Tume wanasimamia sheria.
Hili jambo litoe funzo kubwa kwa vyama kuhusu umakini wa kujaza fomu. Ujazaji fomu usiwe jukumu binafsi la mgombea bali chama chake. Chama kiwakusanye wagombea wake wa jimbo au mkoa pamoja kisha wasimamiwe kujaza na zikaguliwe ndipo waruhusiwe kuzirudisha tena kwa kusindikizwa.
Kumbuka kuna wagombea wanajaza vibaya makusudi na kuna wanaojaza vibaya sababu ya uelewa mdogo.
Hivi kama yule mgombea wa Moshi vijijini hata majina yake yaliyoko katika kitambulisho cha taifa hayajui?
Iweje fomu ajaze jina la Lucy na kitambulisho kina jina Lusesia tena na ubini majina tofauti je hawa ni mtu mmoja au wawili tofauti ? Ni rahisi kulaumu lakini kama wewe ndiyo unatakiwa uamue hizo rufaa na kanuni na sheria ziko wazi utapinda sheria tu ili kufurahisha watu?
Lingine, kwa kuwa hivi vyama viwili vya CDM na ACT ndivyo vinalalamikia zaidi jambo hili, busara hapa ni kumuunga mkono mgombea aidha wa ACT au CHADEMA ambaye amebaki kuliko kujidanganya wanaweza kulazimisha warudishwe kwa kufanya vurugu. Kule Pemba nimeona walau majina yasiyopungua mawili wamerejeshwa hivyo ACT wanaweza wasiwe na wagombea majimbo kama saba au sita hivi, lakini katika majimbo wasio na wagombea, CHADEMA wameweka wagombea kama majimbo manne hivi, kama kweli wanashirikiana kama wanavyodai ina maana mwisho wa siku wana wagombea kwa pamoja Pemba majimbo yasiyopungua 15 kati ya majimbo 18. Hivyo badala ya kuthubutu kufanya vurugu ambazo mwisho wa siku wanaweza hata wasishiriki uchaguzi na wakakosa uwakilishi kwa miaka mingine 5 ni bora waingie katika uchaguzi katika mazingira haya ya sasa kwani wana uhakika wa kambi yao kunyakua viti 15 .
Zaidi hivi ni viti vy bunge la muungano na Maalim Sefu shida yake kubwa ni urais wa Zanzibar ambao kama akishinda ana nafasi ya kuteua wawakilishi 10 katika Baraza la Wawakilishi.
Msijidanganye eti mtafanya vurugu, kwanza hamuwezi na pili hamtafanikiwa kuwarejesha walioenguliwa na mtapoteza hata ambacho ilikuwa mpate.
Jifunzeni sana kutii na kufuata sheria.