Askofu Bagonza: JWTZ ni Jeshi la Wananchi, si Jeshi la Watawala wala Viongozi!

Askofu Bagonza: JWTZ ni Jeshi la Wananchi, si Jeshi la Watawala wala Viongozi!

Katika mazingira hayo Askofu ina maana nchi yetu mfumo wa ulinzi hakuna Amiri Jeshi Mkuu, nafikiri tafsiri ya Jeshi la Wananchi inatafsiriwa kiholela na kupotosha umma, nchi zilizoendelea Sana Zina mifumo mingi ya usalama kabla ya Majeshi ya ulinzi.
Chukulia mfano wa matatizo ya Kibiti Jeshi la Polisi lilizidiwa na raia waliojihami kwa silaha wakiendesha ugaidi, Serikali iliongeza kasi kwa kutuma jeshi la ulinzi na likadhibiti, wakati mwingine nchi zetu Zina wasaliti wanaopanga njama sophisticated ambazo zinazidi uwezo wa Jeshi la Polisi,Serikali makini itachukua hatua mara moja bila ya kuangalia sura ya mtu au cheo chake au Chama.
Gunga

Sent using Jamii Forums mobile app
Wacha uongo wewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Binafsi sipendi sana Maaskofu kuingilia mambo ya siasa pia.. Hii ni kumbukumbu nzuri ila naye Askofu sio kazi yake kuingilia ingilia siasa, kazi yake kuu ni kanisani na kuhubiri injili, ila hii nakubali ni reminder bora kwa viongozi wote, kama Sudan jeshi lilivyoaungana na wananchi, kwani jeshi ni la wananchi..!! Ila Baba Askofu, si kila kazi ya siasa unataka kufanya..!! Ila wamekusikia, niongezee kidogo, nachojua Jeshi la wananchi kazi yao kubwa ni kulinda mipaka ya nchi, tusivamiwe kutoka nje, mambo ya ndani ya nchi, najua ni Jeshi la polisi, sasa naona kama jukumu kuu linasahaulika kidogo kidogo
Siasa ni nini mkuu? Kwangu siasa ni maisha. Bila siasa askofu atahubiri kwa nani?
 
Binafsi sipendi sana Maaskofu kuingilia mambo ya siasa pia.. Hii ni kumbukumbu nzuri ila naye Askofu sio kazi yake kuingilia ingilia siasa, kazi yake kuu ni kanisani na kuhubiri injili, ila hii nakubali ni reminder bora kwa viongozi wote, kama Sudan jeshi lilivyoaungana na wananchi, kwani jeshi ni la wananchi..!! Ila Baba Askofu, si kila kazi ya siasa unataka kufanya..!! Ila wamekusikia, niongezee kidogo, nachojua Jeshi la wananchi kazi yao kubwa ni kulinda mipaka ya nchi, tusivamiwe kutoka nje, mambo ya ndani ya nchi, najua ni Jeshi la polisi, sasa naona kama jukumu kuu linasahaulika kidogo kidogo

Umemwonea Askofu. Mimi naona kaandika kumbukizi la Mwalimu. Jana ilikuwa siku ya Kuzaliwa kwakwe kama juzi ilivyokuwa ya Sokoine. Tunaofanya siasa ni sisi tunaochambua yasiyokuwamo katika kumbukizi. Au mimi miwani yangu haisomi vizuri? Askofu kamkumbuka Mwalimu alivyotoa maoni yake kuhusu maasi ya jeshi. Kuna tatizo gani hapo jay One?
 
HAPPY BIRTHDAY MWALIMU JKN.

Hayati Baba wa Taifa, leo 13/4/2019 angetimiza miaka 97 ya kuzaliwa. Alizaliwa tarehe ya leo mwaka 1922. Niandike jambo moja kama kumbukizi na kumuenzi.

Mwaka 1985, wakati anastaafu, alihojiwa na chombo kimoja cha habari. Akaulizwa ataje jambo moja lililomsikitisha sana katika utawala wake, na moja lililomfurahisha sana. Alifikiri kabla ya kujibu. Na baadaye alitaja maasi ya jeshi (KAR) ya mwaka 1964. Tukio hili lilimsikitisha sana.

Akifafanua, alisema tulikuwa na miaka 3 tangu tupate uhuru. Tuliupata uhuru kwa kuwatukana sana wakoloni na mabeberu na kutangaza kuwa tunataka kuwa huru na kujitawala. Tulitumia kila aina ya lugha kuonyesha ubaya wa waingereza na majeshi yao.

Jeshi lilipoasi, Mwalimu na wenzake walitoa amri kuwataka wanajeshi waweke silaha chini lakini wanajeshi waligoma.

Ndipo baada ya siku kadhaa, Mwalimu na wenzake walilazimika kuomba msaada wa meli ya kijeshi ya Waingereza iliyokuwa Pwani ya mahali fulani. Kamanda wa meli hiyo, akitumia kipaza sauti toka melini, alitoa amri kuwataka wanajeshi walioasi waweke silaha chini na kurudi kambini Kolito. Walitii. Hili lilimsikitisha sana Mwalimu. Kuona wanajeshi wake wanatii amri ya mkoloni na kukaidi amri ya kiongozi wao mzalendo.

Masikitiko ya Mwalimu ndicho kiini cha kuvunja jeshi la KAR na kuunda JWTZ. Katika kifupi hiki cha jina la jeshi letu jipya, Mwalimu alisema, alipenda sana neno "Wananchi".

Kwa fahari kubwa, Mwalimu alipokuwa akitaja kuwa jeshi letu tangu wakati huo ni jeshi la wananchi, alionekana kuwa na furaha kubwa.

Mwalimu alituachia jeshi la Wananchi. Si jeshi la viongozi, wala la vyama, wala la awamu, wala la mtu yeyote. Ni jeshi la Wananchi.

Tukio lilomfurahisha alilitaja. Si kusudi ya kumbukizi hii. Watakaopenda kulijua, wasubiri siku nyingine.

Utaendelea kuishi Mwalimu.

Happy Birthday Mwalimu wetu Asiyestaafu.

Imeandikwa na Askofu Benson Bagonza (PhD)
Kauli ya jana ya cdf inaonyesha kuwa sio jeshi la wananchi tena bali la CCM na wasukuma wa awamu ya tano
 
Hapo ndio ujiulize kama Baba wa Taifa pamoja na kuwa mzalendo wa kweli kwenye nchi yake alipinduliwa ije iwe kwa awa wavunja katiba,sheria, kuminya uhuru wa kujieleza ? Haichukui hata dakika moja kuwekwa chini ya ulinzi na sijui kama Rwanda anaweza Saidia chochote.
Sijui unaenda tena kwa unaowaita mabeberu kuwaomba msaada? !!
Hakupinduliwa, wanajeshi walikuwa wanataka manadiliko kwenye uongozi wa jeshi, ndiyo sababu hawakuenda ikulu.
 
Back
Top Bottom