Askari wauawa Dodoma wakati wakienda kumkamata mtuhumiwa wa uhalifu.

Kifo ni kifo tu.

Moja ya statement za hivyo kabisa kutokea. Athari zake ndio hizi sasa.

By the way, sifa moja kubwa ya Tanzania ni ushirikiano wa dhati kati ya wananchi na wana usalama kwenye mambo ya ulinzi na kuzuia uhalifu.

Hii inayoendelea sasa nani ameitengeneza na ni kwa manufaa ya nani? Maana kitakachoendelea ni kuviziana na kuharibiana mambo mengi kama tunashukiana
 
Tunako elekea Polisi watakua na weledi badala ya kutanguliza kifua mbele kama watunisha misuli.

Ukiwakuta site wanatumia nguvu kubwa kwenye vitu ambavyo haviitaji nguvu. Unprofessional
Sasa hapo nguvu na kutotumia weledi kupi kulikotumika wakati taratibu zote wamefuata?..
 
Safari hii vipi tena? Maana mara zote wao ndiyo wanawaua majambazi kwenye mapambano na wao wanatoka wakiwa hawana hata mchubuko!
 
Na wewe ni polisi au muke wa polisi

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Inaelekea hao askari hawakujua kuwa jamaa alikuwa na silaha. Kama yale ya Zakaria miaka ile.

Wangejua, bila shaka wangemnyemelea kwa tahadhari kubwa kama ilivyokuwa kwa Hamza.

Kwa vyovyote vile, polisi wawe makini na kazi zao. Siasa imewapunguzia weledi. Kushughulika na majambazi wa ukweli si sawa kushughulikia wapinzani au zile drama wanazosimulia kwenye PR zao. Na hizi tuhuma za utekaji badala ya ukamataji ndio zinaharibu kabisa.
 
P
Ukiona bidii kubwa ya jeshi la polisi la Tanzania kwenye tukio la ukamataji fahamu kilichokuwa kinafuatwa ni zaidi ya mtuhumiwa, mfano aliyewacholea ramani kawahadaa jamaa ana kilo 8 za dhahabu, jamaa wakajaa, ni mawazo yangu Tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…