Ok Unataka Tufanye Battle Kisheria?
Come on!
Tuanze na wanaosema Kuhusu NRNE wana haki ya Maoni na Uhuru wa Kujieleza kama Katiba Ibara ya 18 inavyowataka..
Nitasema tena kauli ya “No Reform, No Election” ni maoni ya kisiasa, si uasi. Ni haki ya msingi ya kikatiba kutoa msimamo wa kisera. Haki hii haiwezi kuzimwa kwa kisingizio cha “uasi” pasipo ushahidi wa fujo au uhalifu.
Sijui kama Unaifahamu Sera ya Uwazi, Uwajibikaji na Demokrasia ,Azimio la Arusha na Miongozo ya SADC
SADC Principles and Guidelines Governing Democratic Elections zinataka chaguzi ziwe:
- Huru na haki
- Zinazoshirikisha vyama vyote
- Zisizo na ukandamizaji wa kisiasa
Kudai reform kabla ya uchaguzi ni kuunga mkono miongozo ya kimataifa inayolenga kuweka mazingira sawa kwa vyama vyote. Kauli ya "No Reform, No Election" inatetea misingi hii, si kuivuruga.
Naomba Nikukumbushe Kwamba Kuzuia au Kususia Uchaguzi si Uhalifu wa Kisheria
Sheria za Tanzania hazimlazimishi mtu au chama kushiriki uchaguzi. ila Kususia uchaguzi ni mbinu ya kisiasa inayotambulika kimataifa kama aina ya “civil resistance” au “non-violent protest”.
CHADEMA au mtu binafsi anaposema hatashiriki uchaguzi bila marekebisho, siyo kosa. Ni haki ya kisiasa ya kutojihusisha na mchakato anaouona si wa haki.
Hakuna Tamko la Vurugu wala Uasi Lililotolewa
Kauli ya “No Reform, No Election” haijawahi kusema tutazuia uchaguzi kwa nguvu au Tutatumia Mitutu au tutafanya fujo.
Hivyo, sheria za Penal Code kifungu cha 38, 40, 41 hazihusiki bila ushahidi wa vitendo vya vurugu
Msajili wa Vyama vya Siasa Hafai Kuwabana kwa Maoni Halali
Kifungu cha 11(2)(e) cha Sheria ya Vyama vya Siasa hakipaswi kutumiwa kuadhibu chama kwa kutoa msimamo wa kisiasa.
Msajili anatakiwa kuweka mazingira ya vyama kushiriki siasa kwa uhuru, sio kuwatisha..
Narudia tena kauli ya “No Reform, No Election” haina kosa kisheria, bali ni matumizi halali ya haki ya kikatiba, kisiasa na kijamii.
Kauli ya “No Reform, No Election” haijasema: "Tutapiga kura kwa nguvu," "Tutavuruga uchaguzi," au "Tutavamia vituo vya kupigia kura."
Ni tamko la kisiasa linalosema wazi kuwa, bila mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi, hatutashiriki uchaguzi.
Hakuna kifungu katika Katiba wala sheria inayomlazimisha mtu binafsi au chama kushiriki uchaguzi bila ridhaa.
Katika demokrasia, kuna haki ya kushiriki na pia haki ya kutoshiriki, hasa kama mazingira siyo shirikishi.
Kauli kama "No Reform, No Election" ni tamko la uwajibikaji wa kiraia (civic responsibility).
Raia au chama kinapobaini kuwa uchaguzi hauko sawa, kinapozuia kushiriki bila reform, kinatekeleza wajibu wake wa kuhimiza mabadiliko.
Kauli ya “No Reform, No Election” inatekeleza miongozo hii ya SADC ya Uchaguzi ya mwaka 2004 kwa kudai:
- Uhuru wa vyombo vya uchaguzi
- Usawa kwa vyama vyote
- Ulinzi wa kura na wapiga kura
Sera ya vyama vya upinzani kulalamikia tume ya uchaguzi, mfumo wa uchaguzi, au mazingira ya kisiasa siyo kosa.
Huo ni msingi wa mabadiliko katika nchi nyingi, hata zilizopata mafanikio ya kidemokrasia.
Mfano hai:
- Afrika Kusini (1990s): ANC iligomea kushiriki uchaguzi bila mabadiliko ya mfumo wa kibaguzi.
- Kenya (2007): ODM na mashirika ya kiraia walikataa kushiriki uchaguzi bila tume huru..
Hizo penal code ni sheria za zamani za kikoloni, na matumizi yake lazima yazingatie mazingira halisi.
Kutoa maoni ya kisiasa au kususia uchaguzi kwa amani hakuwezi kufasiriwa kama uchochezi bila matendo ya vurugu au uasi.
Mahakama ya Afrika Mashariki (EACJ) imewahi kusema kuwa:
"Sedition must be proven through incitement to violence, not by disagreement with government policy."