja za kisiasa .
 
Sio muda mrefu Mbowe ataibuka kutoka mapumzikoni and save the day.

Ni lazima umuhimu wake uonekane katika chama.
 
Back
Top Bottom