Uchaguzi 2020 Askofu Bagonza aitaka NEC isitumike kudhulumu Watanzania

Uchaguzi 2020 Askofu Bagonza aitaka NEC isitumike kudhulumu Watanzania

Sasa kama wagombea toka upinzani wameuza nafasi unataka NEC wafanyaje?
 
Kukemea dhambi ndio kazi zao.. Watu wakinajisi chama chetu au mifumo yetu ya kiutawala wametenda dhambi na lazima viongozi wa dini wawakemee.. Wanajua haki huinua taifa lazima waongee shetani ashindwe.

Maaskofu hawahawa wanaokuja hapa na kukemea dhambi lakini majumbani kwao wanashindwa kuzikemea familia zao?

Unakuta baadi ya maasikofu vijana wao wameshindikana na wameshindwa kuwakemea.

Utakuta huyo askofu anakemea lakini yeye mwenyewe ni roho mbaya hata msaada hana kwa jamii anayoiongoza.
 
Na hawa wa makanisani wangekaa kimya kuhusu siasa au Serikali ingewasweka kama mashehe wa Uamsho, maana nao siasa ziliwaponza baada ya kuhangaika na dini zao.
Huyu askofu anajitambua sana siyo wale wanao jikomba komba kwa watawala.
 
Historia gani wakati mtu analaani maovu yanayotendeka wakati huu, tendeni haki kwa wapinzani sanduku la kura litaamua, wacheni huo uhuni wenu wa kuchagulia watu viongozi wasiowataka.
Hawa watu ipo siku watayakumbuka sana maneno yetu ingawa kwa sasa wanatuona kama tunampigia mbuzi gitaaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Askofu unaongea na sikio la kufa?

CCM NA TAASISI ZAKE WAMEKUWA NI MBUZI HATA UWAPIGIE GITARI HAWAWEZI KUUSIKIA MZIKI WOWOTE

HAO NI CANCER NA DAWA YAKE NI KUFANYIWA OPERATION TU
Angalau tumsifu kwa hili aliloweza kulifanya, maana wengi wao wameziba kabisa masikio kisa wanahijaji kujaza matumbo yao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MBARIKIWE MAASKOFU NA WATUMISHI MNAO HUBIRI HAKI.

Najjuliza sana Hivi kwanini selikali inafanya huu upumbavu ??

Mbona ni dharau kubwa sana kwa Watanzania??

Kwa nini muwachagulie wananchi viongozi wa kuwaongoza??????
 
Na hawa wa makanisani wangekaa kimya kuhusu siasa au Serikali ingewasweka kama mashehe wa Uamsho, maana nao siasa ziliwaponza baada ya kuhangaika na dini zao.

Naam, watu wa aina yako, mnapashwa kunyamaza ama kuuliza ili mjifunze maana na uhusiano kati ya Serikali, Siasa na Kanisa. Vinginevyo utakuwa mpumbavu tu kuzungumzia masuala usiyoyajua.
 
Dkt. Kigwangalla badala ya kugombana na Mo Dewji angekuja huku kupata mawaidha!
 
Tume wanasimamia sheria.

Hili jambo litoe funzo kubwa kwa vyama kuhusu umakini wa kujaza fomu. Ujazaji fomu usiwe jukumu binafsi la mgombea bali chama chake. Chama kiwakusanye wagombea wake wa jimbo au mkoa pamoja kisha wasimamiwe kujaza na zikaguliwe ndipo waruhusiwe kuzirudisha tena kwa kusindikizwa.
Kumbuka kuna wagombea wanajaza vibaya makusudi na kuna wanaojaza vibaya sababu ya uelewa mdogo.
Hivi kama yule mgombea wa Moshi vijijini hata majina yake yaliyoko katika kitambulisho cha taifa hayajui?

Iweje fomu ajaze jina la Lucy na kitambulisho kina jina Lusesia tena na ubini majina tofauti je hawa ni mtu mmoja au wawili tofauti ? Ni rahisi kulaumu lakini kama wewe ndiyo unatakiwa uamue hizo rufaa na kanuni na sheria ziko wazi utapinda sheria tu ili kufurahisha watu?

Lingine, kwa kuwa hivi vyama viwili vya CDM na ACT ndivyo vinalalamikia zaidi jambo hili, busara hapa ni kumuunga mkono mgombea aidha wa ACT au CHADEMA ambaye amebaki kuliko kujidanganya wanaweza kulazimisha warudishwe kwa kufanya vurugu. Kule Pemba nimeona walau majina yasiyopungua mawili wamerejeshwa hivyo ACT wanaweza wasiwe na wagombea majimbo kama saba au sita hivi, lakini katika majimbo wasio na wagombea, CHADEMA wameweka wagombea kama majimbo manne hivi, kama kweli wanashirikiana kama wanavyodai ina maana mwisho wa siku wana wagombea kwa pamoja Pemba majimbo yasiyopungua 15 kati ya majimbo 18. Hivyo badala ya kuthubutu kufanya vurugu ambazo mwisho wa siku wanaweza hata wasishiriki uchaguzi na wakakosa uwakilishi kwa miaka mingine 5 ni bora waingie katika uchaguzi katika mazingira haya ya sasa kwani wana uhakika wa kambi yao kunyakua viti 15 .

Zaidi hivi ni viti vy bunge la muungano na Maalim Sefu shida yake kubwa ni urais wa Zanzibar ambao kama akishinda ana nafasi ya kuteua wawakilishi 10 katika Baraza la Wawakilishi.

Msijidanganye eti mtafanya vurugu, kwanza hamuwezi na pili hamtafanikiwa kuwarejesha walioenguliwa na mtapoteza hata ambacho ilikuwa mpate.

Jifunzeni sana kutii na kufuata sheria.
 
Back
Top Bottom