PreGE2025 Askari watawanya Watu mkutano wa CHADEMA Songea, mabomu ya machozi yarushwa, Polisi wawabeba Heche na Lema

PreGE2025 Askari watawanya Watu mkutano wa CHADEMA Songea, mabomu ya machozi yarushwa, Polisi wawabeba Heche na Lema

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
No reforms no election imeleta balaa. Wakati huu Watanzania ndio tulipaswa kuonyesha nguvu ya umma, viongozi waliokamatwa ni katika harakati za reforms tunazozitaka.

Huu ukamataji hovyo lazima ukome.
Jitokeze na wewe upate mkong'oto.Unajificha nyuma ya Keyboard.
 
Ok Unataka Tufanye Battle Kisheria?
Come on!
Tuanze na wanaosema Kuhusu NRNE wana haki ya Maoni na Uhuru wa Kujieleza kama Katiba Ibara ya 18 inavyowataka..

Nitasema tena kauli ya “No Reform, No Election” ni maoni ya kisiasa, si uasi. Ni haki ya msingi ya kikatiba kutoa msimamo wa kisera. Haki hii haiwezi kuzimwa kwa kisingizio cha “uasi” pasipo ushahidi wa fujo au uhalifu.

Sijui kama Unaifahamu Sera ya Uwazi, Uwajibikaji na Demokrasia ,Azimio la Arusha na Miongozo ya SADC

SADC Principles and Guidelines Governing Democratic Elections zinataka chaguzi ziwe:
  • Huru na haki
  • Zinazoshirikisha vyama vyote
  • Zisizo na ukandamizaji wa kisiasa
Kudai reform kabla ya uchaguzi ni kuunga mkono miongozo ya kimataifa inayolenga kuweka mazingira sawa kwa vyama vyote. Kauli ya "No Reform, No Election" inatetea misingi hii, si kuivuruga.

Naomba Nikukumbushe Kwamba Kuzuia au Kususia Uchaguzi si Uhalifu wa Kisheria

Sheria za Tanzania hazimlazimishi mtu au chama kushiriki uchaguzi. ila Kususia uchaguzi ni mbinu ya kisiasa inayotambulika kimataifa kama aina ya “civil resistance” au “non-violent protest”.

CHADEMA au mtu binafsi anaposema hatashiriki uchaguzi bila marekebisho, siyo kosa. Ni haki ya kisiasa ya kutojihusisha na mchakato anaouona si wa haki.

Hakuna Tamko la Vurugu wala Uasi Lililotolewa

Kauli ya “No Reform, No Election” haijawahi kusema tutazuia uchaguzi kwa nguvu au Tutatumia Mitutu au tutafanya fujo.

Hivyo, sheria za Penal Code kifungu cha 38, 40, 41 hazihusiki bila ushahidi wa vitendo vya vurugu

Msajili wa Vyama vya Siasa Hafai Kuwabana kwa Maoni Halali

Kifungu cha 11(2)(e) cha Sheria ya Vyama vya Siasa hakipaswi kutumiwa kuadhibu chama kwa kutoa msimamo wa kisiasa.

Msajili anatakiwa kuweka mazingira ya vyama kushiriki siasa kwa uhuru, sio kuwatisha..

Narudia tena kauli ya “No Reform, No Election” haina kosa kisheria, bali ni matumizi halali ya haki ya kikatiba, kisiasa na kijamii.

Kauli ya “No Reform, No Election” haijasema: "Tutapiga kura kwa nguvu," "Tutavuruga uchaguzi," au "Tutavamia vituo vya kupigia kura."

Ni tamko la kisiasa linalosema wazi kuwa, bila mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi, hatutashiriki uchaguzi.

Hakuna kifungu katika Katiba wala sheria inayomlazimisha mtu binafsi au chama kushiriki uchaguzi bila ridhaa.

Katika demokrasia, kuna haki ya kushiriki na pia haki ya kutoshiriki, hasa kama mazingira siyo shirikishi.

Kauli kama "No Reform, No Election" ni tamko la uwajibikaji wa kiraia (civic responsibility).

Raia au chama kinapobaini kuwa uchaguzi hauko sawa, kinapozuia kushiriki bila reform, kinatekeleza wajibu wake wa kuhimiza mabadiliko.

Kauli ya “No Reform, No Election” inatekeleza miongozo hii ya SADC ya Uchaguzi ya mwaka 2004 kwa kudai:
  • Uhuru wa vyombo vya uchaguzi
  • Usawa kwa vyama vyote
  • Ulinzi wa kura na wapiga kura
Sera ya vyama vya upinzani kulalamikia tume ya uchaguzi, mfumo wa uchaguzi, au mazingira ya kisiasa siyo kosa.

Huo ni msingi wa mabadiliko katika nchi nyingi, hata zilizopata mafanikio ya kidemokrasia.

Mfano hai:
  • Afrika Kusini (1990s): ANC iligomea kushiriki uchaguzi bila mabadiliko ya mfumo wa kibaguzi.
  • Kenya (2007): ODM na mashirika ya kiraia walikataa kushiriki uchaguzi bila tume huru..
Hizo penal code ni sheria za zamani za kikoloni, na matumizi yake lazima yazingatie mazingira halisi.

Kutoa maoni ya kisiasa au kususia uchaguzi kwa amani hakuwezi kufasiriwa kama uchochezi bila matendo ya vurugu au uasi.

Mahakama ya Afrika Mashariki (EACJ) imewahi kusema kuwa:
"Sedition must be proven through incitement to violence, not by disagreement with government policy."
Hivi Kenya Ruto anaweza kumkamata Odinga mkutanoni akafanikiwa?
 
Acha kelele, akili za wafuasi wa Lissu ni sawa sawa na za ng'ombe tu.
Unatia huruma yaan kanga , vitenge , kofia na elf 20 zinazoporwa kutoka kweny pesa za maendeleo ndo zinakufanya ujitoe akili na kusahau kituo chako cha afya hakina maji safi , huduma bora mpk utoe hongo , umeme unakatika , hakuna constistence ya stock ya dawa muhimu , huna bararabara ya mtaa huna guarantee ya usalama hapo kweny makaz yako ( kituo kipo 10km kutoka ulipo na hata doria hakuma )

Ila ww unaona haya yote sawa tu

Unakenua wakila hela ila wanaowaamsha watz unawaona wabaya

Hv ukiunganisa nguv kutokomeza utawala mbovu , unahis atanufaika Lissu na Heche tu ? Hv hao ndo wanatumia barabara pekee yao ? Umeme pia ? Usalama pia usafi pia , na huduma za kiafya ?

WEWE UMEKATA TAMAA KBS YAAN DUNIANI KWAKO UNAMALIZIQ UHAI TU NA HUNA MPANGO WOWOTE ULE
 
Anza kujitokeza wewe,ule mkong'oto,uko nyuma ya keyboard jitokeze utiwe akili.
endeleeni kuongeza kuni.......; Congo tutafanana nao muda si mrefu, hakuna kujitokeza kiboya boya... nyie fanyeni yenu na wanyonge watajua la kufanya; tusilaumiane mbeleni
 
WATANDIKWE TU, NCHI IMETULIA WANATAKA KUTULETEA UJINGA.
LISU MWENYEWE DIKTETA HATA TUKIMPA NCHI ATAENDELEZA YALE YA MWENDAZAKE.
MAMA YETU SAMIA USIRUHUSU UJINGA HUU WA LISU KUSEMA ATAASI, ASHUGHULIKIWE IPASAVYO
Huna marinda wewe *****
 
WATANDIKWE TU, NCHI IMETULIA WANATAKA KUTULETEA UJINGA.
LISU MWENYEWE DIKTETA HATA TUKIMPA NCHI ATAENDELEZA YALE YA MWENDAZAKE.
MAMA YETU SAMIA USIRUHUSU UJINGA HUU WA LISU KUSEMA ATAASI, ASHUGHULIKIWE IPASAVYO
20250410_122039.jpg
 
well done vyombo vya ulinzi na usalama Songea:KasugaYeah:
ni muhimu sana magenge ya kihalifu yanayojificha nyuma ya kufanya mikutano ya kisiasa kote nchini, yakasamabaratishwa mapema iwezekanvyo bila huruma, kabla hayajaleta uharibifu na madhara kwa wananchi :NoGodNo:
Magenge gani ya wahalifu sasa hapo? Hahaha 😂 😂 😂 watekaji mmeshndwa kuwakomesha
 
Mpigwe tu mpaka akili ziwakae sawa. Maana haiwezekani mnatoa maneno ya kichochezi tu kila siku
. Mpigwe vizuri mpaka mbubujikwe na machozi.
Kuna maneno ya kichochezi kama wanayotoa ccm dhidi ya wapinzani au wao wanahatimiliki ya nchi?
 
Vurugu wanazofanya Polisi kwa Chadema jana na leo ni blessings in disguise,wanapaisha hoja ya wapinzani juu ya matumizi ya polisi wenye silaha za moto kudhibiti wanasiasa wenye ushawishi. Asanteni sana polisiccm kwa kuwa mabalozi wa kuelezea dunia udhalimu wa serikali ya CCM.
 
jikite kwenye hoja bila kuwaza uchafu gentleman :NoGodNo:
We fanya kazi yako maalum, ila stage hi ikishindikana, kifuatacho tunaenda kuwa kama Congo. Chadema mnayoionea haina ubavu huo wacha inyanyaswe. Subiri mziki kama wa m23 utaanza ki aina yake. wambie maboss zako inakuja .....
 
Mpaka aliitwa mhaini anataka kumpindua Mfalme
Yaan,
Binafsi hata Nyerere aliwai kusema hatamani kujenga taifa la watu waoga waoga.

Binafsi nimemsikia mwabukusi ni mkomavu Sana wa siasa.. issue UCHAGUZI ufanyike na CCM waache uhuni mtu akishinda atangazwe pia uhuni wa ku LIG ELECTIONS waache kabisa.

Kuengua wapinzani kwenye majimbo, wizi wa kura, utaratibu mbovu wa kuwaapisha mawakala wa upinzani uachwe Mara moja, uhuni wa kupiga mabomu watu.
 
WATANDIKWE TU, NCHI IMETULIA WANATAKA KUTULETEA UJINGA.
LISU MWENYEWE DIKTETA HATA TUKIMPA NCHI ATAENDELEZA YALE YA MWENDAZAKE.
MAMA YETU SAMIA USIRUHUSU UJINGA HUU WA LISU KUSEMA ATAASI, ASHUGHULIKIWE IPASAVYO
kama unalipwa mshahara na serekali, utajiona uko sawa maana unaishi ili ule uende chooni ufe mtot ako kama unae usikute ndo wale hawana mtoto na hawataki na basi kama unae huyo mtoto ako ataendelea kuwa mtumwa wa nchi inailyoiba kura na kunyanyasa kisa mama ake au baba ake amekaa kula mshahara na kuunya chooni huo mshara bila kuuliza kwanini walitoa wamasaai Ngorongoro na kwanini tunadaiwa Trillion 97 na Maisha ya wananchi wengi ni duni..Mwish wa siku unauza utu wako sababu mshahara kwako ndio Msingi wa maisha yako
WATANDIKWE TU, NCHI IMETULIA WANATAKA KUTULETEA UJINGA.
LISU MWENYEWE DIKTETA HATA TUKIMPA NCHI ATAENDELEZA YALE YA MWENDAZAKE.
MAMA YETU SAMIA USIRUHUSU UJINGA HUU WA LISU KUSEMA ATAASI, ASHUGHULIKIWE IPASAVYO
 
Back
Top Bottom