Askofu Almachius Rweyongeza: JamiiForums pekee ndio wameripoti Waraka wa TEC mkataba wa DP World kwa Weledi

Askofu Almachius Rweyongeza: JamiiForums pekee ndio wameripoti Waraka wa TEC mkataba wa DP World kwa Weledi

Toka kwa baba askofu at :5:10

View: https://youtu.be/EOOgv3JLEj0

=====
Media zote Tanzania hajaripoti Waraka wa TEC isipokuwa ni mitadao ya kijamii pekee na JamiiForums pekee ndio wameripoti tena kwa weledi mkubwa, je waraka huo haukukidhi vigezo vya kuw ahabari kubwa? La hasha ulikidhi ila hajaripotiwa kwa kuwa huenda umezuiliwa usiripotiwe ili usiwafikie walio wengi, lakini hawakujua nguvu ya mitandao habari husambaa kwa haraka zaidi kuliko mainstreem.

Na nawaasa wakati wa uchaguzi mchague viongozi watakaofaa, uchaguzi uliopita ulikuwa na makosa mengi sasa mchague viongozi wanaoweza kuwatetea na kuongoza vyema, na nyie mtimize wajibu wenu, mnachagua viongozi wanaobadili sheria za nchi ili ziwafae, na mnapewa rushwa na kuchagua viongozi wasiofaa sasa mnaanza kutuuliza sisi tuwasemee kwa nini mnatusukumia sisi,

Sisi tumetimiza wajibu wetu na tuko tayari kufa ndio maana ya nguo nyekundu hizi, tuko tayari kufa kwani tutakuwa tumekufa pamoja na Kristo kwa kutimiza wajibu wetu tatizo litabaki kwenu mtimize wajibu wenu.

Huyo padri anasubiri jamaa yao kadedi ndio anasema uchaguzi ulikuwa na mapungufu, kama yeye mwanaume kweli angesema kipindi kile mgalatia mwenzao yuko hai.
 
Kama hoja ni mawazo ya wananchi kusikilizwa kwa nini hawakutoa waraka juu ya maoni ya wananchi kusikilizwa pale wananchi walipowalalamikia wenzao kula pesa za escrow?
Kaka kama masuala binafsi yatahitaji kutolewa waraka itakuwa kila siku ni waraka 😆😆😆....
 
Huyo padri zuzu kweli anasubiri jamaa yao kadedi ndio anasema uchaguzi ulikuwa na mapungufu, kama yeye mwanaume kweli angesema kipindi kile mgalatia mwenzao yuko hai.
Huyo Mama yenu asingekuwa Rais, bila Magufuli
 
Huyo padri zuzu kweli anasubiri jamaa yao kadedi ndio anasema uchaguzi ulikuwa na mapungufu, kama yeye mwanaume kweli angesema kipindi kile mgalatia mwenzao yuko hai.
Acheni mambo ya udini nyie watu.

Jee Masheikh waliwahi kulaani utawala Wa Magufuli?
 
Badala yake ni tamko lililo wafikia wengi zaidi kuliko walivyo dhani.
Asante mno jamii forums, hampo kwa bahati mbaya, kusudi la uwepo jamii forum ni ukombozi wa fikra zetu, ukombozi wa uhuru wetu, ukombozi wa kila linalo tupasa.
Jamii forums itakuwepo na itazidi kuwepo
 
Sasa kama limewafikia watu wengi kwa nini mnalalamika halijatangazwa na mainstream media?

Tukisema nyie watu mmechanganyikiwa mnatusema tunawaonea!

Mnasumbuliwa na sonona, chuki na msongo wa mawazo kwa kweli
 
Kwani kuachiwa inamaanisha hujafanya kosa?

Zombe aliachiwa kuhusu mauaji wa wafanyabiashara wa madini ila unaamini hakufanya lile kosa?
Zombe mahakama ilisema Ili kumtia hatiani ni mpaka awepo Koplo Sad kuthibitisha kuwa alitumwa na Zombe kuwaua wale wafanyabiashara wa madini wa mahenge.

Kwa Ivo mahakama haikuwahi kusema kuwa Zombe ana ama hana hatia mpaka pale Koplo Sad atakapopatikana.

Kwa ishu ya Rugemalira yeye hata kesi yenyewe haijawahi kuendeshwa.
 
Media za Tanzania kwa asilimia kubwa zinalelewa na CCM, ingekuwa ishu inayohusu CCM tena wangerusha 'live'.
 
Kwa hiyo malalamiko ya wananchi juu ya pesa za escrow yalikuwa masuala binafsi?
Mm binafsi niliona hivyo,labda nitoe kamfano ;pesa yako umeuza kiwanja ukagawa kwa jamaa zako.
Mm niitake pesa hiyo kwa madai yapi kaka.?

Mm nilielewa ilikuwa sehemu ya mtu binafsi aliyepata gawio lake akaamua kugawa kwa watu wake anawajua.
 
Zombe mahakama ilisema Ili kumtia hatiani ni mpaka awepo Koplo Sad kuthibitisha kuwa alitumwa na Zombe kuwaua wale wafanyabiashara wa madini wa mahenge.

Kwa Ivo mahakama haikuwahi kusema kuwa Zombe ana ama hana hatia mpaka pale Koplo Sad atakapopatikana.

Kwa ishu ya Rugemalira yeye hata kesi yenyewe haijawahi kuendeshwa.
Kwani Rugemalila mahakama ilisema hana hatia?
 
Sasa kama limewafikia watu wengi kwa nini mnalalamika halijatangazwa na mainstream media?

Tukisema nyie watu mmechanganyikiwa mnatusema tunawaonea!

Mnasumbuliwa na sonona, chuki na msongo wa mawazo kwa kweli
Tulia brother, angalia hata upepo unavuma kuekekea wapi, uchawa usikutie aibu kiasi hicho.
 
Back
Top Bottom