Bado najiuliza kuhusu kauli ya Mabeyo sijapata majibu. Hivi kama ni kweli akiamua kuchukua hatua dhidi ya hao watu anaodai wanahatarisha amani na usalama wa nchi waliopo ndani atakuwa anatumia sheria gani? Atachukua majukumu ya Polisi na Magereza? Kwani Polisi wameshindwa kazi yao? Au anataka kuwapindua? Au atatangaza hali ya hatari? Haoni atakuwa amevunja sheria?
Nasikitika sana kwa mara ya kwanza Jeshi linataka kujitumbukiza ktk siasa, hata kipindi cha awamu ya kwanza wakati chama kimoja kilipokuwa pia Jeshini haikuwa hivi lengo lilikuwa ni kutengeneza uzalendo tu kwa wanajeshi, lakini Jeshi kama Jeshi lilifanya majukumu yake kwa kujibu wa sheria, sembuse leo hii wakati wa vyama vingi?
Tunaenda wapi huku, my country Tanzania
Sent using
Jamii Forums mobile app