Sifi Leo
Platinum Member
- Mar 30, 2012
- 6,408
- 12,100
Nchini kwetu sauti kama hii zimefifia na kupotea. Tunamshukuru baba askofu na wote wanaothubitu kusema katika mazingira haya.HAPPY BIRTHDAY MWALIMU JKN.
Hayati Baba wa Taifa, leo 13/4/2019 angetimiza miaka 97 ya kuzaliwa. Alizaliwa tarehe ya leo mwaka 1922. Niandike jambo moja kama kumbukizi na kumuenzi.
Mwaka 1985, wakati anastaafu, alihojiwa na chombo kimoja cha habari. Akaulizwa ataje jambo moja lililomsikitisha sana katika utawala wake, na moja lililomfurahisha sana. Alifikiri kabla ya kujibu. Na baadaye alitaja maasi ya jeshi (KAR) ya mwaka 1964. Tukio hili lilimsikitisha sana.
Akifafanua, alisema tulikuwa na miaka 3 tangu tupate uhuru. Tuliupata uhuru kwa kuwatukana sana wakoloni na mabeberu na kutangaza kuwa tunataka kuwa huru na kujitawala. Tulitumia kila aina ya lugha kuonyesha ubaya wa waingereza na majeshi yao.
Jeshi lilipoasi, Mwalimu na wenzake walitoa amri kuwataka wanajeshi waweke silaha chini lakini wanajeshi waligoma.
Ndipo baada ya siku kadhaa, Mwalimu na wenzake walilazimika kuomba msaada wa meli ya kijeshi ya Waingereza iliyokuwa Pwani ya mahali fulani. Kamanda wa meli hiyo, akitumia kipaza sauti toka melini, alitoa amri kuwataka wanajeshi walioasi waweke silaha chini na kurudi kambini Kolito. Walitii. Hili lilimsikitisha sana Mwalimu. Kuona wanajeshi wake wanatii amri ya mkoloni na kukaidi amri ya kiongozi wao mzalendo.
Masikitiko ya Mwalimu ndicho kiini cha kuvunja jeshi la KAR na kuunda JWTZ. Katika kifupi hiki cha jina la jeshi letu jipya, Mwalimu alisema, alipenda sana neno "Wananchi".
Kwa fahari kubwa, Mwalimu alipokuwa akitaja kuwa jeshi letu tangu wakati huo ni jeshi la wananchi, alionekana kuwa na furaha kubwa.
Mwalimu alituachia jeshi la Wananchi. Si jeshi la viongozi, wala la vyama, wala la awamu, wala la mtu yeyote. Ni jeshi la Wananchi.
Tukio lilomfurahisha alilitaja. Si kusudi ya kumbukizi hii. Watakaopenda kulijua, wasubiri siku nyingine.
Utaendelea kuishi Mwalimu.
Happy Birthday Mwalimu wetu Asiyestaafu.
Imeandikwa na Askofu Benson Bagonza (PhD)
Jaman kwani mnamjua anayetishia utulivu wa nchi??!! Maana mkuu katupa jiwe gizani.Ukimya hua ni Jambo zuri sana kwa watu wenye busara.
Kuna Lugha hakutakiwa azitamke hadharani kwenye mikutano ya wanasiasa hasa wakati huu wa Serikali za Kidemokrasia ambazo zinaongozwa na RAIA wenyewe.
Mkuu wa majeshi akionyesha kuingia kwenye misuguano ya ndani ya kisiasa na kuonekana wazi kuwa yupo upande mmoja ni hatari sana kwa usalama wa nchi dhini ya adui wa nje.
Ni rahisi kuwanyamazisha kabisa wananchi na hata kuwafyekelea mbale wale asiowataka lakini ni hatari sana endepo anatokea adui wa nje mana wale wasipendwa wataungana na adui wa nje.
Umoja wetu ndio uliolifanya jeshi letu kumtoa nduli Iddi Amini . Jeshi la Uganda wakati huo lilizidiwa sana mana lilikua linatumia mabavu kwa wananchi wake hasa wale ambayo hawakumuunga mkono Nduli Iddi Amini. Hali ilipelekea Jeshi letu lilipoingia Uganda lipokelewe kwa Vigelegele kama mkombozi wa Wanyonge.
CDF ni mtu mkubwa sana anapaswa aongee kwa tahadhari kubwa sana mana Chombo anachokiongoza ni cha kimataifa na kitaifa na kina Nguvu kubwa kwa wanasiasa na hata watawala.
Kwa sasa inaonekana kuwa makada wa CCM wameshaanza kuwaona makamanda wa hivi vyombo kuwa kama green guard yao. Hata wale Makaka na madada wakuu wa mikoa na Wilaya wanajaribu kuwatuma tuma mbele za watu na kuwaona kama vile ni wanasiasa wenzao.
Hili sio jambo jema sana.
Itafikia mahali wakishaanza kuzoea utamu wanaoupata raia ambayo ni wanasiasa itakua ni vigumu sana kuwaweka mbali mana wataona raia wao ni nani mpaka wajilimbikizie madaraka na mishahara mikubwa na Mali nyingi ili hali hawana uzalendo wa kuweza kuilinda nchi kwa kujitoa hata maisha!!
Tuepuke sana kuwaingiza wajeda wetu kwenye siasa mana sio wote watakaoipenda CCM tuu. Haiwezekana.
Wengine watakua hawana vyama kabisa kama sheria inavyowataka lakini wataibuka watakaoona kuwa Vyama vingine navyo vina binadamu wanaopaswa kutendewa haki.
Hapo ndio inapokuwa shida.
Sent using Jamii Forums mobile app
Umenena vyema. Inahitaji kutambua kama ulivyo mfano wako wananchi wa uganda walishirikiana na wanajeshi wa Tanzania kumg'oa Idd Amin. Adui akirikiana na wananchi anaweza kulishinda jeshi imara lenye silaha za kisasa. Kulifanya jeshi la chama tawala na viongozi kwa njia yeyote ile ni ujinga na kulidhoofishaUkimya hua ni Jambo zuri sana kwa watu wenye busara.
Kuna Lugha hakutakiwa azitamke hadharani kwenye mikutano ya wanasiasa hasa wakati huu wa Serikali za Kidemokrasia ambazo zinaongozwa na RAIA wenyewe.
Mkuu wa majeshi akionyesha kuingia kwenye misuguano ya ndani ya kisiasa na kuonekana wazi kuwa yupo upande mmoja ni hatari sana kwa usalama wa nchi dhini ya adui wa nje.
Ni rahisi kuwanyamazisha kabisa wananchi na hata kuwafyekelea mbale wale asiowataka lakini ni hatari sana endepo anatokea adui wa nje mana wale wasipendwa wataungana na adui wa nje.
Umoja wetu ndio uliolifanya jeshi letu kumtoa nduli Iddi Amini . Jeshi la Uganda wakati huo lilizidiwa sana mana lilikua linatumia mabavu kwa wananchi wake hasa wale ambayo hawakumuunga mkono Nduli Iddi Amini. Hali ilipelekea Jeshi letu lilipoingia Uganda lipokelewe kwa Vigelegele kama mkombozi wa Wanyonge.
CDF ni mtu mkubwa sana anapaswa aongee kwa tahadhari kubwa sana mana Chombo anachokiongoza ni cha kimataifa na kitaifa na kina Nguvu kubwa kwa wanasiasa na hata watawala.
Kwa sasa inaonekana kuwa makada wa CCM wameshaanza kuwaona makamanda wa hivi vyombo kuwa kama green guard yao. Hata wale Makaka na madada wakuu wa mikoa na Wilaya wanajaribu kuwatuma tuma mbele za watu na kuwaona kama vile ni wanasiasa wenzao.
Hili sio jambo jema sana.
Itafikia mahali wakishaanza kuzoea utamu wanaoupata raia ambayo ni wanasiasa itakua ni vigumu sana kuwaweka mbali mana wataona raia wao ni nani mpaka wajilimbikizie madaraka na mishahara mikubwa na Mali nyingi ili hali hawana uzalendo wa kuweza kuilinda nchi kwa kujitoa hata maisha!!
Tuepuke sana kuwaingiza wajeda wetu kwenye siasa mana sio wote watakaoipenda CCM tuu. Haiwezekana.
Wengine watakua hawana vyama kabisa kama sheria inavyowataka lakini wataibuka watakaoona kuwa Vyama vingine navyo vina binadamu wanaopaswa kutendewa haki.
Hapo ndio inapokuwa shida.
Sent using Jamii Forums mobile app
Kwani ilikuwa lazima yeye aongee. Hata kama ni wakati wa amani ndio aongee vile kwa kuchimba mkwala. Wapi uliona hiyo! Umeongea kitoto, sorry kama nimekukwaza upo form gani?Aisee, kwahiyo yeye kama mkuu wa jeshi mlitarajia angeongela vita wakati hatuna vita, au majukumu ya jeshi wakati wa amani yamebadilika!!!
Kwani baada ya kumaliza vidato vyote ulijuaje kwamba sasa umekua??? , unafikiri kitoto zaidi.Kwani ilikuwa lazima yeye aongee. Hata kama ni wakati wa amani ndio aongee vile kwa kuchimba mkwala. Wapi uliona hiyo! Umeongea kitoto, sorry kama nimekukwaza upo form gani?
Suala la Kibiti lilikua na viashiria vya Ugaidi.Katika mazingira hayo Askofu ina maana nchi yetu mfumo wa ulinzi hakuna Amiri Jeshi Mkuu, nafikiri tafsiri ya Jeshi la Wananchi inatafsiriwa kiholela na kupotosha umma, nchi zilizoendelea Sana Zina mifumo mingi ya usalama kabla ya Majeshi ya ulinzi.
Chukulia mfano wa matatizo ya Kibiti Jeshi la Polisi lilizidiwa na raia waliojihami kwa silaha wakiendesha ugaidi, Serikali iliongeza kasi kwa kutuma jeshi la ulinzi na likadhibiti, wakati mwingine nchi zetu Zina wasaliti wanaopanga njama sophisticated ambazo zinazidi uwezo wa Jeshi la Polisi,Serikali makini itachukua hatua mara moja bila ya kuangalia sura ya mtu au cheo chake au Chama.
Gunga
Sent using Jamii Forums mobile app
Unaweza kuwa unaongea na baba yako humu,kuna siku yoyote umenote baba yako kukosea, je ulimsaidia kumlala mama yako!!!!
Simply kwa sababu nafasi ya baba haina mbadala.
Sasa unaona ulivyojibakiza uchi!!!! Uliuliza kidato ukiwa na maana gani!!! Maana wewe labda umevuka kidato cha sita, lakini upeo wako ni mashaka makubwa.Huku umri wa mtu unapimwa kwa hoja zake. Ukija na hoja za kitoto hata kama una karne 4 unaonekana mpuuzi tu.
Katika mazingira hayo Askofu ina maana nchi yetu mfumo wa ulinzi hakuna Amiri Jeshi Mkuu, nafikiri tafsiri ya Jeshi la Wananchi inatafsiriwa kiholela na kupotosha umma, nchi zilizoendelea Sana Zina mifumo mingi ya usalama kabla ya Majeshi ya ulinzi.
Chukulia mfano wa matatizo ya Kibiti Jeshi la Polisi lilizidiwa na raia waliojihami kwa silaha wakiendesha ugaidi, Serikali iliongeza kasi kwa kutuma jeshi la ulinzi na likadhibiti, wakati mwingine nchi zetu Zina wasaliti wanaopanga njama sophisticated ambazo zinazidi uwezo wa Jeshi la Polisi,Serikali makini itachukua hatua mara moja bila ya kuangalia sura ya mtu au cheo chake au Chama.
Gunga
Sent using Jamii Forums mobile app
Na yeye ndie alietufikisha hapa na li chama lakeNiliacha Sana kutumia references za Mwalim ...mwalimu aliongoza nchi ya chama kimoja..jeshi lilikuwa la wananchi wa chama kimoja. Jeshi lilikuwa la chama kimoja...yeye mwenyewe mwalimu alipeleka wanaTANU na baadae wanaCCM jeshi ili kuli-politicise jeshi...matokeo yake ndio haya tunayaona Leo...mwalimu alituachia vingi vya hovyo(kwa ujinga wetu tumeshindwa kuvirekebisha) mfano katiba inayomtaka mkuu wa nchi kuwa mkuu wa serikali, inayomtaka rais asishtakiwe mahakamani n.k lengo lake hasa lilikuwa ni Nini???
Happy birthday Mwalimu, upumzike kwa amani Ila you could have done better.
Kwa kweli hata Mimi imenishtua maana hatukuzoea kumsikia kamanda nae anaingia mambo ya siasa na kutumia maneno tata kama uchochezi. Hayo awaachie akina Siro!Huo ndiyo ukweli mchungu
Inashangaza kumwona Kamanda wetu Jenerali Mabeyo ameamua kumlinda Jiwe badala ya kuwalinda wananchi wa Tanzania, kama anavyotakiwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya mwaka 1977
Na yeye ndie alietufikisha hapa na li chama lake
PhD za ukweli utazijua tu,Mungu mbariki Askofu Bagonza.HAPPY BIRTHDAY MWALIMU JKN.
Hayati Baba wa Taifa, leo 13/4/2019 angetimiza miaka 97 ya kuzaliwa. Alizaliwa tarehe ya leo mwaka 1922. Niandike jambo moja kama kumbukizi na kumuenzi.
Mwaka 1985, wakati anastaafu, alihojiwa na chombo kimoja cha habari. Akaulizwa ataje jambo moja lililomsikitisha sana katika utawala wake, na moja lililomfurahisha sana. Alifikiri kabla ya kujibu. Na baadaye alitaja maasi ya jeshi (KAR) ya mwaka 1964. Tukio hili lilimsikitisha sana.
Akifafanua, alisema tulikuwa na miaka 3 tangu tupate uhuru. Tuliupata uhuru kwa kuwatukana sana wakoloni na mabeberu na kutangaza kuwa tunataka kuwa huru na kujitawala. Tulitumia kila aina ya lugha kuonyesha ubaya wa waingereza na majeshi yao.
Jeshi lilipoasi, Mwalimu na wenzake walitoa amri kuwataka wanajeshi waweke silaha chini lakini wanajeshi waligoma.
Ndipo baada ya siku kadhaa, Mwalimu na wenzake walilazimika kuomba msaada wa meli ya kijeshi ya Waingereza iliyokuwa Pwani ya mahali fulani. Kamanda wa meli hiyo, akitumia kipaza sauti toka melini, alitoa amri kuwataka wanajeshi walioasi waweke silaha chini na kurudi kambini Kolito. Walitii. Hili lilimsikitisha sana Mwalimu. Kuona wanajeshi wake wanatii amri ya mkoloni na kukaidi amri ya kiongozi wao mzalendo.
Masikitiko ya Mwalimu ndicho kiini cha kuvunja jeshi la KAR na kuunda JWTZ. Katika kifupi hiki cha jina la jeshi letu jipya, Mwalimu alisema, alipenda sana neno "Wananchi".
Kwa fahari kubwa, Mwalimu alipokuwa akitaja kuwa jeshi letu tangu wakati huo ni jeshi la wananchi, alionekana kuwa na furaha kubwa.
Mwalimu alituachia jeshi la Wananchi. Si jeshi la viongozi, wala la vyama, wala la awamu, wala la mtu yeyote. Ni jeshi la Wananchi.
Tukio lilomfurahisha alilitaja. Si kusudi ya kumbukizi hii. Watakaopenda kulijua, wasubiri siku nyingine.
Utaendelea kuishi Mwalimu.
Happy Birthday Mwalimu wetu Asiyestaafu.
Imeandikwa na Askofu Benson Bagonza (PhD)
Ulaji viwavi jeshi ni hatari kwa afya ya akili.Wewe utakuwa Mgogo, ndiyo maana akili yako haina kumbukumbu na inachokuamuru kuandika.
Huna tofauti na ndugai na lusinde.
UTAPIA MLO
Sent using Jamii Forums mobile app