Polisi wenye silaha wamevamia Kanisa Katoliki, Mwanjelwa Mbeya, na kuwatoa nje wafuasi wa Chadema ambao ni waumini wa kanisa hilo kwa madai ya kutaka kumuombea Mbowe na kufanya maandamano baada ya ibada.
Polisi wamesema wafuasi wa Chadema walipanga leo wakamuombee Mbowe, na wakimaliza ibada wafanye maandamano kupinga kiongozi wao kushikiliwa kwa tuhuma za ugaidi. Hivyo wakazingira Kanisa hilo na kuamuru wafuasi wote wa Chadema watoke nje. Baadhi walitoka lakini wengine waliendelea na ibada.
Kiongozi mmoja wa jumuiya ambaye ni mjumbe wa CCM wilaya, aliwaambia polisi kwamba kuna waliokataa kutoka. Hivyo aliongozana na polisi kuingia ndani ya kanisa, na ku-point wafuasi wa Chadema anaowajua na polisi kuwatoa kwa nguvu. Hali hiyo imesababisha taharuki na kusimamisha ibada kwa muda hadi Polisi walipomaliza zoezi lao.
#MyTake:
1. Wafuasi wa Chadema wana haki ya kumuombea kiongozi wao kwa imani zao bila kuingiliwa na yeyote. Ni upumbavu kuwazuia kumuombea. Mmemkamata, mmemtuhumu kwa ugaidi. Bado mnaumia hata akiombewa? What a shame.!
2. Kama polisi waliambiwa Chadema wamepanga kuandamana baada ya ibada, wangesubiri ibada imalizike waone kama wataandamana ndipo wawadhibiti. Sio kwenda kuvamia iabda na kuwatoa kwa nguvu.
3. Polisi hawana mamlaka ya kuingilia ibada yoyote (hata ya mizimu) kama ibada hiyo haihatarishi amani. Elisha alipokua ktk ibada, kuna vijana walimdhihaki pale Betheli, ghafla wakatoka dubu porini na kuwararua wakafa. Wale waliopona vizazi vyao vililaaniwa, wakazaa mapooza. Kwahiyo Polisi wote waliohusika na dhambi hii wajiandae kubeba laana kwao na vizazi vyao.
4. Makanisa yote ya Kikristo yanapaswa kutoa KAULI KALI kukemea UDIKTETA huu. Kwanini waumini watolewe nje kwa sababu tu ni wa chama fulani? Uko wapi uchaji wa ibada? Iko wapi heshima ya Kanisa? Leo wametoa waumini, tusipokemea kesho watamtoa Askofu kwa mateke.
5. Hiki ni kiwango cha juu cha kudharau imani. JPM pamoja na "ubabe" wake hakuthubutu kutoa watu kanisani ili awakamate. Kanisa limedharauliwa sana leo. Litoke liseme NENO. Kanisa lisiposema, MUNGU mwenyewe ATASEMA.!
View attachment 1867776