Pre GE2025 Askofu Bagonza: Kanisa likijenga Shule ama Hospitali halihojiwi na Serikali, lakini likihoji mbona dawa hakuna linaambiwa lisichanganye dini na siasa

Pre GE2025 Askofu Bagonza: Kanisa likijenga Shule ama Hospitali halihojiwi na Serikali, lakini likihoji mbona dawa hakuna linaambiwa lisichanganye dini na siasa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Rwakatare alikuwa kiongozi wa kanisa na aligombea ubunge viti maalum ccm na alipata na hakujivua uongozi wa kanisa lake. Dini na Siasa
Mwamposa alipewa ubunge wa Kawe akiwa kiongozi wa kanisa, na hakujivua uongozi wa kanisa lake. Dini na Siasa.
Hii imekaaje?
Mkuu sio mwamposa ni gwajima
 
Dkt.Benson Bagonza Askofu wa KKKT Dayosisi ya Karagwe alikuwa akihojiwa na Mwanahabari nguli Jenerali Ulimwengu ambaye alimuuliza " Baba Askofu ningependa nikuulize, wewe umekuwa ukitoa mawazo yako hadharani juu ya masuala ya kisiasa huwa hakuna 'contradiction' kwamba unaingiza labda Siasa ndani ya Dini?..."

Askofu Dkt. Bagonza. “Mimi nadhani siasa ni uwanja wa watu wote lakini Dini ni uchaguzi wa mtu binafsi, Siasa ni yetu wote kwakuwa tunapiga kura, tunalipa kodi, ni yetu wote na sioni sababu ya mtu kumuwekea mtu mwenzake mipaka..." -

Aliongeza kusema, "Kwanini mnahoji kwamba nachanganya Dini na Siasa?, nikijenga Shule mbona hamsemi nachanganya Elimu na Dini?, nikijenga Hospitali mbona sihojiwi kwamba nachanganya Afya na Dini?, nikichimba kisima cha maji kwa wananchi mbona hawasemi kwamba unaingilia idara ya maji?..." -Askofu Dkt. Bagonza

"... nikimkuta mgonjwa pale nikampa dawa siulizwi kwanini unachanganya Dini na Siasa na hata sihojiwi kwanini unachanganya Afya na Dini lakini nikihoji kwanini mgonjwa huyu hana dawa?, kwanini serikali haileti dawa kwaajili ya mgonjwa wanasema aaah.., anachanganya Dini na Siasa, sasa huoni hapo kwamba kuna shida ya kimantiki?” -Askofu Dkt. Bagonza.
Huyu mpigaji tu. Ameenda ROMA ati kumsindikiza Cardnal Pengo kwa kisingizio kuwa ni MKARAGWE MWENZAKE.
 
Serikali makini isiyo na upigaji ya Rwanda imeweka taratibu halali kabisa za kielimu za nani anayefaa kuwa na kanisa na nani asiyefaa, Kagame anajiamini katika ufanisi wa utendaji kazi wa serikali yake na anakuwa na jeuri ya kuwawekea mipaka viongozi wa dini akijijua kuwa anao uwezo wa kutimiza wajibu wake.

Hapa Tanzania bado kuna ombwe la ufanisi wa serikali yetu upigaji ni mwingi sana na hiyo ni fursa ya viongozi wa dini kujihusisha na masuala mengi ya kijamii na mwishoni wanajiona wanayo haki ya msingi ya kushiriki maendeleo ya kila siku ya watu wanaosali makanisani mwao.

Kagame kuweza kuwa na sauti ya mwisho kwa taasisi za kidini ni kuona mbali kunakotokana na utashi wake wa kushughulika na masuala ya kijamii kuwa mkubwa na wa dhati kuliko walionao viongozi wetu.

Hata huo waraka uliosambazwa na maaskofu ni kwa sababu wanajua kuna ombwe katika ufanisi mzima wa kiserikali, wanatumia ushawishi wao wa kiroho walionao mbele ya waumini wakijua ubovu wa jamii zetu za kitanzania.

Tumejenga jamii ya hovyo sana na maaskofu wetu wanautumia ubovu huo kwa kuimarisha ushawishi wanaokuwa nao maishani mwetu.

Ukimwangalia Kagame kwa karibu kabisa si kiongozi bora hata koidogo.Kagame ni mfano wa kiongozi wa hovyo kabisa.Kagame anaamini katika kutawala yeye na si mtu mwingine.
Kagame ni mkabila upitiliza.
Kagame kawafanya wanyarwanda wote mazuzu.
 
Tanzania tuna demokrasia kwa wingi sana kipi cha maana tumeweza kufanya zaidi ya kila mtu kuishia kuongea maneno meengi ya malalamiko?.
 
Usipindishe. Ninamaanisha yeye aendelee na kazi yake ya uongozi wa kiroho na kazi za kisiasa awaachie wanasiasa.
Unaelewa maana ya siasa? Eleza japo kwa sentensi moja.
 
Labda Askofu Bagonza anatamani sana majukwaa ya kisiasa kuliko kutumikia wanakondoo wake. Aamue moja tu kama Padre wa zamani Dr Wilbroad Slaa, atoke madhabahuni aje apambane na akina Nape na Iddi Nondo.

Bagonza anajuwa kabisa kuwa Biblia imeandika:-
Mathayo 22:21 BHN
Wakamjibu, “Ni ya Kaisari.” Hapo Yesu akawaambia, “Basi, ya Kaisari mpeni Kaisari, na ya Mungu mpeni Mungu.”
Hujajibu hoja zake hata moja. Ya Kaisari mpe Kaisari nayo hujaipatia tafsiri yake, mfano kusimamia uchaguzi ni jukumu la serikali, dini ni wapiga kura tu hawasimamii, hapo ndio ya Kaisari umumpa Kaisari, lakini kujenga hospital ni jukumu la serikali na dini, hapo hakuna Cha Kaisari mpe Kaisari.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Wakati mwingine huwa tunafanya marejeo ya mistari ya biblia bila kujua ni nini kililengwa
 
Labda Askofu Bagonza anatamani sana majukwaa ya kisiasa kuliko kutumikia wanakondoo wake. Aamue moja tu kama Padre wa zamani Dr Wilbroad Slaa, atoke madhabahuni aje apambane na akina Nape na Iddi Nondo.

Bagonza anajuwa kabisa kuwa Biblia imeandika:-
Mathayo 22:21 BHN
Wakamjibu, “Ni ya Kaisari.” Hapo Yesu akawaambia, “Basi, ya Kaisari mpeni Kaisari, na ya Mungu mpeni Mungu.”
Hujui mandiko wewe nyamaza!

Kwa kifupi sana nisikie!

Watu wale wale wa Dini, wanapokuwa kwenye uwanja wa Kaisali, kaisali apewe vyake, na wanapokuwa kwenye uwanja wa Dini, heshima iende kwa Mungu!

Umejifunza nini hapo?
 
Unakurupuka kujibu wakati wewe ni mbumbumbu wa kuandika. Hakuna mtu kwenye Biblia anaitwa Kaisali. Labda huyo Kaisali ni wa kijijini kwenu
 
Shule si ni Biashara tu kama biashara nyingine. kwani wanasoma bure kwenye hizo shule.
 
Unakurupuka kujibu wakati wewe ni mbumbumbu wa kuandika. Hakuna mtu kwenye Biblia anaitwa Kaisali. Labda huyo Kaisali ni wa kijijini kwenu
Ume quote mandiko ya mtu mbumbu?? Wewe ni mjinga sana aisee
 
Back
Top Bottom