Mwanamwana
Platinum Member
- Aug 1, 2011
- 9,604
- 22,722
Askari wawili wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia Mkoa wa Mbeya, wamefariki dunia katika ajali ya barabarani iliyotokea jana Desemba 16, 2025, katika eneo la Karasha, Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe, kwenye Barabara Kuu ya Mbeya—Tunduma.
Ajali hiyo ilihusisha gari la Mitsubishi Canter Boxbody la SGA Mbeya, lililokuwa likisafirisha fedha kutoka Tunduma kwenda Mbeya, pikipiki aina ya Fekon na gari la abiria Toyota Coaster lililokuwa likielekea Tunduma kutoka Mbeya. Askari waliopoteza maisha ni CPL Chirungu Misango John na PC Amina Japhari Hamisi.
Uchunguzi wa awali wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe umeeleza kuwa chanzo cha ajali ni uzembe wa dereva wa Coaster, aliyegonga pikipiki na kupoteza mwelekeo na kusababisha kugongana uso kwa uso na Canter, huku mwendo kasi katika eneo la makazi ukichangia.