Askofu Bagonza: JWTZ ni Jeshi la Wananchi, si Jeshi la Watawala wala Viongozi!

Askofu Bagonza: JWTZ ni Jeshi la Wananchi, si Jeshi la Watawala wala Viongozi!

Tatizo la Jiwe anajua madhambi anayoyatenda na Ndiyo maana anataka Kuweka imani katika Majeshi! Bila shaka hata Watumwa wake kawaambiwa Waongezewa posho na Mishahara kama Mkuchika alivyotanabaisha pale Bungeni.
'To every action there is an equal opposite reaction' 3rd Newton's Law of Motion. Atavuna anachokipanda huyu Jiwe.
 
tusijisumbue wakuu wa majeshi kama mkuu wetu wapo duniani. juz tuu imetokea Sudani. wananchi wanajua nani mtenda haki na nini kibaraka wa mtawala. siku ikifika hata yeye wananchi watamkataa pamoja na boss wake.

kwa wasiofatilia mambo huko sudani Bashiri alipofurushwa jeshi lilikamata usukani. na kwa kawaida mkuu wa majeshi ndio huwa rais japo ni rais kijeshi. akatoa amri watu watawanyike na kutangaza hali ya hatari kwa miezi mitatu watu wasitoke nje. wananchi wamemgomea na kumwambia yeye naye atoke kwenye kiti maana alikua karibu na rais dicteta aliyepita na kushirikiana naye kwa maovu meng. hivyo hawana imani naye. kama hatak kujiuzuru nao hawatoki mtaan akitaka awauwe wooote atawale miti. baada ya siku tatu kaondoka madarakan na mwingine kushika kijiti.

ukiwa mtenda mema watu wanaona na ukiwa mwovu wanakujua pia
 
Katika mazingira hayo Askofu ina maana nchi yetu mfumo wa ulinzi hakuna Amiri Jeshi Mkuu, nafikiri tafsiri ya Jeshi la Wananchi inatafsiriwa kiholela na kupotosha umma, nchi zilizoendelea Sana Zina mifumo mingi ya usalama kabla ya Majeshi ya ulinzi.
Chukulia mfano wa matatizo ya Kibiti Jeshi la Polisi lilizidiwa na raia waliojihami kwa silaha wakiendesha ugaidi, Serikali iliongeza kasi kwa kutuma jeshi la ulinzi na likadhibiti, wakati mwingine nchi zetu Zina wasaliti wanaopanga njama sophisticated ambazo zinazidi uwezo wa Jeshi la Polisi,Serikali makini itachukua hatua mara moja bila ya kuangalia sura ya mtu au cheo chake au Chama.
Gunga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Binafsi sipendi sana Maaskofu kuingilia mambo ya siasa pia.. Hii ni kumbukumbu nzuri ila naye Askofu sio kazi yake kuingilia ingilia siasa, kazi yake kuu ni kanisani na kuhubiri injili, ila hii nakubali ni reminder bora kwa viongozi wote, kama Sudan jeshi lilivyoaungana na wananchi, kwani jeshi ni la wananchi..!! Ila Baba Askofu, si kila kazi ya siasa unataka kufanya..!! Ila wamekusikia, niongezee kidogo, nachojua Jeshi la wananchi kazi yao kubwa ni kulinda mipaka ya nchi, tusivamiwe kutoka nje, mambo ya ndani ya nchi, najua ni Jeshi la polisi, sasa naona kama jukumu kuu linasahaulika kidogo kidogo
 
HAPPY BIRTHDAY MWALIMU JKN.

Hayati Baba wa Taifa, leo 13/4/2019 angetimiza miaka 97 ya kuzaliwa. Alizaliwa tarehe ya leo mwaka 1922. Niandike jambo moja kama kumbukizi na kumuenzi.

Mwaka 1985, wakati anastaafu, alihojiwa na chombo kimoja cha habari. Akaulizwa ataje jambo moja lililomsikitisha sana katika utawala wake, na moja lililomfurahisha sana. Alifikiri kabla ya kujibu. Na baadaye alitaja maasi ya jeshi (KAR) ya mwaka 1964. Tukio hili lilimsikitisha sana.

Akifafanua, alisema tulikuwa na miaka 3 tangu tupate uhuru. Tuliupata uhuru kwa kuwatukana sana wakoloni na mabeberu na kutangaza kuwa tunataka kuwa huru na kujitawala. Tulitumia kila aina ya lugha kuonyesha ubaya wa waingereza na majeshi yao.

Jeshi lilipoasi, Mwalimu na wenzake walitoa amri kuwataka wanajeshi waweke silaha chini lakini wanajeshi waligoma.

Ndipo baada ya siku kadhaa, Mwalimu na wenzake walilazimika kuomba msaada wa meli ya kijeshi ya Waingereza iliyokuwa Pwani ya mahali fulani. Kamanda wa meli hiyo, akitumia kipaza sauti toka melini, alitoa amri kuwataka wanajeshi walioasi waweke silaha chini na kurudi kambini Kolito. Walitii. Hili lilimsikitisha sana Mwalimu. Kuona wanajeshi wake wanatii amri ya mkoloni na kukaidi amri ya kiongozi wao mzalendo.

Masikitiko ya Mwalimu ndicho kiini cha kuvunja jeshi la KAR na kuunda JWTZ. Katika kifupi hiki cha jina la jeshi letu jipya, Mwalimu alisema, alipenda sana neno "Wananchi".

Kwa fahari kubwa, Mwalimu alipokuwa akitaja kuwa jeshi letu tangu wakati huo ni jeshi la wananchi, alionekana kuwa na furaha kubwa.

Mwalimu alituachia jeshi la Wananchi. Si jeshi la viongozi, wala la vyama, wala la awamu, wala la mtu yeyote. Ni jeshi la Wananchi.

Tukio lilomfurahisha alilitaja. Si kusudi ya kumbukizi hii. Watakaopenda kulijua, wasubiri siku nyingine.

Utaendelea kuishi Mwalimu.

Happy Birthday Mwalimu wetu Asiyestaafu.

Imeandikwa na Askofu Benson Bagonza (PhD)
Niliacha Sana kutumia references za Mwalim ...mwalimu aliongoza nchi ya chama kimoja..jeshi lilikuwa la wananchi wa chama kimoja. Jeshi lilikuwa la chama kimoja...yeye mwenyewe mwalimu alipeleka wanaTANU na baadae wanaCCM jeshi ili kuli-politicise jeshi...matokeo yake ndio haya tunayaona Leo...mwalimu alituachia vingi vya hovyo(kwa ujinga wetu tumeshindwa kuvirekebisha) mfano katiba inayomtaka mkuu wa nchi kuwa mkuu wa serikali, inayomtaka rais asishtakiwe mahakamani n.k lengo lake hasa lilikuwa ni Nini???

Happy birthday Mwalimu, upumzike kwa amani Ila you could have done better.
 
Jeshi linalotishia tishia wananchi halina hadhi ya kuitwa jeshi la wananchi inafaa liitwe jeshi dhidi ya wananchi. Linapoteza sifa na kufanana na jeshi la kikoloni!! Mobeyo ajitafakari kauli yake.
Sikuhizi limekuwa jeshi la kujenga jenga hata kama hakuna dharuru wakati tunahitaji makampuni ya ujenzi yakuwe na yatoe na ajira kwa watoto wetu. Wanajeshi wana ajira na mishahara tayari ingefaa wawaache vijana wengine walio wengi nao wajipatie kipato katika ujenzi. Hukuti maajabu haya nchi zinazoendelea labda hizi zisizoeleweka zinaenda ama zinarudi.
 
Katika mazingira hayo Askofu ina maana nchi yetu mfumo wa ulinzi hakuna Amiri Jeshi Mkuu, nafikiri tafsiri ya Jeshi la Wananchi inatafsiriwa kiholela na kupotosha umma, nchi zilizoendelea Sana Zina mifumo mingi ya usalama kabla ya Majeshi ya ulinzi.
Chukulia mfano wa matatizo ya Kibiti Jeshi la Polisi lilizidiwa na raia waliojihami kwa silaha wakiendesha ugaidi, Serikali iliongeza kasi kwa kutuma jeshi la ulinzi na likadhibiti, wakati mwingine nchi zetu Zina wasaliti wanaopanga njama sophisticated ambazo zinazidi uwezo wa Jeshi la Polisi,Serikali makini itachukua hatua mara moja bila ya kuangalia sura ya mtu au cheo chake au Chama.
Gunga

Sent using Jamii Forums mobile app
Pole aana We hujui kinachoendelea kibiti ni heri ungekaa kimya.lait kama vyombo vya habari vingeruhusiwa kuripoti usingeandika ulicho andika hapa.Mbona walimzima Azory gwanda alipokwenda kuripoti.You are just arguing from ignorance.
 
Akae kimya inatosha. Kama ujumbe wapo wasemaji wa ulinzi wangelisemea. Mpaka yeye kasema ina maana hali tete! Kweli au ni siasa na mihemuko yake?
Aisee, kwahiyo yeye kama mkuu wa jeshi mlitarajia angeongela vita wakati hatuna vita, au majukumu ya jeshi wakati wa amani yamebadilika!!!
 
Kivipi mkuu!!! Nyinyi mlitaka amkabe na kisu au mnatakaje makamanda!!!
Ukimya hua ni Jambo zuri sana kwa watu wenye busara.

Kuna Lugha hakutakiwa azitamke hadharani kwenye mikutano ya wanasiasa hasa wakati huu wa Serikali za Kidemokrasia ambazo zinaongozwa na RAIA wenyewe.

Mkuu wa majeshi akionyesha kuingia kwenye misuguano ya ndani ya kisiasa na kuonekana wazi kuwa yupo upande mmoja ni hatari sana kwa usalama wa nchi dhini ya adui wa nje.
Ni rahisi kuwanyamazisha kabisa wananchi na hata kuwafyekelea mbale wale asiowataka lakini ni hatari sana endepo anatokea adui wa nje mana wale wasipendwa wataungana na adui wa nje.

Umoja wetu ndio uliolifanya jeshi letu kumtoa nduli Iddi Amini . Jeshi la Uganda wakati huo lilizidiwa sana mana lilikua linatumia mabavu kwa wananchi wake hasa wale ambayo hawakumuunga mkono Nduli Iddi Amini. Hali ilipelekea Jeshi letu lilipoingia Uganda lipokelewe kwa Vigelegele kama mkombozi wa Wanyonge.

CDF ni mtu mkubwa sana anapaswa aongee kwa tahadhari kubwa sana mana Chombo anachokiongoza ni cha kimataifa na kitaifa na kina Nguvu kubwa kwa wanasiasa na hata watawala.

Kwa sasa inaonekana kuwa makada wa CCM wameshaanza kuwaona makamanda wa hivi vyombo kuwa kama green guard yao. Hata wale Makaka na madada wakuu wa mikoa na Wilaya wanajaribu kuwatuma tuma mbele za watu na kuwaona kama vile ni wanasiasa wenzao.
Hili sio jambo jema sana.
Itafikia mahali wakishaanza kuzoea utamu wanaoupata raia ambayo ni wanasiasa itakua ni vigumu sana kuwaweka mbali mana wataona raia wao ni nani mpaka wajilimbikizie madaraka na mishahara mikubwa na Mali nyingi ili hali hawana uzalendo wa kuweza kuilinda nchi kwa kujitoa hata maisha!!

Tuepuke sana kuwaingiza wajeda wetu kwenye siasa mana sio wote watakaoipenda CCM tuu. Haiwezekana.
Wengine watakua hawana vyama kabisa kama sheria inavyowataka lakini wataibuka watakaoona kuwa Vyama vingine navyo vina binadamu wanaopaswa kutendewa haki.
Hapo ndio inapokuwa shida.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom