Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Hii logical fallacy ni logical non sequitur.Cheo cha Rais, Makamo, PM, Mawaziri na Wakuu wa Mikoa vimetajwa kwenye katiba, nionyeshe cheo cha Naibu PM kimetajwa kwenye ibara ipi? Kwamba Waziri Mkuu aliyepo ameshindwa kazi mpaka awe na Naibu? Mrema alivyoomba maslahi ya Naibu PM aliambiwa hicho cheo hakipo kikatiba na Ndugai au ulikuwa bado mchanga?
Kwa kuwa kuna vyeo vimetajwa kwenye katiba, hilo halimaanishi kila cheo ni lazima kitajwe kwenye katiba.
Kwani katiba imetaja mabalozi? Katiba imetaja makatibu wakuu wa wizara? Katiba imetaja ma RAS?
Mbona rais anateua watu kushika hivyo vyeo kila mara?
Mrema cheo kutokuwepo kwenye katiba si issue, kwa sababu kuna vyeo vingi sana haviko kwenye katiba. Labda useme kuna vitu havikurasimishwa na kuandikwa vizuri, katiba inasema rais ana mamlaka ya kuunda na kuondoa vyeo katika utumishi wa umma. Maana yake anaweza kuweka cheo cha Naibu Waziri Mkuu, kama anavyoweza kuamua Wizara ya Fedha iwe na manaibu wawili.
Hoja ya "mbona cheo hakipo katika katiba" ni mufilisi, kwa sababu mabalozi, ma RAS, makatibu wakuu wa wizara, wakurugenzi wa mashirika ya umma wanateuliwa na rais, lakini vyeo vyao haviko katika katiba.