Askofu Bagonza: JWTZ ni Jeshi la Wananchi, si Jeshi la Watawala wala Viongozi!

Askofu Bagonza: JWTZ ni Jeshi la Wananchi, si Jeshi la Watawala wala Viongozi!

HAPPY BIRTHDAY MWALIMU JKN.

Hayati Baba wa Taifa, leo 13/4/2019 angetimiza miaka 97 ya kuzaliwa. Alizaliwa tarehe ya leo mwaka 1922. Niandike jambo moja kama kumbukizi na kumuenzi.

Mwaka 1985, wakati anastaafu, alihojiwa na chombo kimoja cha habari. Akaulizwa ataje jambo moja lililomsikitisha sana katika utawala wake, na moja lililomfurahisha sana. Alifikiri kabla ya kujibu. Na baadaye alitaja maasi ya jeshi (KAR) ya mwaka 1964. Tukio hili lilimsikitisha sana.

Akifafanua, alisema tulikuwa na miaka 3 tangu tupate uhuru. Tuliupata uhuru kwa kuwatukana sana wakoloni na mabeberu na kutangaza kuwa tunataka kuwa huru na kujitawala. Tulitumia kila aina ya lugha kuonyesha ubaya wa waingereza na majeshi yao.

Jeshi lilipoasi, Mwalimu na wenzake walitoa amri kuwataka wanajeshi waweke silaha chini lakini wanajeshi waligoma.

Ndipo baada ya siku kadhaa, Mwalimu na wenzake walilazimika kuomba msaada wa meli ya kijeshi ya Waingereza iliyokuwa Pwani ya mahali fulani. Kamanda wa meli hiyo, akitumia kipaza sauti toka melini, alitoa amri kuwataka wanajeshi walioasi waweke silaha chini na kurudi kambini Kolito. Walitii. Hili lilimsikitisha sana Mwalimu. Kuona wanajeshi wake wanatii amri ya mkoloni na kukaidi amri ya kiongozi wao mzalendo.

Masikitiko ya Mwalimu ndicho kiini cha kuvunja jeshi la KAR na kuunda JWTZ. Katika kifupi hiki cha jina la jeshi letu jipya, Mwalimu alisema, alipenda sana neno "Wananchi".

Kwa fahari kubwa, Mwalimu alipokuwa akitaja kuwa jeshi letu tangu wakati huo ni jeshi la wananchi, alionekana kuwa na furaha kubwa.

Mwalimu alituachia jeshi la Wananchi. Si jeshi la viongozi, wala la vyama, wala la awamu, wala la mtu yeyote. Ni jeshi la Wananchi.

Tukio lilomfurahisha alilitaja. Si kusudi ya kumbukizi hii. Watakaopenda kulijua, wasubiri siku nyingine.

Utaendelea kuishi Mwalimu.

Happy Birthday Mwalimu wetu Asiyestaafu.

Imeandikwa na Askofu Benson Bagonza (PhD)


Wewe Ecolizer ni mchochezi. Unachukua maneno mawili unayakuza ili kushibisha tamaa yako. Askofu amemkumbuka Mwalimu katika siku yake ya kuzaliwa, wewe unakimbilia kuchochea tu. Hata mimi nimefurahi kujifunza kitu katika kumbukizi hii nzuri. Inanifanya nimuelewe Baba wa Taifa kwa mapana zaidi. Huyo Baba alikuwa kichwa, tusimuite jembe maana yamekuwa mengi siku hiz.
 
Nakubaliana na Mh zitto amesema sasa hivi nchi yetu imekua ni united republic of gangsters kimsingi hii kauli ya mabeyo ni kumtisha au kumuogopesha CAG hivyo wa tz bila kua seriaz watamuua CAG wetu
Sio Kweli, Kauli ya Kamanda haikulenga misuguano ya ndani ya Kisisasa kati ya CCM na ACT, au Ripoti ya CAG.
bali Tahadhari za kiusalama zenye kushirikisha maadui wa Nje ya mipaka ya Nchi.
Kuna jaribio la kuunda upya vikundi vya kigaidi ili vianze tena kufanya machafuko katika baadhi ya maeneo ya nchi yetu kama vile vya MKIRU.
Nakadhalika.




Sent using Jamii Forums mobile app
 
TUACHE KUDOGODESHA VITU VIKUBWA NA VYA DHAMANI KWENYE NCHI YETU.

Watanzania wenzangu navyofaham mimi, JESHI ni miongoni Mwa vyombo vya ulinzi na usalama wa Taifa Letu, na hati sisi wananchi ni sehemu ya ulinzi na usalama wa Nchi YETU pia. Sasa ikawa ndivyo kuna Ubaya gani kiongozi mkuu wa JESHI kuzungumza juu ya uimarishaji wa usalama wa Nchi yetu.

Tusisahau Chokochoko za kuvuruga amani zinaweza zikawa ndani ya Nchi au nnje ya Nchi, Sasa kama kiongozi wa JESHI anatoa tahadhari kwa wanaofanya hivyo kuna Kosa/dhambi gani mpaka tuwabebeshe mizigo ya Kisiasa isiyo wahusu?

Watanzania tufike hatua tuache kuhukumu kwa kila jambo. SIO kila anayezungumza ni interest za Kisiasa, mana "mtu unaposema JESHI limekuwa la Kisiasa tukisema udhibitishe unao huo ushahidi?"

Tusifikiri ulinzi na usalama wa Nchi ni kitu kdg Cha kuongeaongea tu vyovyote unavyo jisikia. NI issue ya maisha ya sisi watanzania na Nchi yetu. "It is about Death and lives". Sasa mtu unapozungumza jambo senstive kama hili kimasihara ni sawa na kuchezea shilingi Baharini, hebu TUACHENI MIZAHA kwenye mambo ya msingi ya Taifa Letu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole aana We hujui kinachoendelea kibiti ni heri ungekaa kimya.lait kama vyombo vya habari vingeruhusiwa kuripoti usingeandika ulicho andika hapa.Mbona walimzima Azory gwanda alipokwenda kuripoti.You are just arguing from ignorance.
Kiliendelea nini huko kibiti ? Tujulishe wananchi tusiojua kilichojiri kibiti japo kwa ufupi ili tutie nguvu katika kukikemea.
Hili ni jukwaa huru ndio mana ID halisi zimefichwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukimya hua ni Jambo zuri sana kwa watu wenye busara.

Kuna Lugha hakutakiwa azitamke hadharani kwenye mikutano ya wanasiasa hasa wakati huu wa Serikali za Kidemokrasia ambazo zinaongozwa na RAIA wenyewe.

Mkuu wa majeshi akionyesha kuingia kwenye misuguano ya ndani ya kisiasa na kuonekana wazi kuwa yupo upande mmoja ni hatari sana kwa usalama wa nchi dhini ya adui wa nje.
Ni rahisi kuwanyamazisha kabisa wananchi na hata kuwafyekelea mbale wale asiowataka lakini ni hatari sana endepo anatokea adui wa nje mana wale wasipendwa wataungana na adui wa nje.

Umoja wetu ndio uliolifanya jeshi letu kumtoa nduli Iddi Amini . Jeshi la Uganda wakati huo lilizidiwa sana mana lilikua linatumia mabavu kwa wananchi wake hasa wale ambayo hawakumuunga mkono Nduli Iddi Amini. Hali ilipelekea Jeshi letu lilipoingia Uganda lipokelewe kwa Vigelegele kama mkombozi wa Wanyonge.

CDF ni mtu mkubwa sana anapaswa aongee kwa tahadhari kubwa sana mana Chombo anachokiongoza ni cha kimataifa na kitaifa na kina Nguvu kubwa kwa wanasiasa na hata watawala.

Kwa sasa inaonekana kuwa makada wa CCM wameshaanza kuwaona makamanda wa hivi vyombo kuwa kama green guard yao. Hata wale Makaka na madada wakuu wa mikoa na Wilaya wanajaribu kuwatuma tuma mbele za watu na kuwaona kama vile ni wanasiasa wenzao.
Hili sio jambo jema sana.
Itafikia mahali wakishaanza kuzoea utamu wanaoupata raia ambayo ni wanasiasa itakua ni vigumu sana kuwaweka mbali mana wataona raia wao ni nani mpaka wajilimbikizie madaraka na mishahara mikubwa na Mali nyingi ili hali hawana uzalendo wa kuweza kuilinda nchi kwa kujitoa hata maisha!!

Tuepuke sana kuwaingiza wajeda wetu kwenye siasa mana sio wote watakaoipenda CCM tuu. Haiwezekana.
Wengine watakua hawana vyama kabisa kama sheria inavyowataka lakini wataibuka watakaoona kuwa Vyama vingine navyo vina binadamu wanaopaswa kutendewa haki.
Hapo ndio inapokuwa shida.


Sent using Jamii Forums mobile app
Umeongea neno la maana sana.

Mwenye masikio na asikie.
 
Utamu wa jeshi unapowatamanisha kuna siku watanogewa utamu na kukunyanyua kwenye kiti, asali tamu wewe
 
Wewe Ecolizer ni mchochezi. Unachukua maneno mawili unayakuza ili kushibisha tamaa yako. Askofu amemkumbuka Mwalimu katika siku yake ya kuzaliwa, wewe unakimbilia kuchochea tu. Hata mimi nimefurahi kujifunza kitu katika kumbukizi hii nzuri. Inanifanya nimuelewe Baba wa Taifa kwa mapana zaidi. Huyo Baba alikuwa kichwa, tusimuite jembe maana yamekuwa mengi siku hiz.
Halafu majembe yanakongomekwa mipini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naona jamaa wanakula tu mavyeo na wengine kuahidiwa ajira... Hii ina maana ya kuweka mazingira mazuri kwa walio juu wapate usingizi wa kutosha.
 
Hapo ndio ujiulize kama Baba wa Taifa pamoja na kuwa mzalendo wa kweli kwenye nchi yake alipinduliwa ije iwe kwa awa wavunja katiba,sheria, kuminya uhuru wa kujieleza ? Haichukui hata dakika moja kuwekwa chini ya ulinzi na sijui kama Rwanda anaweza Saidia chochote.

Sijui unaenda tena kwa unaowaita mabeberu kuwaomba msaada? !!
1. Nyerere alipinduliwa na nani ?
2. Nyerere alipinduliwa mwaka gani ?

Nb tafuta tofauti ya revolution na army mutiny
 
Huo ndiyo ukweli mchungu

Inashangaza kumwona Kamanda wetu Jenerali Mabeyo ameamua kumlinda Jiwe badala ya kuwalinda wananchi wa Tanzania, kama anavyotakiwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya mwaka 1977
Usishangae mkuu, wakuu wetu wa sasa wanachagua wakuu wa majeshi kwa ajili ya kulindwa wao pindi wanapofanya mafyongo, hujiulizi kwanini amiri jeshi mkuu anakua Rais? Na hajui hata cheo chochote cha kijeshi?
 
Hatujawahi kumpata unpopular commander kama huyu wa sasa. Amekinajisi chombo chetu tunachokipenda na kukiheshimu.

Uzuri ni kwamba makamanda wapo imara na wanajua boss wao ni kikaragosi kisicho na weledi lakini ukanda umembeba.
 
Jeshi limekuwa la 'Sisiemu' mfikishie taarifa JK Nyerere.

5/5
 
Back
Top Bottom